Wananchi wa Korogwe tunakereka kusimamishwa muda mrefu barabarani ili kupisha misafara ya viongozi wa Siasa, hii sio sawa

Kayugumis

Member
Jun 6, 2022
85
63
Hapa Korogwe Mkoani Tanga tuna changamoto ambayo naomba leo tuiweke wazi kwa sababu imetufika hapa (shingoni).

Naomba kuripoti kero juu ya misafara ya viongozi wanaopita hapa Korogwe Mjini yaani tunasimamishwa muda mrefu sana kisa msafara wa viongozi au kiongozi.

Mara nyingi tu shughuli zimekuwa zikisimama mpaka tunachelewa kazini na kwenye mambo mengine ya muhimu.

Nimeona msafara unavyokuwa kwa sehemu nyingine ni kweli huwa kuna mchakato wa kuwaweka watu pembeni ili viongozi wetu wapiti lakini lakini hapa Korogwe imezidi ndugu, askari wanasimamisha watu kwa muda mrefu zaidi ya saa kadhaa wakati unakuta kiongozi yuko mbali.

Hivi ni haki kweli shughuli za uchumi za Wananchi wote zisimame kwa zaidi ya saa kadhaa kisa tu kuna kiongozi anapita tena unakuta hana mpango wa kusimama, nashauri mamlaka ziangalie utaratibu mzuri wa kufanya.

Juzi kati nilimsikia Makamu wa Rais anasema hapendi kuona Wananchi wanasimamishwa muda mrefu ili yeye apite, nafikiri hilo lizingatiwe.
 
Badala ya viongozi kuwa wanajali raia pia kuwanyenkekea, sasa Wananchi wametekwa nyara na usumbufu wa viongozi waliovimba vichwa ambao kiuhalisia wameajiri na wananchi, lakini waajiriwa hao wamegeuka kero na miungu-watu na kuwadharau walipakodi.
 
Dhalimu ndio aliboresha huu uhuni wa kusujudia viongozi.
 
Wakati fulani Polisi hawatumii akili. Kiongozi ndio kwanza anaamka Kitandani walishasimamisha Magari
 
Wakati fulani Polisi hawatumii akili. Kiongozi ndio kwanza anaamka Kitandani walishasimamisha Magari
Wewe ndio huna akili,nani anataka amwagiwe ugali? Likitokea napo tutasema polisi ni wazembe.Acha polisi wetu wafanye kazi zao kwa uhuru.
 
Back
Top Bottom