Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi (Jimbo la Segerea)

Maamuzi Kama haya yatapelekea chaguzi zijazo kuwa ngumu na fujo sana. Kama watu wataona dosari yoyote hawatategemea mahakama kutafuta haki yao, watatumia nguvu na hata kumwaga damu ili kulinda haki.

Mkuu Lyimo umeona mbali, na hicho ndicho kitakacho tokea.
 
Last edited by a moderator:
.
Mpendazoe angeshinda kama pasingekuwa na mkono wa mzee wa visasi a.k.a mkuu wa kaya. Huyu ajipangapo kudhulumu haki haangalii mbinguni wala duniani. Ila mimi ninachojua ni hiki kwamba Mungu hakuwahi kumwacha mwenye haki wake na nawahakikishieni haki itapatikana katika shauri hili kwa njia sote tusiyotarajia.
.
napata kigugumizi na wanasheria wetu na vyomba vya mahakama zetu yaani zinapoteza uelekewe na kutoaminika kwa wananchi maana vinatumiwa vibaya na kundi la watawala ambalo ni dogo halafu likisaidiwa na watawaliwa ambao ndiyo wanaoumizwa halafu wanalalamika,dah siamini kama mahanga angechomoka kwa hili na hapa kutakuwa kuna leader interference kwa kias kikubwa jamani.watanzania inatupasa tuamke kwa pamoja tuangalie hili swala la mambo ya kisheria(Mahakama) hiki chombo kinaumiza sana wananchi.
haya yote huwezi kujua haraka haraka yanatuelekeza wapi!
Mimi nipo nasikiliza wimbo wa dada yangu hapa Saida Kalori unaitwa "nchi yangu Tanzania", anaacha ujumbe ambao unasikitisha sana!

 
Hukumu nyingine ya kihuni kutoka kwenye mhimili tegemeo. Kule Sumbawanga inasemekana Jaji alietoa hukumu na kutengua ubunge wa Hilal Haish (ccm) amehamishwa na kuletwa makao makubwa.

Una ushahidi wowote katika hili? Hiyo nyingine ya kihuni unayoijua ni ipi utujuze? Kama huna ushahidi wa unachokisema mkuu kaa kimya,vinginevyo peleka post yako kwenye thread za udaku au tetesi.
 
Mkuu hivi kwa nini mnakuwa vigeugeu mahakama kuu ilivyotupilia mbali madai ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Singida Mashariki na kutangaza Tindu Lissu alishinda kihalali wote humu mlitoa pongezi kwa Mahakama leo kushindwa nyie mnasema Mahakama haikutenda haki sijui mnataka haki gani.

Haki sio tu itendeke bali ionekane ikitendeka. Mnajenga chuki kubwa sana miongoni mwa jamii. Yanatuja kutufika kabla hata hatujafa. Kuanzia leo sikosoi mtu kuchukua sheria mkononi
 
Ndio maana naona kuna umuhimu mkubwa sana kwa wananchi kulinda KURA zao walizopiga kiuhalali kwa sababu mahakama hazi-base kwenye UHALISIA bali kwenye USHAHIDI uliotolewa mahakamani. Wananchi wangelinda KURA zao vizuri, wangemnyang'anya Mahanga yale mabox na kuhakikisha kuwa kila kituo kinaingizwa kwenye list, Ushindi wa CDM ungepatikana na kusingekua na haja ya kwenda mahakamani ambako wamejaa mashabiki na wapenzi wa CCM tokea uhuru!!
 
Mkuu hivi kwa nini mnakuwa vigeugeu mahakama kuu ilivyotupilia mbali madai ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Singida Mashariki na kutangaza Tindu Lissu alishinda kihalali wote humu mlitoa pongezi kwa Mahakama leo kushindwa nyie mnasema Mahakama haikutenda haki sijui mnataka haki gani.

ya kwao duu ya wenzao midomo juu
 
Kesi ya leo ni ngumu sana hasa ikizingatiwa kuwa MPENDAZOE anamjua vizuri mahanga..na MAHANGA ni mwamba kwenye matukio fulani fulani...ila mpaka sasa chanzo changu cha ndani kinadai hiyo alitakiwa kushinda mpendazoe ila kuna kamchezo kakichezwa atashinda Mahanga ila kasipofanikiwa mpendazoe atashinda na chaguzi kurudiwa upyaa.

source-subiri hukumu isomwe.


kama ni vifijo ndo tunavyosubir hapa
Mie hata kabla ya kesi haijaanza nilijua ni kati ya Mahanga au Mpendazoe ndiyo atayeshinda. :sleepy:
 
wewe unaongea nini sasa, mbona hata haueleweki? nipe sababu za msingi kwanini cdm wasikate rufaa

Huwezi kuelewa kama una hasira na kuamini kuwa the court is your mother! Waweza kupitia tena ukipumzika bwana robati.
 
Jamani watu wengi sana walikuwa wameandaliwa kisaikolojia kwamba makongoro atashindwa kuliko hata ile kesi ya sumbawanga. kwa kweli hata mimi nilikuwa nadhani makongoro atashindwa hasa ile issue ya kukimbia na box la kura.
Kuna mtu alisema humu kwamba mapenzi ya mungu yatimizwe.
 
Viva CHADEMA!! hakuna Barabara isiyokuwa na kona ,hizi ni changamoto we have to face...Peoples power forever!(M4C)

Pamoja sana mkuu,Ila ccm na Serikali yake wakumbuke leo wanachekelea kesho watalia mabaya yao haya wanayoyafanya
 
Mkuu hivi kwa nini mnakuwa vigeugeu mahakama kuu ilivyotupilia mbali madai ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Singida Mashariki na kutangaza Tindu Lissu alishinda kihalali wote humu mlitoa pongezi kwa Mahakama leo kushindwa nyie mnasema Mahakama haikutenda haki sijui mnataka haki gani.


wanasema kunya anye kuku,akinya bata ooooooooh anaharisha

sina chama
lakini nashangaa wanajf kuona kuwa singida na sumbawanga sheria zilizotumika labda zinatoka kenya na arusha na segerea sheria zake zimetoka tanzania,hili hatuwezi kulikubari,hatuwezi kuwalazimisha majaji wahukumu kwa maneno na kelele za wana jf

tukubari tu kuwa SHERIA NI MSUMENO-IMEKATA SEGEREA na IMEKATA SUMBAWANGA
 
Nalia kwa Uchungu baada ya police kuendeshwa kwa rimort control na CCM NIlijua wazi kuwa wengi elimu ndogo hawajui wafanyalo.

Naona mahakama sasa inafanya kufuru. Wasomi wote hoi akuna mwanasheria wala jaji wanatumiwa ka big g

hukumu za mgombea binafsi. Kesi za epa zinazokula fedha bila hukumu. Milahab

ya madini. Dhamana ya mdotopile. Hukumu za zombe. Mauaji wabunge kukatwa mapanga ni kazi kwelikweli.

HATUNA WASOMI NI CHAkula cha wanasisa
 
Umenena kweli hakika, tatizo Godfather, TZ hakuna sheria bali, uadilifu tatizo na mhimili moja kuwa juu ya nyingine hukumu yetu ni kwa Mungu; tubaki na kauli moja tu" WAO WANA DOLA SISI TUNA MUNGU, hilo ndilo la msingi kwetu ambalo linatupa faraja.
 
Ingawa simjui huyo prof. jaji, lakini nilishaanza kuwa na wasiwasi na mafrofesor wetu kitambo kirefu sana kilichopita. Wasomi wetu wengi na hasa maprofesor ni watu ambao walishakata tamaa na maisha, hivyo vitendo vyao vingi havitabiliki. Badala ya kujenga heshima za nafasi zao kama wafanyavyo wenzao wengine duniani, hawa wa kwetu wanatafuta ukwasi tu na heshima kutoka kwa watawala waovu.

Nashauri hukumu hii ichunguzwe vizuri ili rufaa ikatwe, na ukweli utaonekana tu mbele ya safari.
 
It is real wonderful judgment with all those disparities, clear signs of cheating and the like, still the judgment is not in favor of the now awaken giant(CDM). Anyway I believe that what is going on is just a rat race, and just a the corner, 2015, we are going to make it. Keep going strong, long live and don't give Mpendazoe.
 
Nalia kwa Uchungu baada ya police kuendeshwa kwa rimort control na CCM NIlijua wazi kuwa wengi elimu ndogo hawajui wafanyalo.

Naona mahakama sasa inafanya kufuru. Wasomi wote hoi akuna mwanasheria wala jaji wanatumiwa ka big g

hukumu za mgombea binafsi. Kesi za epa zinazokula fedha bila hukumu. Milahab

ya madini. Dhamana ya mdotopile. Hukumu za zombe. Mauaji wabunge kukatwa mapanga ni kazi kwelikweli.

HATUNA WASOMI NI CHAkula cha wanasisa

Asante kwa kuliona hilo na kulitambua hilo,kuna wakati tutakuwa Kama ndege wafananao na hakika tutaruka pamoja.
 
Hata mimi sikutegemea kwamba Makongoro atashinda. Lakini tujenge utamaduni wa kuviamini vyombo vyetu vya mahakama. Kama tulivyokubaliana na maamuzi ya huko Singinda, Biharamulo na Sumbawanga. Nadhani mahakama zina uhuru tuupalilie huo uhuru.


utamaduni huo utajengeka tu endapo Haki itaonekana Ikitendeka!! Kwa sababu Maamuzi katika maeneo hayo uliyoyataja CHADEMA ilishinda haimaanishi katika hili tukiona Haki inapindishwa tukae Kimya!!

Ni Ukweli kabisa kwamba Mahanga alikamatwa na masanduku ya kupigia kura!! Haki haijaonekana ikitendeka katika Hukumu!!
 
Back
Top Bottom