Wewe bora ukae kimya, umechemka kupita maelezo.here was just my strategic choice, kwani kuna nini hapa? anyway, hata kule nimebandika majibu pia, tatizo Dr. hujaenda kusoma kule
Mkuu..una akili iliyopofuka, unafikira rojo mithiri ya ute wa yai, unatazama mambo kwa macho yaliyojazwa kiwi, una tongotongo za tamaa za madaraka kwa jasho la walalahoi wa taifa letu, anayaona mambo katika sura ya ccm kwanza, taifa baadae.
anawaza kimasikini, anajivika kilemba cha uchapakazi na kutetea vibovu, anasema anakwaza na baraza la mawaziri bila kukerwa na alieliteua baraza hilo, haiwezekani ukawa unaumizwa na rushwa halafu anaeilea rushwa akawa rafiki yako. ...huu ni unafiki, uzandiki na ubinafsi wa kiwango cha juu.
Hivi kweli wewe una fikra huru??
Wewe inamaana hata ukiona nchi imetafunwa na nyie mchwa utakaa kimya kwa sababu Serikali ni ya chama chako??
Vipi kuhusu vile vimisemo vyenu vya 'Taifa mbele, Chama baadaye'??
Unaelewa maana ya concept ya 'Tanzania ilikuwepo kabla ya CCM'??
Nadhani ndio maana ulibebwa kwenye kura za maoni, hufai kuwa hata balozi wa nyumba kumi!!
Brother, waliopo CCM pia ni wananchi wa nchi hii hii, na ninakuhakikishia kabisa kwamba ndani ya wabunge wa CCM kuna watu wazuri sana, tena wazalendo kupita kiasi kuliko unavyotaka kufikiri, na ndiyo maana tunaendelea kuchaguliwa na wananchi. Suala la kusaini ama kutokusaini ni la kiutaratibu na kwa mfumo tulionao si sahihi kwa MB wa CCM kupiga kura ya kitu kizito kama hicho bila kuangalia msimamo wa chama chake. Kusimamia mambo ya kitaifa na hata kuunga mkono hoja za kambi ya upinzani kwenye mambo madogo madogo inakubalika lakini siyo kwenye mambo kama haya, hili la kutokuwa na imani na WM!!!! Hata kama CHADEMA wangekuwa wanatawala wasingekubali hilo...Mkuu kwanza nikupongeze kwa kuja kuleta majawabu sawia!
Ingawa siwezi kuthubutu kukuita mnafiki kutokana na ukubwa wa neno hili kwa muumba, ila naona kama kuna sehemu sijakufahamu vyema kauli yako kwamba
"Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM",
Wasiwasi wangu katika hili ni je ikiwa mambo hayo ambayo kimsingi yanakubaliwa na ccm yatakuwa yanaenda kinyume na matakwa ya wananchi itakuwaje hapo? mfano tunajua kuwa uongozi ni dhamana na ubadhirifu ni kukosa unaminifu na ni dalili ya unafiki kwa kutenda kinyume na dhamana hapo inakuwaje kaka yangu hebu nijibu tafadhari?
" Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic "
Lakini pia katika dhana hiyo hiyo ya kuungana na yatokanayo na chama chetu "CCM" na kutokubali hoja iliyotoka upande wa pili, napo ninaomba unipe ufafanuzi mzuri, naamini kabisa pamoja na sababu chafu na agenda zingine za vyama vyetu vya upinzani lakini bado kuna masuala yalio sahihi na yanayogusa maslah ya umma,
Huenda hoja iliyoanzishwa kwa upande mmoja ikapelekea kuwapa ushindi wa kisiasa wapinzani lakini swali langu kwako Mh. Ni upi msimamo wako pale hoja inapoletwa na wapinzani ikawa ina maslah makubwa kwa taifa lakini itakipunguzia nguvu chama chetu CCM, utaunga mkono hoja au kupinga? na kama ni lazima uitetee serikali yako huoni kama kwa hilo huwatendei haki wananchi?
Best
Tume ya katiba
mbona unajichanganya sana? Hueleweki mbona?!!!!a hakuwa na u-seriousness wa kutaka kweli kumuondoa wm bali ni baadhi ya mawaziri, sema alichomeka tu hiyo kauli ili kutia presha zaidi!). Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama mhe.
Hk.
Najisikia kuugua ghafla baada ya kusoma unafiki huu
na nahisi nikiendelea kuusoma nitajibu ovyo na kutukana na nitaishia kupata BAN
Bora niende kwenye kjukwaa jingine kabisa
here was just my strategic choice, kwani kuna nini hapa? anyway, hata kule nimebandika majibu pia, tatizo Dr. hujaenda kusoma kule
Hukuweza kusaini karatasi ya Zitto kwa sababu ni 'sawa na kukata mti uliokalia'. kwa hapa ndugu nimekuelewa. Hofu ni haki ya kila mmoja na hasa linapokuja suala la kuchagua. Ulikuwa na hofu na huoni maisha nje ya baraza hili na serikali hii na kwa maana hiyo hata kelele na misimamo yako ya kutetea wananchi wa Nzega kupata faida na utajiri unaowazunguka (rejea msimamamo wako kwenye Resolute co.) ilikuwa ni kuzuga tu!
Kazi njema bwana HK, na ukweli ni kuwa pamoja na kuwa umeingia ndani, bado tunaona umekanyaga kapeti letu na viatu vyako vichafu'
Kama huna utetezi ni bora kunyamaza.
Utetezi wa aina hii hauna tofauti na ule wa Nundu!!
Tawi ulilokalia sio? Mkono unaokulisha sio?
Tutang'oa mtu wote tuone utakula wapi!