Malumbano ya Spika Sitta na Mzee Mrema

Ok,hebu tuangalie mantiki za hoja zenyewe,je kisheria kweli Mrema hajakashifiwa?Maanke kumuita mtu Mhuni si ni kumdhalilisha?Sasa hapa kisheria haya madai ya Mrema yamekaaje?

Wanasisa wa Bongo sijui kwa nini wanapenda kuropoka namna hii,pia mtu wa kiwango cha sitta kutoa maneno kama hayo kwa mtu kama Mrema pia si ni tatizo?

Mrema pia nae aache kujitafutia umaarufu usio na maana
 
Hivi hizi heading za kupotosha nanmna hii zitatufikisha wapi.Yaani Bongo siku hizi ni ngumu kutenganisha magazeti ya habari rasmi na magazeti ya udaku

Kwenye hoja:

Wanasiasa wa tanzania hawaheshimiani,na kama hali ndiyo hii je wanaweza kumheshimu mwananchi wa kawaida,kuheshimu ahadi zao na pia kulinda heshima ya dhamana waliyopewa?
 
Mim ni mchaga, japo najinadi kama mtanzania. Kitendo chamrema kumuita spika Sita nimchochezi na anavuruga aman ya nchi nikama kujikomba kwa mrema kwa watu wenye fedha. Mim namlaani kwakutaka kuuchafuwa umma wa wa Tanzania na ninamuombea Mungu ikimpendeza Sita akaibuke kidedea kwa kumshinda ktk hyo Kesi. Sita ametenda mambo mazuri ktk hl taifa naasie ona ni kama marehemu. Mungu ibarik Tanzania, Mungu mbariki spika wa bunge la Jamuhur ya Tanzania.
 
Natamani sana Mrema afanye kweli baada ya siku hizo saba. Nina wasiwasi hata hivyo kama hiyo 37m aliyotutangazia juzi itatosha kumlipa Sitta gharama za kesi.
 
Ok,hebu tuangalie mantiki za hoja zenyewe,je kisheria kweli Mrema hajakashifiwa?Maanke kumuita mtu Mhuni si ni kumdhalilisha?Sasa hapa kisheria haya madai ya Mrema yamekaaje?

Wanasisa wa Bongo sijui kwa nini wanapenda kuropoka namna hii,pia mtu wa kiwango cha sitta kutoa maneno kama hayo kwa mtu kama Mrema pia si ni tatizo?

Mrema pia nae aache kujitafutia umaarufu usio na maana

Mkuu una pointi nzuri. Kwanza tujue maana ya neno mhuni na kama lina entail defamation. Na tuangalie ni vitendo gani vinaweza kufananishwa na na uhuni tuone kama kweli Mrema alistahili kuitwa hivyo, ay kama hakustahili kuitwa hivyo.

Tuangalie nani alizua mjadala na nani alijibu.

Kwa kumbukumbu zangu kuna wanasiasa wengi tu wamewahi kuitwa wahuni. Nakumbuka Mwalimu amewahi kuwaita wanasiasa kadhaa wahuni, sijui maana yake ilikuwa ni nini. Inawezekana Mrema amechoka na sasa amekubali kutumika ili walau awe kwenye kurasa za magazeti.
 
Mrema hana jipya nadhani kama wanavyosema wengi hapa anatafuta umaarufu kupitia kwa Sita na vyombo vya habari haya na tungoje hizo siku saba kama zamani alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.
 
1. Issue sio Mrema amesema au Sitta amejibu nini. Suala hapa ni kuwa wamesema nini!
Hizi siasa za maji taka, ambazo Sitta ni muongo na ni muhuni, Mrema ni muongo na ni muhuni.

Fact: wote Sitta na Mrema wanatumiwa na makundi maslahi ambayo wao wanayajua wenyewe kwa faida zao wenyewe.
Fact: wote wanataka sisi wananchi tuwashangilie wakati maigizo haya ni kwa faida zao.

Fact: wote ni watumishi wa dola ambao wameapa kuitumikia na kuilinda. Ila hili la siasa za maji taka silo waliotumwa na usalama wa taifa. Wanatumia siasa kumwonyesha mwajiri wao kuwa skills walizonazo. It is true that in the world of spionage your skills can be measured by the ability to create controversies. and if it is to name names, that will definately be Mrema and Sitta
Swali: tunapowasikiliza hawa mabwana, tunapima vipi akili au nia zao? Tunaweza kusema kuwa tunawajua hawa mabwana wapo kwa ajili ya nani?
Swali: Apart from these two gentlement stiring up our emotions, tusingependa waweze kuwajibika zaidi ya kutukasirisha au kutukera au kutufurahisha?

They are always playing with our emotions, they will always play with our emotions!
 
pix.gif

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema.

MWENYEKITI wa Chama chaTanzania Labour (TLP) amemtaka Spika wa Bunge, Samuel Sitta, amlipe fidia ya Sh bilioni moja ndani ya wiki moja kuanzia juzi, vinginevyo atamfungulia kesi ya madai Mahakama Kuu kwa kile anachodai kwamba amedhalilishwa...
Mrema amempa Sitta taarifa ya kusudio la kumfungulia kesi ya madai mahakamani endapo hatatimiza masharti ya kumfidia na kumwomba radhi.

Katika barua aliyoiandika juzi, Mrema amempa Sitta siku saba hadi Jumatatu ijayo, kutimiza masharti yake kabla ya kumfikisha mahakamani.

“Naomba kukufahamisha, kwamba ninakusudia kukufungulia kesi ya madai Mahakama Kuu ya Tanzania kutokana na wewe Mheshimiwa Sitta kunitukana, kunikashifu, kunivunjia heshima na kunidhalilisha kupitia magazetini,” inasema sehemu ya barua ya Mrema kwa Spika Sitta.

Barua hiyo inaendelea: “Vinginevyo, uniombe radhi kupitia magazeti yale yale na kwa uzito ule ule katika kipindi cha siku saba tangu utakapopokea barua hii; unilipe fidia ya Sh bilioni moja.”

Akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Pili, Mrema alikuwa na kawaida ya kutoa siku saba kwa wahusika kutekeleza maagizo yake kabla hajachukua hatua.

Alinukuu gazeti la Mwananchi la Machi 5 mwaka huu, ambalo lilimkariri Sitta akimwita Mrema mhuni na aliyepitwa na wakati, aliyefilisika kisiasa na kifedha na kwamba sasa anatafuta njia ya kujinasua kutoka hali hiyo.

Mrema anadai kwamba kauli hizo, akiwa Mwenyekiti wa Taifa wa TLP, zimesababisha wanachama wapatao 500,000 nchini wakose imani naye. Na pia kauli hizo anadai zimemvunjia heshima aliyojijengea kutokana na utumishi wake wa zaidi ya miaka 30 akiwa Ofisa Usalama wa Taifa, Mbunge, Waziri na Naibu Waziri Mkuu.

Alisisitiza: “Kauli zako zimeniathiri, kwa sababu nimeshajitangaza kugombea ubunge wa jimbo la Vunjo.

Hivyo kauli zako zinaweza kutumiwa na wapinzani wangu dhidi yangu.” Akizungumza na gazeti hili, Mrema alisema anaendelea na mchakato wa kuandaa mwanasheria atakayesimamia shauri lake.

Alisema Mahakama pekee ndiyo itakayotoa tafsiri halali kama Sitta alimdhalilisha au la. Gazeti hili lilimtafuta Spika Sitta kwa simu kwa lengo la kumuuliza kama amepokea taarifa ya Mrema, lakini simu yake haikupatikana.

Mazingira ya kutofautiana kati ya Spika Sitta na Mrema yamekuwa yakidhihirika kupitia vyombo vya habari.

Mrema aliitisha mkutano wa waandishi wa habari hivi karibuni na kudai kwamba Sitta ni mchochezi, mjenga makundi na mtu anayehatarisha amani na usalama wa nchi, kauli ambayo inadaiwa pia Spika aliijibu kupitia Mwananchi.

CHANZO: HABARILEO
 
Ok,hebu tuangalie mantiki za hoja zenyewe,je kisheria kweli Mrema hajakashifiwa?Maanke kumuita mtu Mhuni si ni kumdhalilisha?Sasa hapa kisheria haya madai ya Mrema yamekaaje?

Wanasisa wa Bongo sijui kwa nini wanapenda kuropoka namna hii,pia mtu wa kiwango cha sitta kutoa maneno kama hayo kwa mtu kama Mrema pia si ni tatizo?

Mrema pia nae aache kujitafutia umaarufu usio na maana
Kwa tafsiri ya neno Mhuni hata mimi nasema Mrema ni mhuni
 
whether i was right or wrong, once i doubted his credibility! And i still doubt. ..
 
Lakini kama umeisoma historia ya Six vizuri na ukailewa huna sababu ya kushangaa kwa haya yanayotokea sasa katika duru yake ya kisiasa.Huyu Mzee ni mgomvi, anayejiona yeye ni bora zaidi ya viongozi wenzake na mwenye kupenda sifa tena za kijinga.Sasa kama mambo yameongelewa tayari kwenye vikao vya NEC, sasa cha nini yeye kuyaongelea makasani? anachotafuta nini? Je huo ndo usafi na maadili ya viongozi wanaotakiwa Tanzania yetu ya sasa? lazima tujue jkuwa hapa kuna jambo na siyo bure, Absolutely anachokifanya Mrema ni sahihi kabisa, kama mtu anaharibu lazima aambiwe na siyo vinginevyo>
 
Back
Top Bottom