Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

Aliiba kura mwaka jana bana, hata kama tungepiga kura watu laki 4, kura zikahesabiwa kwa haki na akatangazwa aliyepata kura nyingi ndo mshindi KIKWETE ASINGESHINDA, ila jamaa(JK) anatu-cost jameni, lets do something, pls
 
We still have a chance, but I see people don't want to use this chance we have now!! Tunasubiri hadi kila kitu kigome ndo tuamke.
 
Nafkiri mtu kama kikwete kuwepo madarakani hadi sasa says something about US! ME AND YOU!
Na the best thing to do ni kuto subiri uchaguz bali kujaribu kumngoa sasa,hata tukishindwa mpaka hio 2015 itakua fundisho kwa anaeingia kuwa mitanzania ya sasa sio ya mwaka 47!
 
Madhara ya kuwachagua viongozi waliomwamgusha mwalimu ndo haya.Hii kauli ya kejeli si mpya kwa viongozi waliomrithi mwalimu.Ni kauli zilizokuwa zikitolewa na viongozi hao toka wakiwa mawaziri.Hata Christian Kisanji alishawahi kutoa kauli kama hizi kipindi alipokuwa waziri wa maji chini ya Mwinyi.Nilikuwepo huko Same Sekondari na ziara ya waziri huyo tuliisubiria tukidhani itakuwa ya matumaini kwa kusikilizwa vilio vyetu vya ukame wa maji wa kupindukia na kuja na solutions.Nakubaliana na ukweli kwamba tunavuna tulichopanda.Sioni vongozi kabisa.Kwa upande mwingine,nimesoma mahojiano na BBC nimechoka.Tofauti na wengineo,kwangu ni vigumu kuamini kwamba hizo ni kauli za viongozi waliopewa dhamana.Siamini kabisa kuwa Tanzania haina watu wenye kufikiri beyond this.Wenye kuweza kutufanikisha hawapewi nafasi.Na ukiangalia,wananchi milioni 40 wanachaguliwa viongoz/Kiongozi na wananchi milioni 4 tu,yani ten pasenti ya wananchi wanawatuvunisha milioni arobaini haya makapi.
Tatizo letu watanzania ni namna tunavyowapata viongozi. Kupata uongozi hapa nchini ni sawa na kucheza "TOMBOLA" kila mtu anaweza kuwa kiongozi...hii ndio tofauti yetu ya msingi na walioendelea.
 
Nikirejea mahojino kati ya Rais Kikwete na mwandishi wa BBC majuzi kuhusiana nasuala la umeme, hisia kadhaa zinakuja akilini mwangu, masikitiko, kicheko na hasira!

Kama nilitarajia majibu yenye kuleta maana, basi nilikosea sana, lakini sikutegemea kuona majibu yaliyokosa busara na umakini na zaidi uungwana wa kukiri kuwa kuna makosa katika mipango na utekelezaji wa kazi katika uongozi wa ais Kikwete.

Ingekuwa rahisi sana kwa Kikwete kupokelewa kwa kusamehewa kama angekiri wazi kuwa Serikali yake ilifanya makosa katika mipango hii ya kuzalisha umeme na angejibebesha msalaba mzima na kusema tumeanza kazi mpya na tutaliangalia kwa upya kwa kasi, basi tungemuelewa.

Lakini Rais kajibu kwa ghadhabu, kiburi, kejeli na masikhara. Zaidi anawabeza wale wanaohoji kwa nini bado tunaendelea na tatizo hilo.
Cha kusikitisha ni Rais kulaumu mvua na ukame na hata kudai Serikali haiwezi kuleta mvua. Swali langu kwa Rais KIkwete, leo hii ambapo inafahamika wazi dunia nzima kuwa kuna mizunguko ya hali ya hewa ambayo imevurugika, somo la njaa na ukame wa mwaka 1974, 1984, 1994 na hata miaka ya 2000, halijaingia katika akili za watawala au mtawala wetu?

Yeye si Mchumi, je wachumi si watu wanaobobea katika takwimu na mipango? Je alishindwa vipi kuling'amua hili hata pale alipokuwa Waziri katika wizara ya Maji na Nishati kwa miaka 6? Je si yeye au katika uongozi wake ndipo Tanzania iliingia mkataba na IPTL hata kama alikwisha hama Nishati, lakini si alikuwa Hazina alipoidhinisha fedha?

Leo anapojitapa na kujisifia kuzalisha umeme wa megawati 300 kwa kipindi cha miaka minne, je umeme huo uko wapi leo hii ikiwa tunaambiwa hakuna mafuta na gesi ya kutosha na mitambo mingine ni mibovu? Je atatuambia nini ilhali inafahamika wazi kuwa hizo megawati 300 zimanuka harufu ya rushwa na hujuma kama Dowans?

Anapodai kuwa mitambo ya kuzalisha umeme haijengwi siku moja, je kasahau kilio cha Mchungaji mwaka 2006 alipoomba Rais akutane na GE akienda Marekani kwa swahiba wake George Bush?

Kama yeye ni kiongozi makini, je tatizo hili la umeme kalivalia njuga gani? Mbona Kenya wamejenga mfumo wa umeme wa Upepo kwa miaka mitatu bila kutokwa jasho au kusubiri upungufu wa maji na ukame waanze kuhaha kutafuta miradi uchwara ya kuzalisha umeme?

Kama yeye ni kiongozi fanisi, je mbona hajatumia ile methali ya kinga ni bora kuliko tiba kwa kuwa mstari wa mbele kuagiza hiyo mitambo ambayo haiuzwi kama shati la mtumba?

Rais Kikwete ametudhihaki Watanzania na kukishusha hadhi cheo na dhamana aliyopewa. Na zaidi, ameonyesha wazi dharau yake pale alipoamua kumuonyesha dharau ya wazi Mbunge Mnyika na kumfanya aonekane ni mwendawazimu ilhali ni viongozi wake na uongozi wake uliojaa ahadi za uongo, uvivu na ukosefu wa umakini katika kufanya kazi.

Lakini, sitaendelea kumchutumu sana, maana niliiona hili la uongozi wa kizembe tangu awali.

Majibu aliyotoa yanaonyesha ni Kiongozi asiyejali lolote linalotokea ndani ya nchi, haelewi kwa nini Tanzania ni masikini, anawabembeleza wahalifu wajisalimishe, uchumi unadidimia lakini yupo tayari kuzitumbua fedha zaidi kwa safari, semina na vikao vya kufundishana kazi na kuvuana magamba huku akilalamika na si kuonyesha ushupavu an umadhubuti wa kuwa Rais na hata mwenyekiti wa Chama chake CCM.

Watanzania tumevuna tulichokipanda! Wala tusiwalaumu CCM pekee yaom bali ni sisi sote kama Taifa kwa kukubali kwa umoja iwe ni kupitia kura zetu za ndiyo au hapana, au hata kuendelea kutazama uongozi huu wa awamu ya nne ukijiendeaa tuu kama jongoo au konokono bila kuelewa ni wapi dira inasema tuelekee.

Tumelelea mfumo mbovu wa watu kutokuwajibika, na haya ni matunda ya watu wasiowajibika au hata kuogopa kuwa wana wajibu wa kuwajibika kwa dhamana na kazi walizopewa.

Haijali ni nani atakuwa Rais wetu 2016, lakini kwa mwendo huu wa uongozi huu tuliouona na watu ndani ya chama cha CCM na hata Serikalini watu wanakubali kuburuzwa na kiongozi asiye makini na mwenye silika za uzembe na masikhara kama haya, basi safari yetu ni ndefu mno.

Ili kuelewa kuwa tunaongozwa na mtu asiyethamini dhamana aliyopewa, tafakari vicheko vya dharau au masikhara alivyofanya wakati akiulizwa maswali ya msingi kuhusu tatizo hili la ukame.

Ama kweli Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu!


Haapa nasoma lawama tupu. Ningekuona tofauti na Kikwete kama angalau paragraf moja ungetoa mapendekezo ya ufumbuzi wa tatizo la umeme TZ, AMA LIWE LA MUDA MFUPI AU LA KUDUMU.

Huwa napata kichefuchefu kusoma taarifa kama hizo kwani hazina tija wala faraja. Isitoshe zinaonyesha jinsi watanzania au kwa ukika zaidi wanaJF wanavyofanana akili zao. Baya zaidi ni kila utapofungua mada utakuta hali hiyo hiyo hata kwa wale tuliowaamini sana na kuwaita WASOMI WA JF.

Kweli NYANI HAONI KUNDULE!
 
Huyu jamaa alikuwa Mbunge wa Chalize kwa miaka kibao kaiacha haina sekondari hata moja ukiondoa ile ya Lugoba aliyosoma yeye middle school atawezaje kuwa na maono ya maendeleo kwa taifa?
 
Katika majibu yake Kikwete alionyesha 600MW tangu uhuru na hizi 300MW wanazoziongeza, labda tu niwajuvye wakati ule 600MW zilikuwa over and above mahitaji ya umeme na hivyo kuwa excess reserve, mgao wa umeme Tanzania umeanza miaka ya late 90's precisely 97

Hivyo kwanza ni kushukuru awamu 2 za mwanzo kwa kuwa na reserve, nchi nzima ni kama 300MW tu zilizohitajika na si zaidi!!

Awamu 2 zilizofuatia kasi ya ukuaji wa uchumi, uwekezaji na access to electricity imeshika chati, hivyo haiingii akilini kurudi kwenye zama za mawe za awamu 2 za kwanza kwani hazifanani kabisa, maeneo mengi yamebadilika kila kukicha majumba yanajengwa mijini na vijijini , viwanda vipya vinaingia, migodi na kadhalika, katika mipango hii yote huwezi kuacha kukipa kipaumbele umeme kiutaalamu na si kwa kusoma 600MW za miaka ya 80's

Mgodi mkubwa kama Geita hautumii umeme wa TAnESCo pale mahitaji yao ni 40MW,maghorofa yote mazito mazito yanayoporomoshwa mijini hayo mahitaji ni @least 2MW , hujahesabia viwanda nk nadhani ukifanya demand side management utaona mahitaji yanakua kwa 100MW kwa mwaka tangu 2005 hiyo inatosha kuonyesha serikali haiko makini kuwaza 600MW za nyuma na kujisifia kwa 300MW za sasa
 
Tatizo la huyu mtu ni ujuaji, anajua kila kitu, na hili ndilo linalopelekea haya yote, inaoneka hashauriki.
Wakati anapojibu maswali sijui anafikiria wapi, yaani yupo yupo tu, cha kushangaza akishastaafu utasikia eti nae anabusara.
Kuna matukio mengi yanayoonesha dharau zake, kama ulipata kuona mahojiano wakati wa kampeni bukoba ailijibu kwa dharau sana.
Nasijui anatoa wapi jeuri hii, lakini ukweli unabaki wazi kuwa huyu mtu ana IQ ndogo.
 
Huyu jamaa alikuwa Mbunge wa Chalize kwa miaka kibao kaiacha haina sekondari hata moja ukiondoa ile ya Lugoba aliyosoma yeye middle school atawezaje kuwa na maono ya maendeleo kwa taifa?

Hata za kata hakuna?????????
 
Jeyi Keyi anaitaji maombi ya nguvu!!!!!!! "I need Meditation so i can lead my people"-The game
 
Kwakweli kikwete kama ni zarau zimepitiliza rais hatakiwi kuwa hivyo, wananchi tunalia tatizo la umeme yeye anaongea kabisa pumba zake kwa kujiamini huku anacheka, inasikitisha sana na inauma sana kwa alichokijibu kikwete bora mnao hadisiwa kuliko 2lio mshuhudia kwa kuacha kazi ze2 eti 2namsikiliza rais
 
Katika majibu yake Kikwete alionyesha 600MW tangu uhuru na hizi 300MW wanazoziongeza, labda tu niwajuvye wakati ule 600MW zilikuwa over and above mahitaji ya umeme na hivyo kuwa excess reserve, mgao wa umeme Tanzania umeanza miaka ya late 90's precisely 97

Baelezee Engineer.

Lakini...hivi hatuna qualified Engineers pale TANESCO??
 
Wana JF.

Nadhani JK amerudisha ile kauli ya RUKSA kila mtu achukuwe na afanye atakavyo sasa
 
Sipendi kuitwa mkabira lakini na hii inabidi kuwa kati ya vitu vya kuviangalia kuteuwapo wagombea nafasi za Urais. Sasa kama Rais atatokea kwenye kabila ambalo mila na desturi zao hazioni hasara ya kuuza ardhi au makazi yake Mazuri, yalio sehemu mzuri iliyo mjini kwa mgeni na yeye akawa tayari kuhama kwenda sehemu ya mashambani isiyo na maendeleo. Unategemea nini si kama atauza Raslimali za Nchi kwa wageni na kutona tatazi lolote kama wananchi wake watakosa umeme kwa ajili ya kujiendeshea maisha yao na uchumi wa nchi yao.

Kama nilivyosema sipendi kuwa mkabila lakini mila na desturi zituelekeze kwani kuna mila ambazo huwa zinalinda sana raslimali yaani KIAMBA, hebu jaribu kumdhulumu mchagga, mhaya, myakyusa kipande kidogo tuu cha ardhi au mkurya, mmasai, mnyamwezi mdhulumu ng'ombe utaona moto wake.
 
Back
Top Bottom