benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mango akiwa ziarani Mwanza amesema hataki kusikia tena Barabara zikifungwa kwa masaa mengi ili apite, huku akisema dakika 10 zinatosha ili Wananchi waendelee na shughuli zao.
Dr. Mpango amewaomba radhi Wananchi kwa usumbufu walioupata baada ya jana Barabara kufungwa kwa saa nne ili veve apite "Nilishamwambia IGP na nirudie kuwaambia Makamanda wa Polisi wa Mikoa, mambo ya kufunga barabara kwa masaa mengi kisa tu Mtoto wa masikini Philip Mpango anapita hapana"
"Jana naambiwa mmefunga Barabara mpaka masaa manne haiwezekani, kwanini?, sitaki kusikia tena hili linajirudia, muambizane na wanaopokea msafara huko tutakakopita"
"Acheni Wananchi wapite kwani dakika 10 hazitoshi), masaa manne kweli!? Nawaomba radhi ya dhati kabisa Wananchi"
======
Kauli ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango inafuatia Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Jijini Mwanza kufunga Barabara kwa Saa 4 katika ziara yake na kusababisha foleni na adha kwa Watumiaji Barabara wengine.
Kitendo hicho kimefanya Dkt. Mpango kuwaomba radhi Wananchi huku akiwahoji Polisi kama Dakika 10 hazitoshi kupisha Misafara. Pia, amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yote kutorudia tena utaratibu huo.
Kumekuwa na Malalamiko ya Wananchi ya mara kwa mara kuhusu Misafara ya Viongozi kusababisha Foleni na usumbufu katika maeneo mbalimbali Nchini lakini bado suala hilo halijapatiwa ufumbuzi.