Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Nikirejea mahojino kati ya Rais Kikwete na mwandishi wa BBC majuzi kuhusiana nasuala la umeme, hisia kadhaa zinakuja akilini mwangu, masikitiko, kicheko na hasira!

Kama nilitarajia majibu yenye kuleta maana, basi nilikosea sana, lakini sikutegemea kuona majibu yaliyokosa busara na umakini na zaidi uungwana wa kukiri kuwa kuna makosa katika mipango na utekelezaji wa kazi katika uongozi wa ais Kikwete.

Ingekuwa rahisi sana kwa Kikwete kupokelewa kwa kusamehewa kama angekiri wazi kuwa Serikali yake ilifanya makosa katika mipango hii ya kuzalisha umeme na angejibebesha msalaba mzima na kusema tumeanza kazi mpya na tutaliangalia kwa upya kwa kasi, basi tungemuelewa.

Lakini Rais kajibu kwa ghadhabu, kiburi, kejeli na masikhara. Zaidi anawabeza wale wanaohoji kwa nini bado tunaendelea na tatizo hilo.
Cha kusikitisha ni Rais kulaumu mvua na ukame na hata kudai Serikali haiwezi kuleta mvua. Swali langu kwa Rais KIkwete, leo hii ambapo inafahamika wazi dunia nzima kuwa kuna mizunguko ya hali ya hewa ambayo imevurugika, somo la njaa na ukame wa mwaka 1974, 1984, 1994 na hata miaka ya 2000, halijaingia katika akili za watawala au mtawala wetu?

Yeye si Mchumi, je wachumi si watu wanaobobea katika takwimu na mipango? Je alishindwa vipi kuling'amua hili hata pale alipokuwa Waziri katika wizara ya Maji na Nishati kwa miaka 6? Je si yeye au katika uongozi wake ndipo Tanzania iliingia mkataba na IPTL hata kama alikwisha hama Nishati, lakini si alikuwa Hazina alipoidhinisha fedha?

Leo anapojitapa na kujisifia kuzalisha umeme wa megawati 300 kwa kipindi cha miaka minne, je umeme huo uko wapi leo hii ikiwa tunaambiwa hakuna mafuta na gesi ya kutosha na mitambo mingine ni mibovu? Je atatuambia nini ilhali inafahamika wazi kuwa hizo megawati 300 zimanuka harufu ya rushwa na hujuma kama Dowans?

Anapodai kuwa mitambo ya kuzalisha umeme haijengwi siku moja, je kasahau kilio cha Mchungaji mwaka 2006 alipoomba Rais akutane na GE akienda Marekani kwa swahiba wake George Bush?

Kama yeye ni kiongozi makini, je tatizo hili la umeme kalivalia njuga gani? Mbona Kenya wamejenga mfumo wa umeme wa Upepo kwa miaka mitatu bila kutokwa jasho au kusubiri upungufu wa maji na ukame waanze kuhaha kutafuta miradi uchwara ya kuzalisha umeme?

Kama yeye ni kiongozi fanisi, je mbona hajatumia ile methali ya kinga ni bora kuliko tiba kwa kuwa mstari wa mbele kuagiza hiyo mitambo ambayo haiuzwi kama shati la mtumba?

Rais Kikwete ametudhihaki Watanzania na kukishusha hadhi cheo na dhamana aliyopewa. Na zaidi, ameonyesha wazi dharau yake pale alipoamua kumuonyesha dharau ya wazi Mbunge Mnyika na kumfanya aonekane ni mwendawazimu ilhali ni viongozi wake na uongozi wake uliojaa ahadi za uongo, uvivu na ukosefu wa umakini katika kufanya kazi.

Lakini, sitaendelea kumchutumu sana, maana niliiona hili la uongozi wa kizembe tangu awali.

Majibu aliyotoa yanaonyesha ni Kiongozi asiyejali lolote linalotokea ndani ya nchi, haelewi kwa nini Tanzania ni masikini, anawabembeleza wahalifu wajisalimishe, uchumi unadidimia lakini yupo tayari kuzitumbua fedha zaidi kwa safari, semina na vikao vya kufundishana kazi na kuvuana magamba huku akilalamika na si kuonyesha ushupavu an umadhubuti wa kuwa Rais na hata mwenyekiti wa Chama chake CCM.

Watanzania tumevuna tulichokipanda! Wala tusiwalaumu CCM pekee yaom bali ni sisi sote kama Taifa kwa kukubali kwa umoja iwe ni kupitia kura zetu za ndiyo au hapana, au hata kuendelea kutazama uongozi huu wa awamu ya nne ukijiendeaa tuu kama jongoo au konokono bila kuelewa ni wapi dira inasema tuelekee.

Tumelelea mfumo mbovu wa watu kutokuwajibika, na haya ni matunda ya watu wasiowajibika au hata kuogopa kuwa wana wajibu wa kuwajibika kwa dhamana na kazi walizopewa.

Haijali ni nani atakuwa Rais wetu 2016, lakini kwa mwendo huu wa uongozi huu tuliouona na watu ndani ya chama cha CCM na hata Serikalini watu wanakubali kuburuzwa na kiongozi asiye makini na mwenye silika za uzembe na masikhara kama haya, basi safari yetu ni ndefu mno.

Ili kuelewa kuwa tunaongozwa na mtu asiyethamini dhamana aliyopewa, tafakari vicheko vya dharau au masikhara alivyofanya wakati akiulizwa maswali ya msingi kuhusu tatizo hili la ukame.
Rais Kikwete: Kwanza, serikali haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe, unajua, unajua hivyo, Kwa sababu (kicheko) ingekuwa na uwezo wa kufanya mvua inyeshe mabwawa yale yangejaa.

Ama kweli Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu!
 
Hivi Rais wetu ni mchumi kweli?

Mi nadhani mambo ya JWTZ kile cheo cha Kanali vili delete mpaka kwenye recycle bin anything to do with uchumi kwenye "RAM" yake.
 
Lakini inawezekana ni kweli kuwa yeye siye mvua but kwa uwezo wake wa kuelewa!
 
Mkuu Rev. Kishoka, kutarajia busara na umakini kutoka kwa huyu mcheza kiduku ni sawa kutegemea guta libebe 40 feet container lililojaa mzigo wa vyuma. Watanzania tukubali kuwa nchi hii haina rais, kuna sharobaro anajiita rais tu.
 
Nikirejea mahojino kati ya Rais Kikwete na mwandishi wa BBC majuzi kuhusiana nasuala la umeme, hisia kadhaa zinakuja akilini mwangu, masikitiko, kicheko na hasira!

Kama nilitarajia majibu yenye kuleta maana, basi nilikosea sana, lakini sikutegemea kuona majibu yaliyokosa busara na umakini na zaidi uungwana wa kukiri kuwa kuna makosa katika mipango na utekelezaji wa kazi katika uongozi wa ais Kikwete.

Ingekuwa rahisi sana kwa Kikwete kupokelewa kwa kusamehewa kama angekiri wazi kuwa Serikali yake ilifanya makosa katika mipango hii ya kuzalisha umeme na angejibebesha msalaba mzima na kusema tumeanza kazi mpya na tutaliangalia kwa upya kwa kasi, basi tungemuelewa.

Lakini Rais kajibu kwa ghadhabu, kiburi, kejeli na masikhara. Zaidi anawabeza wale wanaohoji kwa nini bado tunaendelea na tatizo hilo.
Cha kusikitisha ni Rais kulaumu mvua na ukame na hata kudai Serikali haiwezi kuleta mvua. Swali langu kwa Rais KIkwete, leo hii ambapo inafahamika wazi dunia nzima kuwa kuna mizunguko ya hali ya hewa ambayo imevurugika, somo la njaa na ukame wa mwaka 1974, 1984, 1994 na hata miaka ya 2000, halijaingia katika akili za watawala au mtawala wetu?

Yeye si Mchumi, je wachumi si watu wanaobobea katika takwimu na mipango? Je alishindwa vipi kuling'amua hili hata pale alipokuwa Waziri katika wizara ya Maji na Nishati kwa miaka 6? Je si yeye au katika uongozi wake ndipo Tanzania iliingia mkataba na IPTL hata kama alikwisha hama Nishati, lakini si alikuwa Hazina alipoidhinisha fedha?

Leo anapojitapa na kujisifia kuzalisha umeme wa megawati 300 kwa kipindi cha miaka minne, je umeme huo uko wapi leo hii ikiwa tunaambiwa hakuna mafuta na gesi ya kutosha na mitambo mingine ni mibovu? Je atatuambia nini ilhali inafahamika wazi kuwa hizo megawati 300 zimanuka harufu ya rushwa na hujuma kama Dowans?

Anapodai kuwa mitambo ya kuzalisha umeme haijengwi siku moja, je kasahau kilio cha Mchungaji mwaka 2006 alipoomba Rais akutane na GE akienda Marekani kwa swahiba wake George Bush?

Kama yeye ni kiongozi makini, je tatizo hili la umeme kalivalia njuga gani? Mbona Kenya wamejenga mfumo wa umeme wa Upepo kwa miaka mitatu bila kutokwa jasho au kusubiri upungufu wa maji na ukame waanze kuhaha kutafuta miradi uchwara ya kuzalisha umeme?

Kama yeye ni kiongozi fanisi, je mbona hajatumia ile methali ya kinga ni bora kuliko tiba kwa kuwa mstari wa mbele kuagiza hiyo mitambo ambayo haiuzwi kama shati la mtumba?

Rais Kikwete ametudhihaki Watanzania na kukishusha hadhi cheo na dhamana aliyopewa. Na zaidi, ameonyesha wazi dharau yake pale alipoamua kumuonyesha dharau ya wazi Mbunge Mnyika na kumfanya aonekane ni mwendawazimu ilhali ni viongozi wake na uongozi wake uliojaa ahadi za uongo, uvivu na ukosefu wa umakini katika kufanya kazi.

Lakini, sitaendelea kumchutumu sana, maana niliiona hili la uongozi wa kizembe tangu awali.

Majibu aliyotoa yanaonyesha ni Kiongozi asiyejali lolote linalotokea ndani ya nchi, haelewi kwa nini Tanzania ni masikini, anawabembeleza wahalifu wajisalimishe, uchumi unadidimia lakini yupo tayari kuzitumbua fedha zaidi kwa safari, semina na vikao vya kufundishana kazi na kuvuana magamba huku akilalamika na si kuonyesha ushupavu an umadhubuti wa kuwa Rais na hata mwenyekiti wa Chama chake CCM.

Watanzania tumevuna tulichokipanda! Wala tusiwalaumu CCM pekee yaom bali ni sisi sote kama Taifa kwa kukubali kwa umoja iwe ni kupitia kura zetu za ndiyo au hapana, au hata kuendelea kutazama uongozi huu wa awamu ya nne ukijiendeaa tuu kama jongoo au konokono bila kuelewa ni wapi dira inasema tuelekee.

Tumelelea mfumo mbovu wa watu kutokuwajibika, na haya ni matunda ya watu wasiowajibika au hata kuogopa kuwa wana wajibu wa kuwajibika kwa dhamana na kazi walizopewa.

Haijali ni nani atakuwa Rais wetu 2016, lakini kwa mwendo huu wa uongozi huu tuliouona na watu ndani ya chama cha CCM na hata Serikalini watu wanakubali kuburuzwa na kiongozi asiye makini na mwenye silika za uzembe na masikhara kama haya, basi safari yetu ni ndefu mno.

Ili kuelewa kuwa tunaongozwa na mtu asiyethamini dhamana aliyopewa, tafakari vicheko vya dharau au masikhara alivyofanya wakati akiulizwa maswali ya msingi kuhusu tatizo hili la ukame.

Ama kweli Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu!

Mkulu alikuwa anarap au maana sikuelewa alichokuwa anaongea mie...kila kitu unajua sisi, unajua sisi, wewe nani? Rais hatuna tena hatuna na hatuna.....
 
Nikimwangaliaga huyu Mkwer.e kwenye TV naishia kucheka tu! Nadhani mnajua sababu.

Si bora wewe unacheka mimi nashikwa na Hasira natamani nimrukie na kuanza kumchapa Makonde. Kwanza hata kwenye hii Post nimeshikwa na hasira Juzi niliona gazeti lina picha yake nikalichoma moto jinsi nisivyompenda kwa ajili ya kuliagamiza Taifa langu. Aaggghhhhh anatia Kinyaa ni bora ukanyage mavi kuliko kuiona picha yake
 
Madhara ya kuwachagua viongozi waliomwamgusha mwalimu ndo haya.Hii kauli ya kejeli si mpya kwa viongozi waliomrithi mwalimu.Ni kauli zilizokuwa zikitolewa na viongozi hao toka wakiwa mawaziri.Hata Christian Kisanji alishawahi kutoa kauli kama hizi kipindi alipokuwa waziri wa maji chini ya Mwinyi.Nilikuwepo huko Same Sekondari na ziara ya waziri huyo tuliisubiria tukidhani itakuwa ya matumaini kwa kusikilizwa vilio vyetu vya ukame wa maji wa kupindukia na kuja na solutions.

Nakubaliana na ukweli kwamba tunavuna tulichopanda.Sioni vongozi kabisa.

Kwa upande mwingine,nimesoma mahojiano na BBC nimechoka.Tofauti na wengineo,kwangu ni vigumu kuamini kwamba hizo ni kauli za viongozi waliopewa dhamana.Siamini kabisa kuwa Tanzania haina watu wenye kufikiri beyond this.Wenye kuweza kutufanikisha hawapewi nafasi.Na ukiangalia,wananchi milioni 40 wanachaguliwa viongoz/Kiongozi na wananchi milioni 4 tu,yani ten pasenti ya wananchi wanawatuvunisha milioni arobaini haya makapi.
 
Nikirejea mahojino kati ya Rais Kikwete na mwandishi wa BBC majuzi kuhusiana nasuala la umeme, hisia kadhaa zinakuja akilini mwangu, masikitiko, kicheko na hasira!Kama nilitarajia majibu yenye kuleta maana, basi nilikosea sana, lakini sikutegemea kuona majibu yaliyokosa busara na umakini na zaidi uungwana wa kukiri kuwa kuna makosa katika mipango na utekelezaji wa kazi katika uongozi wa ais Kikwete.Ingekuwa rahisi sana kwa Kikwete kupokelewa kwa kusamehewa kama angekiri wazi kuwa Serikali yake ilifanya makosa katika mipango hii ya kuzalisha umeme na angejibebesha msalaba mzima na kusema tumeanza kazi mpya na tutaliangalia kwa upya kwa kasi, basi tungemuelewa.Lakini Rais kajibu kwa ghadhabu, kiburi, kejeli na masikhara. Zaidi anawabeza wale wanaohoji kwa nini bado tunaendelea na tatizo hilo.Cha kusikitisha ni Rais kulaumu mvua na ukame na hata kudai Serikali haiwezi kuleta mvua. Swali langu kwa Rais KIkwete, leo hii ambapo inafahamika wazi dunia nzima kuwa kuna mizunguko ya hali ya hewa ambayo imevurugika, somo la njaa na ukame wa mwaka 1974, 1984, 1994 na hata miaka ya 2000, halijaingia katika akili za watawala au mtawala wetu?Yeye si Mchumi, je wachumi si watu wanaobobea katika takwimu na mipango? Je alishindwa vipi kuling'amua hili hata pale alipokuwa Waziri katika wizara ya Maji na Nishati kwa miaka 6? Je si yeye au katika uongozi wake ndipo Tanzania iliingia mkataba na IPTL hata kama alikwisha hama Nishati, lakini si alikuwa Hazina alipoidhinisha fedha?Leo anapojitapa na kujisifia kuzalisha umeme wa megawati 300 kwa kipindi cha miaka minne, je umeme huo uko wapi leo hii ikiwa tunaambiwa hakuna mafuta na gesi ya kutosha na mitambo mingine ni mibovu? Je atatuambia nini ilhali inafahamika wazi kuwa hizo megawati 300 zimanuka harufu ya rushwa na hujuma kama Dowans?Anapodai kuwa mitambo ya kuzalisha umeme haijengwi siku moja, je kasahau kilio cha Mchungaji mwaka 2006 alipoomba Rais akutane na GE akienda Marekani kwa swahiba wake George Bush? Kama yeye ni kiongozi makini, je tatizo hili la umeme kalivalia njuga gani? Mbona Kenya wamejenga mfumo wa umeme wa Upepo kwa miaka mitatu bila kutokwa jasho au kusubiri upungufu wa maji na ukame waanze kuhaha kutafuta miradi uchwara ya kuzalisha umeme?Kama yeye ni kiongozi fanisi, je mbona hajatumia ile methali ya kinga ni bora kuliko tiba kwa kuwa mstari wa mbele kuagiza hiyo mitambo ambayo haiuzwi kama shati la mtumba?Rais Kikwete ametudhihaki Watanzania na kukishusha hadhi cheo na dhamana aliyopewa. Na zaidi, ameonyesha wazi dharau yake pale alipoamua kumuonyesha dharau ya wazi Mbunge Mnyika na kumfanya aonekane ni mwendawazimu ilhali ni viongozi wake na uongozi wake uliojaa ahadi za uongo, uvivu na ukosefu wa umakini katika kufanya kazi.Lakini, sitaendelea kumchutumu sana, maana niliiona hili la uongozi wa kizembe tangu awali. Majibu aliyotoa yanaonyesha ni Kiongozi asiyejali lolote linalotokea ndani ya nchi, haelewi kwa nini Tanzania ni masikini, anawabembeleza wahalifu wajisalimishe, uchumi unadidimia lakini yupo tayari kuzitumbua fedha zaidi kwa safari, semina na vikao vya kufundishana kazi na kuvuana magamba huku akilalamika na si kuonyesha ushupavu an umadhubuti wa kuwa Rais na hata mwenyekiti wa Chama chake CCM.Watanzania tumevuna tulichokipanda! Wala tusiwalaumu CCM pekee yaom bali ni sisi sote kama Taifa kwa kukubali kwa umoja iwe ni kupitia kura zetu za ndiyo au hapana, au hata kuendelea kutazama uongozi huu wa awamu ya nne ukijiendeaa tuu kama jongoo au konokono bila kuelewa ni wapi dira inasema tuelekee.Tumelelea mfumo mbovu wa watu kutokuwajibika, na haya ni matunda ya watu wasiowajibika au hata kuogopa kuwa wana wajibu wa kuwajibika kwa dhamana na kazi walizopewa.Haijali ni nani atakuwa Rais wetu 2016, lakini kwa mwendo huu wa uongozi huu tuliouona na watu ndani ya chama cha CCM na hata Serikalini watu wanakubali kuburuzwa na kiongozi asiye makini na mwenye silika za uzembe na masikhara kama haya, basi safari yetu ni ndefu mno.Ili kuelewa kuwa tunaongozwa na mtu asiyethamini dhamana aliyopewa, tafakari vicheko vya dharau au masikhara alivyofanya wakati akiulizwa maswali ya msingi kuhusu tatizo hili la ukame. Ama kweli Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu!
Pole mkuu wengi tumesikitika sana kwa ile interview...it was a terrible one...arrogance, incompetence, disregard for people who are suffering because of power shortage...you name it...he simply showed the world that he as president of the country had no idea of the consequence of power shortage to economy of TZ..
 
Kikwete ni Zigo tulijadili sana kwenye thread alianzisha Pasco hapa tutalibeba lakini likizidi uzito tutalibwaga ,KIKWETE ni disaster Dunami bin sunami maafa zaidi yaja unaona serikali ilivyofilisika
 
Back
Top Bottom