Makonda: Wakuu wa Wilaya waondoeni Machinga ndani ya siku 14

Maisha haya,kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa? Lini sisi wananchi tulilalamika kwamba wamachinga wanatubughuzi? Maisha hayapo fair kabisa
 
UKUTA haupo, sasa machinga unarudi kuisoma namba!

kila nchi kuna machinga, hata China nenda Guangzhu uone watu wanavyohustle kitaa
 
ukiona uliowachagua wanapinga maelezoyako ujue unatabia mbaya ya kuropoka AMA kukurupuka...
mkulu alisema kamavp barabara moja zifungwe jioni biashara ifanike
 
Makonda alifanya vizuri, raisi akaja kuwaruhusu warudi barabarani, aliniudhi sana raisi.
 
Wamachinga wasibugudhiwe waache wafanye biashara, huyo makonda mbona alishatoa muda na alishindwa
mbona kwenye uchaguzi mlisema mgambo watafute kazi nyingine ?
waacheni wapige kazi sasa kuwapeleka pembezoni sehemu hakuna biashara maana yake ni nini?
kuweni wabunifu .
 
Sasa wakuu wa wilaya watatumia polisi au wana mgambo?

Si mliwaruhusu kuwakomoa mameya wa ukawa waonekane hawafanyi kazi miji inachafuliwa na wamachinga sio?
 
Hiyo hata mimi namwunga mkono. Lakini nashauri hivi vitu viwe endelevu. Kama tunaamua kuwaondoa machinga mitaani waondoke na wasirudi tena. Hii habari ya kumwaga mgambo leo na kisha baada ya siku mbili unaona business as usual haisaidii sana. Kudos Makonda.
 
Kwa sasa mnaweza waondoa sababu tamko la mkulu ilikuwa kupoza UKUTA,

Sababu wale vijana walihamasika kuingia barabarani.
 
Huyu makonda itakuwa burdani ktk roho za wazalendo wanademokrasia ktk jiji la Dar, kama atatupia karata yake mwaka wa 2020, au kibamba, au kawe....!
Huyu hata akipiga kampeni kwa kutumia mapepo na majini , hayo majimbo unayompeleka unamchuuza vibaya sana ! Kwanini asigombee kwao kondoa ?
 
Nasikia mtaa wa Congo hakufai, sijaendaga kitambo pale ngoja weekend hii niende nikajionee kwa macho tena sikuhizi kuna Mwendokasi kuanzia Moroco nitaupanda huo.

Mwenyekiti CCM JF
mkuu usiende na chochote cha thamani mfukoni au mwilini
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo ametoa siku 14 kwa Wakuu wa Wilaya za Jiji hili kuhakikisha machinga wote wanafanyia biashara katika maeneo waliyopangiwa.

“Kauli ya Rais aliyoitoa kwamba machinga wasibugudhiwi isitumike vibaya kwani hata wao hawapaswi kuwabugudhi wananchi wengine kwa kufanya biashara zao mbele ya maduka na barabarani,”amesema Makonda.

Ameongeza kuwa anatambua kuwa machinga wanajitafutia riziki lakini hawapaswi kuvunja sheria kwa kufanya biashara hata katika maeneo yasiyokuwa rasmi.

“Barabara zimejengwa kwa gharama kubwa hivyo haziwezi kubadilishiwa matumizi na kuwa sehemu ya machinga kupanga na kuuzia bidhaa zao” amesema.

Chanzo: Fahari News
Kweli nami nikiri wamachinga ni kero ktkt ya jiji...lkn je wakiwatoa hapo watawapeleka wapi?! Maana Dsm hakuna mipango miji hamna sehemu iliyoandaliwa kwa ajili yao ili kuweza kupata suluhisho la moja kwa moja.
Hapa kuna makundi ya Machinga, Mama ntilie, na bodaboda mara nyingi hutumika kama mitaji ya kura kwa wanasiasa, ndio maana tatizo lao linasumbua sana......
Lakini pia ni kundi la semi literate, ambalo lina mitaji midogo na halina mategemeo ya kupata ajira, ukiwasambaratisha wanatulia siku moja kesho yake wapo tena mtaani ......
Their struggle is endless.
Kila la heri Mh. Makonda.
 
Kitendo cha Mh' Makonda kuwaondoa hawa jamaa ni cha kupongezwa maana mji kidogo ugeuke kuwa Kampala, ingawa na huko majuzi wametimuliwa mitaani na kuzusha vurugu kubwa, lakini haya mambo yanachangiwa na viongozi kutokuwa proactive, wanafumbia macho uvunjifu wa sheria halafu wanakurupuka wakati mambo yameshaotamizizi, mifano ni ujenzi kwenye maeneo yabarabara, mabondeni n.k, lini tutajifunza kutokana na makosa wakati tunaelekea yetu miaka 50 baada ya uhuru,?! Ndio maana namshauri mkuu wa mkoa avuje manispaa hizi zinazoendeshwa kitapeli na posho za vikao vya madiwani na badala yake aunde mamlaka ya jiji au wizara kamili ya jiji la daresalaam kama ilivyo Nairobi. Mji huu unataka direct administration sio kwa mfumo huu uliopo haufai,
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom