Makonda: Wakuu wa Wilaya waondoeni Machinga ndani ya siku 14

“Barabara zimejengwa kwa gharama kubwa hivyo haziwezi kubadilishiwa matumizi na kuwa sehemu ya machinga kupanga na kuuzia bidhaa zao” amesema

Kwanini msiwatengenezee mazingira yanayofanana na hayo wakayatumia nanyi mkakusanya kodi badala ya kuwafukuza kwa mawazo ya kitamaduni!
 
Kwa wenye shughuli kariakoo lazima tumshukuru RC. bavicha watapinga. Kiukweli kariakoo ni too much. Kwangu ile ni zaidi ya uchafu. Takataka za machinga, kutumia barabara. Kelele zao, wingi wao. Zote hizo ni aina za uchafu . Hatuutaki. Ikumbukwe sina nia mbaya na machinga yoyote. Mimi ni mdau wa usafi tu
 
Kweli RC, rais Kasema wasibugudhiwe, inaelekea hapo rais kaona mbali kutokana tanzania haina sera yakudhibiti ongezeko la watu, mtu ni RUKSA kufyatua idadi anayo itaka, wakisha kuwa wakubwa, kazi hakuna, je wataishi vipi, kama sikubabisha na vibiashara vidogovidogo.
Kwahilo basi, mimi naona bora itumike amri alio itoa mkuu wa inchi, ya mgambo wa jiji kutowabugudhi wamachinga
976dd1d912d7cac63d4609e7a2211a30.jpg
 
Makonda aliyekupa wewe ndio aliyemnyima yule,usikufuru Mkuu....

Ningekuwa na confidence ningeanzisha charity ya homeless,cancer na mental health,ila ndio hivyo ujanja jamii forums unajificha ndani ya fake id unaropoka unavyotaka.:D:cool::p
 
Tena wa hapo kariakoo wangepunguziwa mda kabisa, watu ni wengi alafu genge la vibaka wamejazana hapo
 
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa nakuunga mkono katika suala hili.Ila nashauri:

pawepo utashi wa kisiasa wa kuwasaidia hawa wafanya biashara ndogo ndogo
Pawepo sera inayoanzia mamlaka husika(Halmashauri za Miji na Majiji) za kuwatengea maeneo maalum hawa wafanyabiashara wa kundi hili
Sehemu zinazotengwa ziwe zile zenye mvuto kwa wateja /walengwa ,ili wasishawishike kufuata wateja katikati ya miji
ufanywe utafiti wa makusudi kujua ni aina gani za biashara zinavutia wafanya biashara ndogo ndogo na kundi lipi la waTanzania linahusika katika biashara hii.(hapa elimu,uwezo kimtaji, Umri nk)
pawepo maandalizi ya kielimu na kisaklojia kwa walengwa kabla ya kuwahamishia sehemu ambazo zimetengwa
wakishahamishiwa sehemu pawepo ufuatiliaji wa makusudi kuhakikisha wamepata huduma muhimu kama choo,maji na umeme na ulinzi
 
Kwahili naunga Mkono kabisa na sijui kwanin uamuzi huu haukuchukuliwa mapema. Katika eneo la kariakoo haiwezekani sa nne asubuhi unapita kwenye eneo la magari wakati kuna space ya watembea kwa miguu ambayo machinga ndio wamemwaga kila kitu na ule msongamano unatengeneza wezi sana. Ila angalizo ni je maeneo waliyotengewa yanatosha hawa wote au tunahitaji kuwaongezea eneo?
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo ametoa siku 14 kwa Wakuu wa Wilaya za Jiji hili kuhakikisha machinga wote wanafanyia biashara katika maeneo waliyopangiwa.

“Kauli ya Rais aliyoitoa kwamba machinga wasibugudhiwi isitumike vibaya kwani hata wao hawapaswi kuwabugudhi wananchi wengine kwa kufanya biashara zao mbele ya maduka na barabarani,”amesema Makonda.

Ameongeza kuwa anatambua kuwa machinga wanajitafutia riziki lakini hawapaswi kuvunja sheria kwa kufanya biashara hata katika maeneo yasiyokuwa rasmi.

“Barabara zimejengwa kwa gharama kubwa hivyo haziwezi kubadilishiwa matumizi na kuwa sehemu ya machinga kupanga na kuuzia bidhaa zao” amesema

Naunga mkono uamzi huo maana una mashiko na faida kwa jamii nzima.
Mhe. RC matamko ya aina hiyo ninayakaribisha sana na karibu tena na tena
 
Debe tupu limeibuka tena; kabla ya Novemba 15 hili suala litakuwa limeshasahaulika.
Kama wamachinga wanavunja sheria, itajwe hiyo sheria na kisha polisi wafanye kazi yao, wakuu wa wilaya inawahusu nini wakati masuala hayo ni majukumu ya mameya?
So mameya hawajafanya kazi yao ipasavyo??
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo ametoa siku 14 kwa Wakuu wa Wilaya za Jiji hili kuhakikisha machinga wote wanafanyia biashara katika maeneo waliyopangiwa.

“Kauli ya Rais aliyoitoa kwamba machinga wasibugudhiwi isitumike vibaya kwani hata wao hawapaswi kuwabugudhi wananchi wengine kwa kufanya biashara zao mbele ya maduka na barabarani,”amesema Makonda.

Ameongeza kuwa anatambua kuwa machinga wanajitafutia riziki lakini hawapaswi kuvunja sheria kwa kufanya biashara hata katika maeneo yasiyokuwa rasmi.

“Barabara zimejengwa kwa gharama kubwa hivyo haziwezi kubadilishiwa matumizi na kuwa sehemu ya machinga kupanga na kuuzia bidhaa zao” amesema
Tamko la ngapi hili wadau namshauri mkuu wetu wa mkoa awe anafuatilia hatua kwa hatua manake hii nchi ina manunda balaa.
 
Hapo ndio nakumbuka wimbo wa prof Jay bongo dar es Salam
Ule mstari u asema hivi

''Mnawaita machinga ingawa si watu kutoka mtwara, mnapovunja vibanda vya, wengine walikuwa wezi je warudie zama zao''
 
Lakini agizo hili sio mara ya pili..? ambapo mkulu alisema waachwe tu, sasa imekuwaje tena.?
 
Back
Top Bottom