Malengo ya mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo(Comunity Development Catalyst Fund-CDCF)

Tatizo huwa tunawaumiza wabunge kwa kuomba watoe fedha kwa ajili ya maendeleo badala ya kuhamasisha maendeleo na shughuli nyingine za kibunge ndio maana na wabunge wa viti maalumu wanaomba fedha za mifuko ya jimbo ili wakifika majumbani (wanakotoka) wasikose cha kutoa
Hakuna lolote huo mfuko wa jimbo uko na maslahi binafsi ndio maana wanaulilia, wala siyo kama wanalilia ili watatue changamoto za kijamii
 
uwepo wa mfuko wa jimbo ni makosa na ni mhimili wa bunge kuingilia shughuli za utendaji za serikali.!

jukumu la mbunge ni kusimamia halmashauri inapotekeleza miradi ya maendeleo na sio kuwa sehemu ya utendaji kwa kugawa fedha bila kuwa na vigezo maalum.

Fedha hizi zimekuwa zikigawanywa kisiasa kwa eneo mb anakubalika na maeneo mengine yakiachwa, ndio maana wenzao viti maalum wanaona nao wanahaki ya kupata.

Napendeleza kufutwa kwa huu unaoitwa mfuko wa maendeleo ya jimbo na fedha hizi zielekezwe katika vyanzo vingine vya ruzuku zinazopelekwa halmashauri na Mbunge abaki na jukumu lake la msingi la kuhamasisha maendeleo, kusimamia serikali na kutunga sheria.
 
Ndugu wana JF leo kumetokea mvutano kati ya baadhi ya wabunge wenye majimbo na wale wasio na majimbo wang'ang'aniana fedha za mfuko wa jimbo.
Wabunge wasio na majimbo wanazitaka hizo fedha wapewe wakati hawana majimbo.
Hoja hiyo imeniachia maswali mengi imenibidi nilete maswali hayo tujadiliana.
>Kwa nini wabunge wasio na majimbo watake kupewa hizo fedha?
>Je inawezekana hizo fedha zinapigwa na wabunge bila kuwafikia wanajimbo?
>Je hiyo sheria ya fedha za jimbo ifutwe?
>Rais aache kutoa fedha za mfuko wa jimbo?
>Huko jimboni kwako unafahamu fedha hizo zimefanya shughuli zipi?
 
Hizi nafasi za ubunge wa upendeleo huwa nazichukia sana maana hazina faida kwa taifa zaidi ya hasara, hizi nafasi zinapaswa zifutiliwe mbali kabisa na katiba ya nchi maana ni upuuzi mtupu
Hata Mimi huwa nawaza wazifute wabaki wa majimboni tu
 
uwepo wa mfuko wa jimbo ni makosa na ni mhimili wa bunge kuingilia shughuli za utendaji za serikali.!

jukumu la mbunge ni kusimamia halmashauri inapotekeleza miradi ya maendeleo na sio kuwa sehemu ya utendaji kwa kugawa fedha bila kuwa na vigezo maalum.

Fedha hizi zimekuwa zikigawanywa kisiasa kwa eneo mb anakubalika na maeneo mengine yakiachwa, ndio maana wenzao viti maalum wanaona nao wanahaki ya kupata.

Napendeleza kufutwa kwa huu unaoitwa mfuko wa maendeleo ya jimbo na fedha hizi zielekezwe katika vyanzo vingine vya ruzuku zinazopelekwa halmashauri na Mbunge abaki na jukumu lake la msingi la kuhamasisha maendeleo, kusimamia serikali na kutunga sheria.
Nimefurahia mchango wako maana kuna ukweli wabunge wanapendelea kuzielekeza maeneo Fulani Fulani tu kwa watu waliokaribu naye.
 
Sasa mbunge mnamwalika kuzindua album ya kwaya ananunua CD kwa mill 30 unafikr anazitoa wapi?

Ila kipindi cha magu sijaona hizo show off?
 
uwepo wa mfuko wa jimbo ni makosa na ni mhimili wa bunge kuingilia shughuli za utendaji za serikali.!

jukumu la mbunge ni kusimamia halmashauri inapotekeleza miradi ya maendeleo na sio kuwa sehemu ya utendaji kwa kugawa fedha bila kuwa na vigezo maalum.

Fedha hizi zimekuwa zikigawanywa kisiasa kwa eneo mb anakubalika na maeneo mengine yakiachwa, ndio maana wenzao viti maalum wanaona nao wanahaki ya kupata.

Napendeleza kufutwa kwa huu unaoitwa mfuko wa maendeleo ya jimbo na fedha hizi zielekezwe katika vyanzo vingine vya ruzuku zinazopelekwa halmashauri na Mbunge abaki na jukumu lake la msingi la kuhamasisha maendeleo, kusimamia serikali na kutunga sheria.
  • Naunga mkono hoja, bora wafute huo upuuzi then hizo pesa waziongezee halmashauri
 
Harafu mbaya zaidi hata uko majimboni hatuwaoni karibu hata miezi 7 unabaki kujiuliza hizo hela hua zinatumika wapi.
 
Ivi kazi za mfuko wa jimbo ni nini??? na Je ishu ya mfuko wa jimbo ipo kisheria???? na kwenye hiyo sheria zimebainishwa bayana kuwa kazi za pesa wa mfuko wa jimbo ni zipi????
 
29026181_965973646911935_6027479090514036228_n.jpg
 
Ivi kazi za mifuko ya jimbo ni nini??? tunatakiwa kujua maana ni hela za walipa kodi. Pili ivi hii mifuko ya jimbo huwaga inafanyiwa Auditing yoyote ile na ofisi ya CAG??? Na je hii mifuko ipo kisheria???
 
YAFAHAMU MALENGO YA MFUKO WA JIMBO.
Mfuko wa jimbo ni mfuko ulianzishwa kisheria na ulipitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na lengo kuu la kupitishwa kwa mfuko huo ni kuchochea na kuongeza kasi katika miradi mbali mbali iliyoanzishwa na wananchi katika majimbo yao (The Constituencies Development Catalyst Fund Act. Na. 16 ya mwaka 2009)

Kama ilivyoahinishwa hapo juu lengo la kuanzishwa kwa mfuko huu ni kuchochea maendeleo katika majimbo ya uchaguzi. Ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo ufanyika kwa juhudi za wananchi wakishirikiana na mbunge wao, pamoja na serikali kuu kama mchochezi mkuu anayetoa pesa husika.

Serikali kupitia bunge tukufu ilifanya hivi hili kurahisisha maendeleo kwa kasi katika majimbo husika; ikiamini kuwa kwa kuwa mbunge yupo karibu na wapiga kura wake itamuwia rahisi kutekeleza maendeleo hayo japo, maskini serikali haikujua kuwa asilimia kubwa ya wabunge wetu wanaishi mbali na sisi na huwa tunaonana nao kipindi cha kuomba tena ridhaa yetu.

Kama wengi wasemavyo kuwa "ukitaka kupima utu wa mtu mwangalie katika mambo mawili PESA na CHAKULA" mara nyingi pesa hizi zimekuwa hazifahamiki matumizi yake hasa baada ya serikali kuzitoa. Kunakuwa hakuna ufuatilia wa kina juu ya matumizi yake; jambo ambalo limekuwa faida kwa wabunge.

Utaratibu unasema kuwa pesa hizi za mfuko wa maendeleo ya jimbo (CDF) hupewa kwa kila mbunge wa jimbo na huwabagua wabunge wa viti maalumu na wale wabunge wa kuteuliwa na Rais.

Mfuko huu hudhibitiwa na kamati maalumu ya watu sita (6) kama sikosei ambao wote huteuliwa na mbunge husika ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa mfuko huo. Kamati hii hukoma pale mbunge husika anapokoma kuwa mbunge kwa kushindwa ubunge, kung'olewa na mahakama au kifo.

Mbunge na kamati yake ndiyo wenye kauli ya mwisho juu ya matumizi ya pesa za mfuko huu na si lazima matumizi hayo yaende sambamba au yawiane na vipaumbele vya halmashauri ya mji,wilaya au manispaa.

Wabunge wa viti maalumu wanataka pia kupewa pesa za CDF kwa madai kwamba wana majukumu sawa au hata kupita yale ya wabunge wa majimbo. Kabla ya kufikiria kuwajumuisha wabunge wa viti maalumu na wale wa kuteuliwa na Rais katika kupata fedha za mfuko wa jimbo ni vema ukaguzi na upembuzi ufanyike kwanza ili kubaini manufaa ambayo yameletwa na mfuko huu kama yapo.

Ushirikishwaji wa wananchi katika hili umekuwa haufahamiki, ajabu ukijaribu kuwahoji hata baadhi ya madiwani katika halmashauri zetu mbalimbali hawajui huwepo wa pesa hizi na kama wanajua hawafuatilii matumizi ya pesa hizi.

Miradi mingi ya wananchi inakwama kwasababu ya kukosa kichocheo muhimu kama hichi ambacho serikali iliona umuhimu wake ila ikasahau kufuatilia utekelezaji wake.

Suhala la shule kutokuwa na huduma bora zinazopaswa hupelekea wanafunzi wengi wa sekondari kukata tamaa na kuacha shule kabisa ama kupata matokeo mabaya mwishoni. Lakini ukiwasikiliza watu hawa wana moyo na hali yakujitoa ila support ya viongozi husika inakuwa ndogo! Mfuko wa jimbo na ubunifu wa viongozi wetu ukitumika tunaweza kutatua tatizo hili maana naamini inawezekana sana.

Wabunge wengi wa majimbo ukitaka kugombana nao wahulize kuhusu pesa za mfuko wa jimbo. Kijana mmoja aliwahi kumhoji mbunge wake lakini alichojibiwa hakikuwa kizuri kwa ustawi wa uwajibikaji kwa wananchi waliomchagua.

Mara nyingi wabunge wetu wakitumia pesa za jimbo katika shughuli ndogo za kijamii ujinasibu kuwa hizo ni pesa zao wenyewe toka mfukoni mwao, wanatumia mihanya hiyo ya wananchi kutojua ukweli wa jambo hili.

Hivyo uzitumia pesa husika kujihimarisha kisiasa, ndiyo maana wanaharakati wengi wamekuwa wakiishauri serikali kufuta sheria hiyo na kuondosha hii mifuko ya jimbo kwani imeonekana ilianzishwa kwa lengo zuri ila usimamizi na utekelezaji wake hauleti hali chanya kwa walengwa.

Ukiangalia kwa mfano Mgawanyo wa Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo 2010/2011 majimbo kama kielelezo kwenye picha kinavyoonesha yalipata pesa nyingi tu lakini nani anaweza kujua zilitumikaje katika majimbo yetu?

WITO WANGU KWA WANANCHI, baada ya kutambua matumizi na malengo ya pesa za jimbo tuanzishe miradi mbalimbali na tuwashirikishe wabunge wetu na wakigoma kutusupport tuwahoji hizi pesa zilitumika kwa matumizi gani?

Yamkini viongozi wetu (wabunge) wamejisahau sasa tuwakumbushe kwa kuanzisha miradi mbalimbali na kutaka mchango wao toka mfuko wa jimbo.

ANDIKO HILI LINALENGA KUEMILIKISHA JAMII JUU YA SHERIA YA MFUKO WA JIMBO NA MALENGO YAKE.
 
Hivi CAG alisemaje kuhusu ruzuku ya chadema
Mimi sio mwanasiasa na ndiyoy maana siongelei chama chochote. Naongelea mtu kama mtu ambaye ni mwakilishi wa wananchi. Nia ya andiko hili ni kuchochea kasi ya maendeleo kwa wananchi. Watambue hela zao zilipo na wazidai kwa utaratibu. Wasipopewa hela zao .. waachane na huyo mwakilishi wao anayewapora haki zao.
Ni muda muafaka sasa wa kutoa elimu hiyo kwa sababu mwakani tutaanza kuwaona wakija na mbwembwe kuonesha kuwa tuko nao kwenye majimbo.

Nakumbuka kipindi fulani mbunge wa jimbo la nyumbani alilia jukwaani baada ya vijana kumuuliza maswali magumu yaliyomshinda kujibu.
Aliulizwa hivi...
Ndugu Mheshimiwa ni miaka minne sasa hatukuoni jimboni kwetu bali tunaona gari jeusi likipita kwa kasi ya ajabu kuelekea nyumbani kwa mama yako. Marafiki zako wanakutetea eti unaogopa vumbi. Swali .. Mbona vumbi la leo hujaliogopa umesimama tena kuomba kura?
 
Hakuna cha mfuko wala nini, Utakuaje na mfuko ndani ya mfuko? wabunge wapo jimboni na ajimboni kuna serekali kuu na serekali ya zamitaa. hizo ni Bonus za wabunge, Catalyst for increasing women.

Wabunbe walianzisha kwa ajili ya kuswasaidia wanao lia lia, mara misiba, mara wau wenye matatizo. Hayo ni marupurupu ya wabunge. Hakuna kinacho fanyika huku majimboni sisi si tupo huku. Serekali kuu ipo, serekali ya mitaa ipo, na mfuko wa maendeleo ungeuwepo kama Tanzania ipo mbali sana. But cha kushangaza mifuko ipo but nothing is being done at all.

Labda mfuko ubadirishwe jina, uitwe The Constituencies Development Catalyst Fund For MPs luxuries . Ukitaka kujua haya nenda Dodoma hotel au pale Makole kwenye mida ya saa 3 au saa 4 usiku ndo utajua maan ya mfuko wa jimbo. Hizi sheria zinatungwa kwa nia njema sometimes, but mara nyingi kuna kitu kinajificha nyuma ya pazia. nisawa na sha=eria ya mifuko ya jamii. wameunganisha mifuko ili wachote vizuri pesa za waastafu. waliona watu wakijitoa itakua sooo kwa viongozi wa nchi kwa hiyo ni bora wapitishe sheria na wafute fao la kujitoa ili chama kiendelee kuchota.
 
Ni vema ukafanya utafiti wa kufahamu mfuko wa jimbo hupokea kiasi gani? halafu njoo na hoja zako!!
 
WIZI MTUPU MKUU
 
Back
Top Bottom