Mama Mkwe Ndani ya JF

Mhhhh! Sijui kwanini hakuamua kukustua mapema mpaka ulipoandika hayo maneno kwenye rangi ya blue. Je, alijua siku nyingi lakini hakutaka kukwambia kwa kudhani kwamba unaweza kumzimikia mkweo hivyo ukawa ushahidi kwake kwamba hujatulia?

Wanajamii, nawaombeni kwa heshima na taadhima:

Humu JF kuna watu wa kada tofauti tofauti, na watu wa age tofautitofauti.

Nimekuwa nikichat na watu humu JF na kama mjuavyo tena humu hatufahamiani au kama ni kufahamiana ni kwa uchache sana. Mmoja kati ya watu ninaochat nao kila siku ni mama mkwe wangu. siri hii kanipa mke wangu kwani anaijua avatar ya mama yake anayoitumia, tena si avatar tu bali na password yake.

Siku moja nikapost kitu cha kumtania (mama mkwe ni mcheshi sana) akaniuliza kwani wewe una umri gani na kwanini unitanie? Akasema mimi ni mama yako ila napenda sana JF, inaburudisha na watu wana mawazo mengi tofauti na ukikaa ndani ya box bila kuelewa mambo.

Ki ukweli hakujua kama anayechat naye ni mkwe wake, ila ni mama mzuri sana.

Ushauri wangu kwa wana JF wenzangu: Unaweza kuchat na mtu au ukamtukana matusi ya nguoni kumbe ni baba yako, mama yako, au hata mke wako bila kujua. Na ndio maana kuna mwana JF mmoja alianzisha thread ihusuyo kufahamiana nani kaoa, nani bado, nani kapigwa ban na mwenzake nk, mimi nilijibu hivi: Thanda- I am the luckiest man on earth with happy marriage. Wife alipoiona hii akaamua kunitobolea siri kuwa huwa nachat na my inlaw.

Tuwe makini sana humu wapendwa!!
 
Dah!Kwa sisi tulio single raha sana,tunajiachia mpakaaa . . . . . . . !!

Is not all about thos who are commited but ni kwa wote kama upo single how about your mumy,sister,bro,hoja hapa ni kujiheshimu na kuheshimu usiwaona
 
Naona hapo aliona namjali kiasi gani na ndio maana akaamua kunieleza ukweli.
 
hukuwa na cha kupost?
Ndugu yangu Mansa, si kwamba sikuwa na cha kupost humu JF, nina mambo mengi ya kupost na hili ni moja kati ya mambo hayo....hii ni tahadhari tu kwamba humu tunakutana na watu wengi. Si kila kila humu JF kitakufurahisha ukikisoma ila kwa wenzako kama mimi ni faida kubwa sana....pliz naomba nielewe kwa hili
 
Ndugu yangu Mansa, si kwamba sikuwa na cha kupost humu JF, nina mambo mengi ya kupost na hili ni moja kati ya mambo hayo....hii ni tahadhari tu kwamba humu tunakutana na watu wengi. Si kila kila humu JF kitakufurahisha ukikisoma ila kwa wenzako kama mimi ni faida kubwa sana....pliz naomba nielewe kwa hili

taken watch that movie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom