Malecela Vs Kikwete

Kuna njia nyingi za kuendeleza jimbo pasipo kutegemea fedha za serikali. Ina takiwa mbunge awe na initiative, awe creative na awe na vision. Ukikaa kusubiria pesa za serikali tu ndipo hapo inabidi mbunge asubiria mpaka apate uwaziri. Pia wabunge wengi wa CCM wange punguza uchama na kukazania kutetea maslahi ya majimbo yao zaidi kunge kuwa na maendeleo. Tatizo wabunge wengi (haswa wa CCM) ni rubber stamps tu.

ebu toa mifano hai kivipi mbunge anaweza kuendeleza jimbo bila fedha kutoka seriali kwenda jimboni kwani.? Au unamaanisha maendeleo ya kisiasa.


Mi nadhani watu wanakosea kuhusiha maendeleoya jimbo na wabunge. Wabunge ni wanasiasa tu.

Maendeleo ya jimbo Mkoa au wilaya sana sana yanategemea RC DC, Afisa Elimu, Afisa MAdini. RPC, Afisa Mifugo au Afisa Kilimo. Hwa ndio watu wanaotakiwa kuwa front line kuleta maendeleo
sio wabunge. wabunge ni politics tu
 
Nadhani hatutawatendea haki wote wawili kuwapima kwa vigezo vya Urais wakati mmoja amepata nafasi na kuwa Rais tukaona uwezo wake dhahiri na mwingine hakupata nafasi ya kuonyesha uwezo wake. Kupima kuzuri ni kulinganisha pale ambapo kuna uwiano ambao unaweza kutumika ushahidi bila upendeleo.

Nawashauri kwanza muwapime uwezo wao na nia zao njema kwa Taifa hili kwa kulinganisha matukio katika mwaka 1995 na 2005 wakati na kabla ya uteuzi wa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, kwa muono wangu hapo tutapata 'level ground' ya kuweka mizani yetu.
 
we una mawazo ya ubinafsi. Kiongozi mzuri haangalii analifanyia nini jimbo lake anaangalia priorities za nchi. Ukitaka alifanyie nini jimbo lake, kesho utauliza mbona hakufanya chochote kijijini kwake, kesho kutwa utaliza amefanyia nini mtaa wake. Huo ni ubinafsi mkubwa kama wa Magufuli kupindisha barabara ili ipite kijijini kwake. Huyo huyo akataka makao makuu ya mkoa wa Geita yawe kwao Chato badala ya Geita. Huo ni mfano halisi wa ubinafsi.

Sasa priorities za Malecela kwa nchi zilikuwa zipi?Kubadilisha wake?Kuwatukana Watanzania kuwa they could go to hell?Kujenga gereza la kunyongea Isanga au kuelta hospitali ya vichaa Mirembe?
 
Hakuna mwema hapo ondoeni utashi,
oll are dusts,chela anatetea nin?na anakemea baya gani?
 
John angetusilimisha watanzania wote, maana alitaka urais kwa kusilimu.

Nimewai kusikia lakini sina ushahidi wowote ni aibu kubwa sana,

Huyu Mzee amekaa Bungeni Miaka mingi sana lakini sijawai kusikia hata siku moja akiongea lolote jambo la kutetea Umma wa Watanzani labda kama kuna mtu ana kumbukumbu anaweza kuweka hapa JF, hasa Bunge la 1995 hadi 2010 (15 years).

Vipi jitihada za kuleta Tanganyika wakati akiwa Waziri Mkuu au yeye hakujua lolote!

Naungana na wanaosema wote wawili ni zero.
 
huwe kumpima mtu kwa kuangalia jimboni kafanya nini, nadhani hata kikwete hakuchaguliwa kazi alizofanya chalinze,
mtela hapakuweza kuboreshwa si kwa kuwa malechele hakufanya kazi, ni kwa kuwa eneo hilo halikuwa katika mipango ya serikali, kama ambavyo barabara ya kwenda nyumbani kwa mwl,nadhani bado haina lami mpaka sasa

Mkuu usimlinganishe Mwl na hao wote, Barabara ya kwenda kwake huenda baba alitaka kutojirundikia kama Mkulu wetu sasa anavyofanya, angalia Mama Salma na uvujaji wa mali zetu halafu linganisha na Mama wa Taifa..
 
Kuna njia nyingi za kuendeleza jimbo pasipo kutegemea fedha za serikali. Ina takiwa mbunge awe na initiative, awe creative na awe na vision. Ukikaa kusubiria pesa za serikali tu ndipo hapo inabidi mbunge asubiria mpaka apate uwaziri. Pia wabunge wengi wa CCM wange punguza uchama na kukazania kutetea maslahi ya majimbo yao zaidi kunge kuwa na maendeleo. Tatizo wabunge wengi (haswa wa CCM) ni rubber stamps tu.
Duh mkuu wangu mimi sijawahi kusikia Mbunge asiyetegemea fedha za serikali. Yaani hilo ulosema ndio kubinafsisha nchi!..na ndio hatari kubwa sana ya siasa za Tanzania kutegemea mbunge atumie mfuko wake kutimiza ahadi zake. Maana ya ahadi za mbunge Tanzania, ni uwezo wa mbunge kuyatimiza aloahidi kutoka mfukoni mwake.. No wonder Lowassa, Rostam na kina Change wataendelea kushinda ktk majimbo yao..
 
Tatizo hapa sio mgombea yupi angefaa ila ni mfumo mzima wa kumpata na kumpitisha kuwa mgombea wa chama . Hapa panahitaji pesa ya kutosha kufikia hapo, hiyo ndio jinsi hali ilivyo ndani ya CCM .Kwa mantiki hiyo unakuta mtu anaweza kuwa anasifa zote za kuwa kiongozi mzuri lakini bila pesa hapitishwi. Hapo sasa ndipo wanapotokea wafadhili na kukuwezesha ili uingie ikulu . Baada ya kuingia sasa Ikulu ndio mchezo unakuwa kama ligi ilivyo sasa.
 
huyu malecela hafai kwa data zifuatazo dodoma maendeleo aliyofanya ni kujenga gereza la kunyongea watu tulipo lalamika akatujengea hospitali vichaa mirembe akidai sisi ni vichaa huyu hafai ndio mana hata ubunge kakosa
Lakini hao wafungwa na wagonjwa wa akili wanaowekwa huko hawatoki Dodoma tu, wapo hadi wakutoka huku kwetu.
 
Articulate kitu gani. Alibadili na dini ili apate misaada ya waarabu awe Rais. Huyu mzee sindio Mwalimu aliemrefere kama 'ukoma' wa kuogopwa. Watu wanaotaka kuingia ikulu kwa gharama yoyote. Nae hovyo tuu.
 
Vipi Salim je? Ukizingatia ufahamu wake wa mifumo ya utawala katika nchi nyingine
 
Back
Top Bottom