Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

TOG

New Member
Nov 24, 2022
4
4
Nawasalimu katika Jina la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania,

DAWASA ni Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira mkoa wa Dar es salaam pamoja na baadhi ya maeneo ya Pwani. Nianze kwa kupongea juhudi inafsi zinazofanywa na serikali yetu ya kumtua mama ndoo kichwani, na juhudi za kuhakikisha kua Dar es Salaam inapata huduma ya maji kwa 95% ifikapo 2025.

Kwako Waziri husika, ikiwamo Taasisi ya Utumshi na Mamlaka husika:

Tunayo heshima kubwa ya kuwasilisha malalamiko yetu kwenu, kama wahusika wakubwa mliopewa mamlaka ya kusimamia maslahi ya watumishi wa Umma, ikiwamo Taasisi hii ya DAWASA.

Sisi wafanyaakazi tuna malalamiko makubwa sana (ambapo, baadhi ya malalamiko tulimfikishia Waziri Aweso na Naibu wake, lakini naona mpaka leo hayajashugulikiwa, hali bado ipo pale pale).

Sasa hivi Dawasa inaendeshwa kisiasa sana ikiongozwa na CEO wake, tofauti na pale mwanzoni ambapo alipokua anafanya kazi kama Meneja, na CEO wa DAWASCO. alikua na weledi wa kazi na yuko 'very proffesional', tofauti na alivyo sasa hivi.

Kwani sasa hivi, anaendekezaa na anaendesha hili shirika la serikali kwa siasa, ambapo inampelekea yeye kusahau maslahi na hali ya watumishi/wafanyakazi wake. Hivyo, inapelekea kutokua na utawala bora ndani ya shirika hili, pamoja na kati wa wafanyakazi wake.

Mfano;
Maslahi ya wafayakazi hayazingatiwi siku hizi, ambapo ni kinyume na taratubu za kazi.

Unakuta mfanyakazi anafanyishwa kazi na kiongozi wake (Supervisor, Manager au Mkurugenzi) hadi muda wa ziada (overtime hadi usiku, wikiendi ikiwemo Jumapili) lakini, unakuta mfanyakazi hapewi (halipwi) posho yake ya 'overtime' au hata ya kufanya kazi usiku (night allowance) au posho yake ya kufanya kazi siku za wikiendi ikiwemo Jumapili.

Ikumbukwe kuwa, kuna kazi zingine, bosi anakuwa anatoa kazi kubwa kwa mfanyakazi kwa kudhamiria kabisa, ambapo hiyo kazi itapeleeka kufanywa hadi mda wa 'overtime', hadi usiku, 'exta-duties', au hadi siku ya wikiendi hata Jumapili. Hivyo, uongozi husika inakua haitoi maslahi ya wafanyakazi kama inavyotakiwa.

Nafikiri hii inatokana na kutokuwa na muongozo wa kutoa maslahi ya watu hisika, kama ilivyokuwa katika taasisi zingine za serikali, tena ambazo ni 'ISO certified'.

Hapa hatujazungumzia zile stahiki za mtumishi za malipo ya mafunzo au kozi za kujenga uwezo ambazo hucheleweshwa kulipwa kwa wakati kwa watumishi, hadi unakuta watumishi wanarudi kutoka katika mafunzo/kozi bado hajalipwa stahiki zake.

Unakuta wanakuja kulipwa baada ya wiki/miezi kadhaa mbele, ni uonevu mkubwa. Hili jambo si sawa na inapelekea kuzorota kwa morali ya watumishi wa umma katika ufanyaji kazi wake. Watu wanaumia kweli kweli.

Pia, Wakurugenzi na Mameneja, wanasadikika kama wao ndiyo miungu watu.

Kuna baadhi ya wakurugenzi na Mameneja wanaonekana na wanatabia ya uroho mbaya katika kuongoza kwao, na hata kwa watumishi wao. Unakuta, Bosi (yaani Mkurugenzi au Meneja) hajali maslahi ya mtumishi/watumishi wake hasa wale walio Kada ya chini.

Hii inapelekea Bosi kushindwa kumpatia mtumishi wake maslahi na stahiki yake husika anayotakiwa kuipata, kama nilivyo elezea pale juu. Labda, kwa sababu Mabosi hao Mameneja na Wakurugenzi wanamishahara mikubwa, ndiyo maana inapelekea kutojali maslahi ya wengine.

Ingawa CEO wa DAWASA, anawahasa katika vikao vyao kuwa, Wakurugenzi na Mameneja wawe na waongoza watumishi kwa amani na ypendo katika kazi za ofisini na kazi za kijamii (ni jambo jema, tunampa hongera kwenye hilo). Lakini yote kwa yote, Wakurugenzi na Mameneja ni vizuri wakajiboresha.

Pia, mishahara ya wafanyakazi ni kilio kingine, tai na Suti zisitudanganye. Hali ya wafanyakazi maslahi yao siyo mazuri. Kila mwaka tunapewa ahadi ya kila mwaka, tangu kipindi cha Rais wa awamu ya Tano hayati Dr. JPM mpaka leo, tunaambiwa eti bado tunasubiria uthibitisho kutoka kwa viongozi wa juu. Huku miaka inanza na kuisha, hatujajua kuwa, viongozi hao ni wa kutoka utumishi, wizarani au kwa katibu mkuu kiongozi.

Ikumbukwe kua uwezo na pesa shirika linalo la kuwapa watumishi wake kilichobora tena kulingana na sheria kabisa inavyosema. Ingawa Bodi ya DAWASA tayari imshathibitisha kila kitu kisheria. CEO nini kinafuata?

Pia, kwa wafanyakazi wa mikataba (vijana wa mikataba): Vijana hawa wako wengi humu DAWASA, na wameajiriwa kwa mikataba, wengine wamekaa zaidi ya miaka minne, mitatu na hata miwili Ilihali wengi wao wana sifa za kuajiriwa moja kwa moja (Inabidi na hawa tuwasaidie kuwasemea kwani, wao wakiongea, wiki haitoisha wanaweza wakafukuzwa kazi).

Vijana hawa wanafanya sana sana kazi kwa moyo, tena wengine wanafanya kazi mpaka muda wa 'overtime', 'extra duties' na hata siku za wikiendi lakini hawapewi maslahi yao stahiki au posho zao kama inavyotakiwa. Huu ni uonevu sana.

Vijana hawa hawana sehemu ya kusemea, ila unawakuta wanaumia moyo na wengine wananung'unika kimya kimya (na hamna Bosi yoyote anayewajali). Inaonekena wameshafanywa kama vibarua, kutokana na 'output' yao kuwa kubwa.

Na ikumbukwe kuwa, wengi wa hawa vijana ndiyo Mabosi huwatumikisha haswaa, katika 'overtime', hadi kazi za usiku, 'extra-duties', au hadi siku ya wikiendi hata Jumapili bila kuwapa stahiki zao au kwa usahihi.
      
Vijana hawa asiliimia kubwa wanafanya sana kazi, na kuleta 'output' kubwa katika shirika na katika kila idara ikiwemo miradi mbali mbali. Lakini wamekuwa wakipewa ahadi ahadi za kuwa watajiriwa moja kwa moja na kupewa cheki namba ya serikali, lakini hadi leo hatuoni matumaini yoyote juu yao.

Hadi wengine wamekosa morali, ingawa bado wanakomaa na kazi, na ukiwaangalia usoni bado wanat tabasamu vizuri. CEO kila mwaka anatoa ahadi, kila mwaka ahadi hatuoni hatua, huku unakuta bado uongozi inaajiri vijana zaidi wa mikataba ambapo inaweza kupelekea kuongezea mzigo kwa shirika.

Mwaka huu 2022 Julai, walihaidiwa kuwa wataajiriwa, na siku si nyingi kibali kitatoka, lakini mpaka leo hii Novemba 2022 hamna maendeleo yoyote yanayoonekana au kuambiwa kwa vijana hawa. Ikumbukwe kua, uwezo wa kuwaajiri hawa vijana shirika linalo, na kuwapa stahiki zao zote.

Tafadhali, uongozi husika shugulikia swala hili la hawa vijana wa mikataba, kwani wamekaa miaka mingi sana wakilitumikia shirika hili (wengine ata miaka 4), na ikumbukwe kuwa siku hazigandi katika maisha haya. Huu ni uonevu mkubwa na mbaya.

Wameambiwa kuwa, wanasubiria kibali kutoka mamlaka ya juu, je, ni Utumishi, Wizara au Katibu Mkuu kiongozi? Japokuwa Bodi ya DAWASA imeshafanya tathmini na kuona inaweza kuajiri, na tayari wameshatoa uthibitisho wa kuajiri.

Kwanini tuu DAWASA? Siasa zimeendekezwa sana DAWASA na viongozi ndiyo maana hawaendelei. Mbona mamlaka zingine mfano kama TRA, TPA na TCAA zimeajiri na hata kupoandisha mishahara watumishi wake?

Mbona hizi mamlaka mfano, TRA, TPA na TCAA zimepewa kibali na mamlaka za juu za kuajiri na kupandisha mishahara ya wafanyakazi wao? Kwanini DAWASA hawajapewa kibali hiko na hizo hizo mamlaka? Hakika hili jambo linaleta tafrani kwa wafanyakazi wake.

Bila kusahau, inabidi tuelezee kuhusu malipo ya akwandarasi na ya vibarua wa nje.

Malipo haya, Jinsi yanavyocheleweshwa kulipwa. Tena saa nyingine unakuta yanacheleweshwa kwa makusudi kabisa. Hebu fikiria kibarua ambaye anafanyishwa kazi labda ya kuchimba mitaro ya mabomba ya maji safi au majitaka, halafu anakuja kulipwa baada ya miezi mmoja au mili au na zaidi.

Pamoja na malipo ya wakandarasi, malipo ya wakandarasi hucheleweshwa kulipwa kwa wakati. Tena unakuta ratiba ya malipo haifuatwi kama ilivyo pangwa. Inaweza kukuta ile kauni ya "FIFO - First In First Out" inakuwa haifuatwi.

Mfano, unakuta IPC ya mkandarasi imesharuhusiwa na CEO, na imekuwa ya kwanza kuingia na ipo tayari kwa malipo katika ofisi ya fedha/finance llakini unakuta ofisi ya fedha hawakulipi, na wanaweza wakaifanya ikawa ya mwisho au wakakulipa tena baada ya miezi hata mitano au sita.

Huku wakilipa mapema IPC za wakandarasi wao, au wale wakandarasi wanaojuana nao, au wale wakandarasi ambao wana 'coneksheni' na viongozi wa juu kama Mawaziri, maKatibu au viongozi wafanaano na hao, au hata mpaka upenyeze chochote kitu ndiio unakuta wanaingiza IPC yako katika mfumo wa malipo ili ulipwe. Hili pia ni uobevu wa hali ya juu na siyo utaalamu.

USHAURI
- DAWASA ijifunze angalau kutoka katika taasisi zingine za serikali na zisizo zile zisizo za kiserikali kuhusu kujali maslahi ya wafanyakazi wake. Mfano wa taasis hizo ni; TCRA, EWURA, TCAA na Vodacom.

- Wakandarasi walipwe kwa wakati, na ile kanuni ya "FIFO - First In First Out", ingekua vizurii hii kanuni ifuatwe.

- DAWASA iwe na mfumo mzuri wa malipo yeye kujali maslahi na stahiki za wafanyakazi wake, bila kuwasahau wale vibarua wa kufanya kazi za mda mfupi.

- Pia, DAWASA kupitia uongozi wake, usikubali kupokea miradi ambayo haiwezi kuiendesha yenyewe hasa kwa fedha zake ndani, ambapo zinatokana mapato yake ya ndani. Kwani DAWASA ikipokea miradi hiyo inakuja kusababisha DAWASA ikashindwa kufanya shughuli zake zingine kama kulipia gharama za kuendesha mitambo ya maji, kulipia madawa, kulipia maslahi na stahiki za wafanyakazi wake pamoja na kuendeleza miradi yake midogo midogo n.k.

Tunaelewa kwamba CEO wa DAWASA ni 'very strong', 'Flexible' and thabiti, lakini kupitia hii miradi mikubwa ambayo anategemewa kupewaa, au ambayo ameshapewa ni vizuri wizara husika ikatoa na fedha za kutosha za kuiendesha miradi hiyo kupitia DAWASA, na siyo kutegemea DAWASA itumie "Force account" kuiendesha. Hatimaye ikapelekea DAWASA ikawa kifedha kuyumba na kuwa na madeni makuubwa sana.

Asanteni.
 
Sawa mtumishi wa DAWASA tumekusikia. Umefanya vizuri kufungua akaunti mpya kabisa kijana.
 
Leo majira ya mchana nimepita kwenye Junction ya Msimbazi na Uhuru nimekuta na harufu ya Kinyesi iliyochanyanyika na Uvundo nikajiuliza hivi DAWASA ni kitu kilicho hai? au huo Uvundo unatoka kwenye Maiti ya DAWASA?
 
Mm kama mteja wenu naanza kwa kusema kua overtime zenu nyingi mnazitengeneza wenyewe.

Kwa mfano mnakuja saiti saa 4 asubuhi na mlitakiwa kuja mda w mapema kabisa kisha mnaanza kazi mpk saa 8 mchana mnaenda kula masaa 2, kisha makuja kufunga kazi bila kazi kusogea au kumalizika ukiwauliza wafanyakazi wa dasco vp mbona hv unajibiwa kua tunalefusha kazi ili iandikiwe.

Pia sio kipindi sahihi kwenu kudai madai yenu ikiwa maji hakuna,maji mgao kwa walio bahatika.maji ya shida jijini ambako nyie ndio watoa huduma.
MAJI KWANZA MADAI BAADAE.

Wateja tunataka maji ya uwakika, sio kama ilivyo sasa. BIG NO!BIG NO!!BIG NO!!!.
 
Nyie wafanyakazi wa DAWASA wa ovyo sana. Kwanza mnajilipa mishahara mikubwa unakuta mtu ana diploma ila mshahara mkubwa knm, pili kazini mnawekana tu bila kua na taaluma sahihi unakuta mtu ana diploma ga ualimu ila ni technician, tatu mnajiona na mna poor customer service.

Kwa kuanza, tuambie level ya diploma bei gan mnajilipa na bado mnataka staiki zipi tena?

Pigeni kimya fanyeni maji yatoke. ACHENI kualalamika.
 
Serikali inabidi kulitazama hili Jambo kwa ukubwa maana maji ni uhai so serkali naomba muwaongezee posho na mishahara watu wa Dawasco hiyo laki nane na million bado haitoshi.
 
Tudokeze basi hata zone,mkoa n.k labda watu wanaweza kuja kuchungulia huko na kutatua hilo.
 
Serikali inabidi kulitazama hili Jambo kwa ukubwa maana maji ni uhai so serkali naomba muwaongezee posho na mishahara watu wa Dawasco hiyo laki nane na million bado haitoshi.
Nafikiri kwa baadhi ya watendaji haswa wa chini si wote...
 
Back
Top Bottom