Jimbo la Kiteto: Fedha za Mfuko wa Jimbo kwaajili ya Kuchochea Maendeleo ya Miradi ya Wananchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943
Ndugu wananchi wenzangu wa Jimbo la Kiteto nachukua fursa hii kuwatakia Kheri ya Mwaka Mpya 2024. Namwomba Mwenyezi Mungu awape Baraka, Afya Njema na Neema katika mwaka huu 2024.​

Ndugu wananchi wenzangu baada ya salama za Mwaka Mpya napenda kuwafahamisha kuwa Kamati ya Mfuko wa Jimbo (Mfuko wa Mbunge) ambayo Mkiti ni Mbunge iliyoketi tarehe 28. 12. 2023 iliweza kujadilia maombi ya miradi ya wananchi kutoka Kata Kumi na Mbili ( 12) na baada ya kikao kamati ilitenga fedha katika miradi hiyo kwa mchanganuo kama ifuatavyo;

1. Pesa kwaajili ya Umaliziaji wa Vyumba 2 vya Madarasa Shule ya Msingi Ngarenaro Kata ya Kibaya kiasi cha Shs 5,000,000,

2. Pesa kwaajili ya utengenezaji wa madawati Shule ya Msingi Kaloleni Kata ya Kaloleni kiasi cha Shs 5,000,000

3. Pesa kwaajili ya Umaliziaji wa Vyumba 2 vya Madarasa Shule ya Msingi Malimogo Kata ya Lengatei kiasi cha Shs 6,000,000

4. Pesa kwaajili ya Ujenzi wa Soko la Sunya Kata ya Sunya kiasi cha Shs 10,000,000

5. Pesa kwaajili ya Utengenezaji Viti na Meza Shule ya Msingi Mbeli Kata ya Partimbo kiasi cha Shs 5,000,000

6. Pesa kwaajili ya Upauzi wa Vyumba 2 Vya Madarasa Shule ya Msingi Osteti Kata ya Chapakazi kiasi cha Shs 6,000,000

7. Pesa kwaajili ya Umaliziaji wa Nyumba ya Daktari Zahanati ya Ndaleta Kata Njoro kiasi cha Shs 6,000,000

8. Pesa kwaajili ya Utengenezaji wa Madawati Shule ya Msingi Ngabolo Kata Ndedo kiasi cha Shs 5,000,000

9. Pesa kwaajili ya Ukamilishwaji wa Ujenzi Madarasa 2 Shule Msingi Oloimug'i Kata Namelock kiasi cha Shs 6,000,000

10. Pesa kwaajili ya Ukamilishwaji wa Ujenzi Nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Kiteto Kata ya Laiseri kiasi cha Shs 6,000,000

11 . Pesa kwaajili ya Upauzi wa Nyumba ya Daktari Zahanati ya Nchinila Kata Dosidosi kiasi cha Shs 6,584,000

12. Pesa kwaajili ya umaliziaji wa Nyumba ya Waalimu Shule ya Msingi Lembapuli Kata Loolera kiasi cha Shs 5,000,000
Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Kiteto, Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa kuendelea kuboresha maisha yetu Wana Kiteto kwa kuendelea kutuletea miradi mikubwa ya maendeleo na kushughulia changamoto za wananchi katika wilaya yetu. Ahadi za CCM zinaendelea kutekelezwa.

Ndugu wananchi wenzangu wa Kiteto tunayo kila sababu ya kutoa shukuran kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupa fedha nyingi kwaajili ya kutatua miradi ya Maendeleo. Tumwombe Mhe. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Mwenyezi Mungu ampe Afya Njema na kumlinda vyema ili aendelee na maono yake mazuri katika Kujenga Taifa Letu.

Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kusikia kilio chetu kupitia sauti yenu Bungeni.

Ndugu wananchi wenzangu kwa dhati kabisa nawahakikishia kuwa nitaendelea kuwa sauti yenu Bungeni na kuwawakilisha ipasavyo kwa unyenyekevu na uaminifu mkubwa.

MUHIMU: Natoa wito kwa watumishi wote na viongozi ngazi za Vijiji na Kata kuhakikisha kuwa miradi hii inasimamiwa vizuri na kwa ufanisi mkubwa ili wananchi wapate huduma hizi kwa wakati.

Kiteto yetu inaendelea Kung'ara

Mungu Ibariki Kiteto!

Mungu Ibariki Tanzania !

Mungu ambariki Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge

Edward Ole Lekaita Kisau (Mbunge wa Jimbo la Kiteto)

Leo tarehe 1. 1. 2024

Kazi Iendelee
 

Attachments

  • UntitledKMJUI.jpg
    UntitledKMJUI.jpg
    6.8 KB · Views: 2
  • ksXHLeUw_400x400.jpg
    ksXHLeUw_400x400.jpg
    13.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom