Mambo yanayoudhi humu jamvini

ni kero kubwa sana...mim hukerwa hata kwenye simu yananikwaza, kwanini mtu usiandike neno linaloeleweka. hayo maneno ya mkato mkato tuwaachie watoto wa shule wanataka kuonyesha kwa wenzao utaalamu na ujuzi wa kufupisha
dah inaboa sana
 
1.Mtu akipost thread hata kama ya msingi kuna baadhi ya members wanaigeuza kuwa genge la kunywa kahawa
mf:kupiga story tofauti na mada husika lengo la thread mpaka linapotea
2.Watu hawaheshimu mawazo ya watu;Mfano,ooh umepost upupu,unawaza kwa kutumia organ ya mwili,umetumwa e.t.c
3.Thread imenoga,jinsi unavyochangia ndo jinsi PM zinavyoingia mpaka browsing inaenda slow.
4.wengine wanatumia ufupisho wa ajabu mpaka unashindwa kuelewa,mf.sasa anaandika xaxa,sisi anaandika cc.
5.Huku ukieleza kuhusu facebook utapondwa ila 99% wanazo account za facebook.
6.Members wapya wanajua kila jukwaa,wanawajua members wa siku nyingi wanaochangia mada na mbinu za kuwafuatilia.
7.Mtu anapost thread halafu haonekani tena na hujui hata kama ameridhika na ushauri au majibu.
8.Watu wataponda kuhusu thread uliyopost but hawaachi kuchangia,kama wamelazimishwa vile kuponda wengine.
9.Kutafuta ban makusudi ili ujulikane humu

ongezea na mengine yanayokukera

10.Thread za wachovu na wasiofikiri wakiongozwa na Faizafoxy na group lake la magamb kama malaria sugu,Mwita25,Rejao nk
11.Mods kuunga threads ambazo wanadhani zina mahudhui yanayofanana wakati sometimes sio sahihi..
12.Watu kupost thread jukwaa lisilosawa mfano michezo kwenye jukwaa la siasa...
13.Watu wanaochangia kama mlevi..mfano "napita" nk
14.Sioni threads za kudai Tanganyika yetu,na zikianzishwa sijui kuna Mods Mzanzibar anazitupilia mbali au kuzificha...
 
Hizo points zote ni za kweli,ila hilo kundi huwa linapinga kila kitu hata iwe kwa manufaa ya umma,but Mwita ye ni mwelewa
sometimes
 
Ukikosa tu siku kadhaa mambo kibao yamekupita na update ya kupitia yalokupita yachosha sometimes....lol
 
Ukikosa tu siku kadhaa mambo kibao yamekupita na update ya kupitia yalokupita yachosha sometimes....lol
yakishakupita halafu uhondo unapungua coz wengi wameshachangia halafu unakosa kampan
 
penye wengi pana mengi bro!
hapa kuna watu wengi, na vituko ni vingi pia...na kero kama zako ulizoainisha hazikwepeki mahali hapa.
 
Kinachoniudhi mimi hapa JF ni baadhi ya watu kumuona J.K. Nyerere mtakatifu saaaaaana kiasi ambacho wengine hua wanakaribia ata kumpa sifa za uungu, na wengine hua wanadhani iwapo utamtaja kwa ubaya basi laana ya Mungu inaweza kukushukia na au eti huko kaburini aliko anapata habari!! Wacheni mawazo mgando kama haya, tambua hapa duniani Nyerere alikua binadamu sawa sawa na wewe na inawezekana huko aliko sasa wewe ukawa ni bora kuliko yeye.
 
Back
Top Bottom