Majibu ya Kigwangalla: Kwa Nini Sikusaini Hoja ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (MB)!

Mkuu...
Si ukae kimya mbona unatafutia watu ban hapa..

Halafu inaonekana umeridhika sana..
Brother, waliopo CCM pia ni wananchi wa nchi hii hii, na ninakuhakikishia kabisa kwamba ndani ya wabunge wa CCM kuna watu wazuri sana, tena wazalendo kupita kiasi kuliko unavyotaka kufikiri, na ndiyo maana tunaendelea kuchaguliwa na wananchi. Suala la kusaini ama kutokusaini ni la kiutaratibu na kwa mfumo tulionao si sahihi kwa MB wa CCM kupiga kura ya kitu kizito kama hicho bila kuangalia msimamo wa chama chake. Kusimamia mambo ya kitaifa na hata kuunga mkono hoja za kambi ya upinzani kwenye mambo madogo madogo inakubalika lakini siyo kwenye mambo kama haya, hili la kutokuwa na imani na WM!!!! Hata kama CHADEMA wangekuwa wanatawala wasingekubali hilo...
 
Hivi unamshauri kweli wewe?? anyway hiyo point namba 3 inaonyesha kama una miaka 16 hivi!! afu kama vile umemaliza STD VII B.
 
nimekuelewa mkuu unamaanisha ccm kwanza na nchi baadaye sawa kabisa dr na waziri mtarajiwa wa tanzania

...which is sad kwa mtu anayeaminika kuwa amekwendaa shule, isn't it??

ubinafsi utaendelea kuwa kansa mbaya hapa kwetu, hususani culprits wakiwa ni wasomi kama hawa.
uchumi mzuri wa viwanda na biashara aliouasisi mwl nyerere vyote viliuliwa na wasomi wa aina hii.

tunahitaji tingatinga tu nchi hii ili wasomi kama huyu ndugu wa-wake up from their slumber!

that's why i like aggressiveness ya the likes of dr slaa, magufuli or even that boy lema!
hizi ndio tingatinga zinazoweza ku-pump sense into these educated but brainless heads!
 
Unafiki ni utovu wa ukweli katika mwenendo wa binadamu hasa kwa lengo la kujipatia sifa, k. mf. kama mwanadini mwadilifu wakati sio, kampa mpinga ufisadi wakati kwa ndani sio hivyo nk.
Tofauti na mkosefu, mnafiki anatenda vema kwa nje, lakini nia yake si kufuata dhamiri yake na maadili anayojua ni mazuri, bali ni kupendeza watu wengine ili kupata faida fulani kutoka kwao.
Ni jambo linalolaumiwa sana katika dini zote, hasa Ukristo, kutokana na lawama za Yesu dhidi ya viongozi wengi wa Uyahudi. Injili zinasisitiza hasa lawama zake dhidi ya baadhi ya Mafarisayo. Kwa maelezo haya wewe mnafiki tayari hata kwa maelezo yako yanajichanganya; mbona caucus ilifail; mbona hamna kauli kulaani ukimya wa mawaziri it means mlidanganywa na hamuwezi kusema kitu; hovyo mtu mzima
 
I am disappointed by you Honourable and a Colegue.......ni kweli kabisa umekataa kuwa mnafikia na bila kumumunya maneno umesema.....Chama kwanza Taifa baadae and for me this is a Great disappointment from you!! I know you! Your better than This ila Hapa umeamua tena Makusudi kuweka Uchama mbele ya Utaifa.....Hivi madudu yote yale toka kwa Mawaziri wa serikali ya chama chako bado mnatanguliza chama mbele eti kwa sababu ya Technical Flawed of the motion??! U must be kiding Hon. MP!!
 
Watu kama nyie hamfai katika uongozi.
Inaonyesha jinsi gani haupo tayari kupokea mabadiliko.
Na vile vile umeridhika na serikali yenu isiyo sikivu kwa kukumbatia walafi na makupe waliopo nchini.
Huu ndo unafiki wenyewe.
Unachumia tumbo.
Kama Kumuangusha Waziri Mkuu na serikali yote Bungeni na kukimaliza kisiasa CCM si kuyapokea mabadiliko, basi nimeshindwa. wamekosea mawaziri watano (or rather wanane) wewe utake kuiangusha serikali yote, lini tutafanya mambo ya maendeleo? Mimi sikubaliani na huo mtazamo, na kwa kuwa nimeuweka wazi sina unafiki ndani yake, so just take it or leave it!
 
Bora ungeendelea kukaa kimya nayo ni busara kuliko kujibu uhalo huu.
 
Nafikiri ameongea anachosimamia yeye,hawezi kuSupport hoja yoyote inayotoka upinzani hata kama ni ya kujenga..hapa hatuna alternative nyingine zaidi ya kuwangoa madarakani warafi hawa.
 
Nimegafilika sana na huyu Shorobaro. Sijaelewa katika maelezo yake ni lipi la msingi aliloegemea. A hypocrite is Always a hypocrite

 
Ndugu zangu wanabodi,


Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.

Wakatabahu,
HK.

Shule gani uliokwenda wewe, vyeti na jina sio vyako. Peleka posti yako ktk facebook,sio hapa.
 
Kumbe still ni mnafiki uko radhi kuoana watanzania wanaumia,ili kulinda ubunge wako.
 
Tumekusikia tumekuelewa. Pamoja na kuhamasisha maandamano kule Nzega na kuwekwa ndani na polisi, unaiamini serikali yako ya CCM. Kama katika dini kupinga maamuzi ya serikali tena kwa maandamano ni kuiamini, thats funny. Mwisho wa siku umedhihirisha kauli ya ndege wafananao ndio warukao pamoja. "CCM ana imani na CCM, ana imani na serikali ya CCM, huu wizi mdogomdogo utamalizwa na serikali yake pendwa ya CCM". Lakini kihistoria tu, ulianzia mbali sana kidogo kidogo, watu walifoji risiti za manunuzi, enzi ya mzee ruksa, wakafumbiwa macho. Wakapiga EPA, Meremeta, Kiwira ukaitwa kelele za mlango!!!! Sasa wameamua kuuza na miundombinu kabisa Reli, Bandari, viwanja vya ndege. Vimeisha wameamua kushambulia kodi ya wananchi kwa matumizi hewa mpaka wizi kufikia matrilioni ya pesa, huyu dokta bado anaona ni hali ya kawaida sana serikali yake itaimudu. Siku mtakaposikia zimenunuliwa ndege za kivita hewa, na vifaru vya bandia nadhani ndipo tongotongo zitawatoka machoni. Wakati huo nchi imebaki na jeshi lenye silaha bandia. Pole HK.
 
Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo.

Pili, naamini na ninakubali, na kwa hakika ninakerwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana za kuongoza baadhi ya ofisi nyeti za umma wametuangusha watanzania, na hivyo naunga mkono hoja ya kutaka kuwatoa hawa.

Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama Mhe. Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, na kimkakati zaidi angewapa wabunge wa CCM walioibua hoja hizo za kuwataka mawaziri wang'olewe na hapo angefanikisha malengo ya kumuondoa WM na serikali yake Bungeni. Kwa namna ilivyo hawezi kupata support ya wabunge wa CCM na kwa kuwa sisi ndiyo majority, hoja hiyo haitopita

Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao.

Wakatabahu,
HK.

Sina uhakika sana kama mh. HK ulipitia maneno yako kabla ya kumpatia secretary wako akuchapie na ayaweke hapa JF. Maana contradiction zilizomo zinazihirisha wewe ni mnafiki na huna msimamo upo radhi kuikumbatia serikali yako hata kama imefanya madudu bila kujali maisha ya watz wenzako ambayo yanaathirika kutokana na madudu ya serikali yako. Serious ninajua unafanya hivi ili rais akufikirie atakapo amua kuunda baraza jipya la mawaziri but your deadly wrong for that stand.

Ninajua haya ni maoni yako binafsi na tunayaheshimu ila yametusaidia sana kujua kijana kama wewe unasimamia msimamo gani linapokuja swala la chama na maslahi ya taifa kwa pamoja
 
Brother, waliopo CCM pia ni wananchi wa nchi hii hii, na ninakuhakikishia kabisa kwamba ndani ya wabunge wa CCM kuna watu wazuri sana, tena wazalendo kupita kiasi kuliko unavyotaka kufikiri, na ndiyo maana tunaendelea kuchaguliwa na wananchi. Suala la kusaini ama kutokusaini ni la kiutaratibu na kwa mfumo tulionao si sahihi kwa MB wa CCM kupiga kura ya kitu kizito kama hicho bila kuangalia msimamo wa chama chake. Kusimamia mambo ya kitaifa na hata kuunga mkono hoja za kambi ya upinzani kwenye mambo madogo madogo inakubalika lakini siyo kwenye mambo kama haya, hili la kutokuwa na imani na WM!!!! Hata kama CHADEMA wangekuwa wanatawala wasingekubali hilo...

Hujajibu swali, Je linapokuja swala la maslahi ya Taifa regardless ya "UCCM na UCDM" kama hili unasimamia wapi?
 
Alichojitetea kingwangwala ( ambaye yupo kwenye kundi la hawa kupe(ticks)) ni sawa kwa akili zake zilizo jaa ubinafsi na kwa masilahi yao, Lakini lengo letu sisi na Akina Zitto pamoja na wale waelewa wachache waliosaini kutoka kwenye hilo kundi ni kuhakikisha hao ticks hawatudhulu,,,,,,, inatosha sasa.

Kingwangwala umefanya nini wewe kama wewe kuhakikisha walichofanya watendaji(mafisadi) wa chama chenu wame adabishwa kwa mujibu wa sheria kama kweli unaguswa na ubadhilifu wao?
 
Dr.HK naona umesahau ulikotoka,nilifikiri sasa umebadilika, but now nimekuelewa vizuri wewe ni mtu wa namna gani.upo pale mjengoni kwa ajili ya maslahi yako binafsi like u were before. nakushauri tu mhe.embu rudi nyuma na fikiria kwa makini maana ya utaifa (patriotism) then njoo tena na hizo hoja zako tatu. Tanzania tumeikuta,itakuwepo na itaendelea kuwepo hata for generations to come! CCM itapita tu na itaondoka tu tena very soon.
 
I am disappointed by you Honourable and a Colegue.......ni kweli kabisa umekataa kuwa mnafikia na bila kumumunya maneno umesema.....Chama kwanza Taifa baadae and for me this is a Great disappointment from you!! I know you! Your better than This ila Hapa umeamua tena Makusudi kuweka Uchama mbele ya Utaifa.....Hivi madudu yote yale toka kwa Mawaziri wa serikali ya chama chako bado mnatanguliza chama mbele eti kwa sababu ya Technical Flawed of the motion??! U must be kiding Hon. MP!!
Pole sana Colleague, this is another game, its politics and I know how to play the game...trust me. Zitto hayuko serious, anafanya game ya kisiasa kutuingiza kwenye excitement ya bure, sasa mimi huchagua kadi zangu za kucheza vizuri kadri moyo wangu unavyonituma, na safari hii sikuingia kwenye bandwagon ambayo ninajua haitotufikisha kwenye lengo la kumtoa Waziri Mkuu! Najua Mawaziri watatolewa lakini siyo WM, na mimi ningefurahi sana kuona Rais akiwatoa baadhi ya Mawaziri wenye tuhuma lakini siyo kuanza kuvunja Baraza la Mawaziri, kuturudisha nyuma tena....naangalia mambo ya gharama na stress itakayokuwepo nchini kwa action hiyo...mtazamo wangu tu huu, na siyo lazima watu hapa, hata wale wa CHADEMA, wataukubali!
 
Kumbe still ni mnafiki uko radhi kuoana watanzania wanaumia,ili kulinda ubunge wako.



Ndugu Kigwangalla, Kigwangalla, ungetafuta njia nyingine ya kuomba uwaziri labda kupitia mama Salma maana huko nyuma iliwahi kuandikwa kuwa uko karibu nae kuliko hii njia uliyotumia,

Anyway lakini cha ajabu unaweza kuta kweli JK akupatia uwaziri Makubwa na hakika umejimaliza hutapta ubunge tena 2015 labda wanachi wako wasiyasikie na kuyaona majibu yako haya!!
 
Back
Top Bottom