Malengo ya Elimu ya Tanzania ni mawili, 1. Tunasoma ili tufaulu mitihani, 2. Tunasoma ili tuajiriwe. Njoo ubishe kwa hoja

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,716
36,187
Habari!

Ikiwa ndugu, mtoto au rafiki kakupigia simu kisha akasema nilikuwa nawasalimia tu lakini baadaye akaanza kujichekesha na kuomba elfu tano hiyo maana yake ni kwamba lengo la kukupigia halikuwa kuwajulia salamu bali kuomba pesa .

Vivyo hivyo lengo la Elimu ya Tanzania ni kujenga Taifa la kujitegemea, lenye nguvukazi bora yenye ujuzi na maarifa. Lakini UKWELI ni kwamba Tanzania tunasoma kwa malengo mawili hasa;

1. Kufaulu
Serikali na viongozi hufurahi matokea ya kidato cha 4,6 au std 7 yanapokuwa mazuri kuliko mwaka uliopita.
Maafisa Elimu wa mikoa iliyofanya vizuri kwenye makaratasi ya watoto hujionea fahari na wengine hupandishwa vyeo, wakuu wa shule hupandishwa vyeo na wadhifa.
Hapa biashara huishia hapo bila kuangalia jamii itafaidika nini na passes za hao waliofaulu. Au huyo aliyefaulu atanufaika nini na matokeo yake mazuri.
Kwa hali hii basi ili kulinda wadhifa kila mkuu wa shule anahakikisha iwe mvua au jua shule yake isiwe mkiani kwenye matokeo ya kitaifa, mkoa, wilaya au kata. Hapa ndipo unakuja kushangaa mwanafunzi wa kidato cha kwanza (selected) hata kuandika au kuongea Kiswahili fasaha hajui.

2. Kuajiriwa.
Hili lengo hasa limeegemea kwa wazazi na wanafunzi.
Kwanini mzazi humwekea sana bidii mtoto anapokuwa kwenye madarasa ya mitihani kuliko anapokuwa madarasa mengine?
Lengo ni mtoto afaulu aajiriwe .
Darasa la sita lina masomo msingi yote lakini mzazi huweka msisitizo mkubwa kwa mwanae anapokuwa darasa la 7 kuliko la sita.

Sababu hizo mbili hapo juu ndizo huzalisha wasomi wa hovyo kwa kuendekeza Cheating.
Katika mambo ambayo nayachukia duniani ni cheating (udanganyifu) kwenye vyumba vya mitihani .
Kama likizo hakuna basi iwe kwa wanafunzi wote kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita, wote wanatakiwa wapate elimu bora, na kila darasa lina mwongozo wa masomo kwa muhula au mwaka wote.
Watakaomaliza masomo Katika muhula husika ndio wafunge shule waende likizo.

USHAURI
MADA zote zifanyiwe utafiti, kama hazijawahi kuleta tija kwenye maisha ya uhalisia zifutwe. Ni mzigo.
 
images (3).jpeg
 
Back
Top Bottom