Malecela Vs Kikwete

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,544
19,399
Pamoja na mapungufu yake mengineyo, lakini Malecela nadhani alikuwa more articulate katika mambo yake mengi kuliko Kikwete ambaye anaropoka mambo bila ya kuwa na uhakika nayo. Je kama tungemchagua Malecela mwaka 2005 ingekuwaje leo? Naweza kuwa najaribu kupima baina ya the bad and the worse, lakini nadhani kuwa sasa hivi tuna void katika uongozi
 
My own observations

Hali ingekuwa mbaya zaidi huenda hata nchi ingekuwa imebinafsishwa Kama si kuuzwa kabisa. Hakuna unafuu hapo, ngoja nimeze kabisa panadol.
 
Unafuu ungekuwepo angalau mambo yangekuwa yanafanyiwa uchambuzi wa kina na wakitalaam kabla ya utekelezaji. Tofauti na alivyo kikwete, Malecela siyo mbishi na mtu anayejifanya kujua kila kitu. Hana majivuno wala tabia ya kulipa visasi. Ni mwelewa na mshirikishaji na ana uzoefu wa muda mrefu. Unafuu ungekuwepo tena mkubwa tu. Kwa ufupi ni kwamba nchi hii haitakuja iongozwe tena na rais mbumbumbu na mswahili kama sasa. Watanzania tumejifunza mengi sana kupitia kikwete kwamba linapokuja suala la uchaguzi wa rais hatutakiwi kufanya mzaha kamwe. Kwa hilo tunamshukuru kikwete.

.
 
Pamoja na mapungufu yake mengineyo, lakini Malecela nadhani alikuwa more articulate katika mambo yake mengi kuliko Kikwete ambaye anaropoka mambo bila ya kuwa na uhakika nayo. Je kama tungemchagua Malecela mwaka 2005 ingekuwaje leo? Naweza kuwa najaribu kupima baina ya the bad and the worse, lakini nadhani kuwa sasa hivi tuna void katika uongozi

it could be a big mess.

after nyerere, no better president would come from ccm again
 
Mmmmh,tembelea jimbo lake la zaman la malecela liitwalo MTERA then ndo utampima mheshimiwa CHELA
 
Mmmmh,tembelea jimbo lake la zaman la malecela liitwalo MTERA then ndo utampima mheshimiwa CHELA
huwe kumpima mtu kwa kuangalia jimboni kafanya nini, nadhani hata kikwete hakuchaguliwa kazi alizofanya chalinze,
mtela hapakuweza kuboreshwa si kwa kuwa malechele hakufanya kazi, ni kwa kuwa eneo hilo halikuwa katika mipango ya serikali, kama ambavyo barabara ya kwenda nyumbani kwa mwl,nadhani bado haina lami mpaka sasa
 
Kuna njia nyingi za kuendeleza jimbo pasipo kutegemea fedha za serikali. Ina takiwa mbunge awe na initiative, awe creative na awe na vision. Ukikaa kusubiria pesa za serikali tu ndipo hapo inabidi mbunge asubiria mpaka apate uwaziri. Pia wabunge wengi wa CCM wange punguza uchama na kukazania kutetea maslahi ya majimbo yao zaidi kunge kuwa na maendeleo. Tatizo wabunge wengi (haswa wa CCM) ni rubber stamps tu.
 
huwe kumpima mtu kwa kuangalia jimboni kafanya nini, nadhani hata kikwete hakuchaguliwa kazi alizofanya chalinze,
mtela hapakuweza kuboreshwa si kwa kuwa malechele hakufanya kazi, ni kwa kuwa eneo hilo halikuwa katika mipango ya serikali, kama ambavyo barabara ya kwenda nyumbani kwa mwl,nadhani bado haina lami mpaka sasa

wewe andrew unaongea nn?malecela alikua wazir mkuu,ndie aliyekua serikalin lakin aliwapuuza wagogo wenzake,sasa kama jimbo linamshinda je nchi ataiweza?sasa kama kipimo kidogo hicho kashindwa kukisaidia je hicho kikubwa,nenda Mtama kwa membe hata maji anashindwa kuweka halaf ndo awe rais?kila siku yupo daaar je akiwa rais si ndio kila siku atakua angan kama MJOMBA
 
Tanzania sasa inaongozwa vibaya kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi hii, vibaya kuliko hata kipindi cha kikoloni, wakoloni walikuwa anabagua watu kwa rangi zao, leo kuna ubaguzi mkubwa zaidi hata ya ule wa mkoloni, Rushwa is so rampant, hakuna haki tena.

Sidhani kama Tanzania itakuja kuwa na kiongozi mbovu zaidi wa aliyepo sasa sio kwa sababu watanzania sasa wamejifunza laa hasha ila ni kwa sababu hakuna kiongozi mbovu zaidi wa huyu wa sasa, he the worst Leader the world have ever had
 
huyu malecela hafai kwa data zifuatazo dodoma maendeleo aliyofanya ni kujenga gereza la kunyongea watu tulipo lalamika akatujengea hospitali vichaa mirembe akidai sisi ni vichaa huyu hafai ndio mana hata ubunge kakosa
 
huyu mzee kasema watu wa dodoma wamejengewa vyuo ili wauze vyakula kwenye maeneo ya chuo pia amesema kuwa siku hizi guest zinajaa sana baada kujegwa vyuo kwa hiyo yeye anasapoti uzinzi jk yeye anapenda ngoma kwa hiyo ana afazali kidogo
 
huyu malecela hafai kwa data zifuatazo dodoma maendeleo aliyofanya ni kujenga gereza la kunyongea watu tulipo lalamika akatujengea hospitali vichaa mirembe akidai sisi ni vichaa huyu hafai ndio mana hata ubunge kakosa

Loh! Hii nilikuwa siijui, kama ni kweli POLE ZENU WANA IDODOMYA.
 
mimi nahisi kama malecela angekuwa dikteta,sababu huyu babu hana kiasi(self control) majazba kibao tena hana uhusiano mzuri na baadhi ya wanahabari
 
wewe andrew unaongea nn?malecela alikua wazir mkuu,ndie aliyekua serikalin lakin aliwapuuza wagogo wenzake,sasa kama jimbo linamshinda je nchi ataiweza?sasa kama kipimo kidogo hicho kashindwa kukisaidia je hicho kikubwa,nenda Mtama kwa membe hata maji anashindwa kuweka halaf ndo awe rais?kila siku yupo daaar je akiwa rais si ndio kila siku atakua angan kama MJOMBA
we una mawazo ya ubinafsi. Kiongozi mzuri haangalii analifanyia nini jimbo lake anaangalia priorities za nchi. Ukitaka alifanyie nini jimbo lake, kesho utauliza mbona hakufanya chochote kijijini kwake, kesho kutwa utaliza amefanyia nini mtaa wake. Huo ni ubinafsi mkubwa kama wa Magufuli kupindisha barabara ili ipite kijijini kwake. Huyo huyo akataka makao makuu ya mkoa wa Geita yawe kwao Chato badala ya Geita. Huo ni mfano halisi wa ubinafsi.
 
hayo maslah ya nchi ni yepi ambayo yanaonekana yalifanywa na chela?labda useme kwenye chama maana yeye ni TINGATINGA,huyo ndiye aliyehamisha kiwanda cha soda DODOMA na kukipeleka IRINGA,unalijua hilo?kama ni maendeleo yapswa kuonyesha hata jimboni pia......
 
haya mambo ya uraisi inategemea umewekwa/kupigiwa debe na nani
Mwinyi na Mkapa walikuwa pendekezo /chaguo la Nyerere Malechela na Kikwete ni chaguo la mafisadi tofauti isingekuwepo
 
Mimi siwezi kuzungumza ya Malecela japo najua wana CCM ni watoto wa baba mmoja,mama mmoja na kama wapo wachache ambao ni tofauti kidogo basi hawatapewa nafasi kamwe....Ninachojua ni kwamwa huyu Dr wetu wa majukwaani bila kwenda shule hastaili hata kua balozi wa nyumba kumi!
 
Kosa la kumchukua mwema ukamuweka ndani ya waovu ili akufumulie uovu,watakaomuona anaambatano na hao Waovu watamuhesabu ni muovu pia.Ni heri kumtumia mwovu kuangamiza waovu wenzie,kumtakasa mwema ambae ameshirikiana na waovu kwa nia ya kufumua uovu, kwa dunia ya kawaida ya walio wengi hawatakuelewa, kutaka mwema asieleweke ni muovu na mtu huyo akasimama kwenye Public inayotaka kuona Mwema ni Mwema na Muovu ni Muovu,ni kazi kubwa na mfumo huo kwa ulimwengu huu wa sasa mtu wa aina hiyo atakiwi kuwa ni mtu wa watu [Public Figure].

Na haikua sahihi kwa mwema kushirikiana na waovu, muache muovu amfichue muovu mwenzie,kisha wote wasukumiwe hukumu inayostahili wao kupewa.

JK leo hii katufikisha hapa hakika kuna mambo ambayo pia nae kama binadamu mwenye mapungufu kwa kuwa sio Mungu, angependa kuona yanakufa ama yanapotea kwa kuwa yalimkwaza hapo awari kabla ajawa Rais,hayo ni mapungufu ya kibinadamu, lakini ndani ya mapungufu hayo kumezaliwa jambo ambalo kwa namna fulani nimelipenda na ambalo kwa watu wengi wa PWANI wanalo KUCHUKULIA VITU MUHIMU KWA MZAA.[Si nzuri kwa Kiongozi mwenye vision] ila kwa mzaa huu wa kipwani Watanzania wamepata UHURU,ambao kwa KATIBA HII YA SASA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,ambayo inampa Rais Mamlaka makubwa. Kama KWELI bila UNAFIKI Rais Kikwete angesema atumie RUNGU hilo leo hii kusingekua EPA,KAGODA wala DOWANS nani asiyejua Mheshimiwa aliyepita alivyolitumia RUNGU hilo.Leo hii mengi tunayoangaika nayo ni yale awamu iliyopita ukichanganya na mengineyo mapya kama RICHMOND.

Mheshimiwa huyu katika hili la uhuru tulionao leo,anastahiki pongezi sana.kuna vigogo wenzie nahisi wanamuona kama legelege kwa kuwa akutumia mabavu [Dola] kuzibiti matukio yaliyojili.Kwani kuna kashifa ngapi zilikua zinajulikana zama hizo lakini kupitia uthibiti hakuna yoyete iliyofika kwa UMMA na kama ilifika nayo illikandamizwa na kupoteza uhalali wa kujadiliwa na UMMA kwa uwazi kama inavyotoke kwa sasa.

Mheshimiwa huyu kwa kusoma kwake alama za nyakati na kuchukua upepo acha mwenye ubunifu wake kumzidi mwingine kati [Mafisadi na UMMA] ambao kwa ngazi ya Urais ukivaa viatu vyake kwa Mujibu wa katiba yetu [Mfumo] wote ni wake.

Yaani Wananchi na Mafisadi [Sipendi kusikia kuwa RACHEL ndio mafisadi pekee, wakati kuna jamaa zetu kibao mitaani tunawajua ni Mafisadi, natulikua tunawashabikia kila siku kuwa niwajanja kitaa] wote kwa pamoja tunaunda Taifa la Tanzania,kwa mfumo wetu ulivyo na madaraka makubwa aliyonayo Rais, ukichukilia historia ya mfumo wetu wa kutawala Rais anadhamana ya mambo mengi sana kwa kila raia na maliasili zetu.Urais huo ukipata Rais mfujaji aina ya marehemu Mobutu na king'ang'anizi kama Mzee Mugabe nchi hii ni tofauti kabisa.

Kwa kuwa Rais anamamlaka [Invest] mengi na makubwa na ambayo yanategemea Utashi wake ama Hiari yake kuyatekeleza.Makosa yatakayotokea yanatokana na matumizi ya Utashi na Hiari yake na si kwa Muongozo wa Sheria mama. Makosa hayo ambayo yalitakiwa kudhibitiwa na Sheria Mama [KATIBA] yasitendeke yanatendeka au la UMMA usimamie kupingana na Sheria hiyo mama yasitendeke.

Mheshimiwa kwa hili alitumia Utashi wake na Hiari Yake lakini pia akauachia UMMA uamue lipi ni sahihi kwao na kwa faida yao, uku akiwa amewabeba wote kati ya Mafisadi na UMMA.Kwa kuwa vita hii ni dhidi ya mafisadi na wananchi, mshindi ni UMMA ambao kwa pamoja wanaunda jumuhiya na kundi kubwa lenye kudai haki.Na kwa kua mtoa haki anauwezo wa kubana ama kutoa basi kama akitoa haki hiyo anahitaji kupongezwa kwa kuwa ILITAKA MOYO KUFANIKISH HILO.
 
Back
Top Bottom