Majamaa walioingilia Mitikasi ya watu na hawakuachwa Salama

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,864
Basi tu, tuseme hii dunia kuna watu wanapanga mipango yao lakini kuna watu pia wanapangua mipango hiyo yote na kufanya mambo yao.

Kuna mambo huwa hutakiwi kuyaingilia hata kidogo. Hata kama utakuwa rais, kuna system huwa unaikuta, unatakiwa kuiacha kama ilivyo kwa kuwa ni maslahi ya watu wachache waliokufanya kuwa madarakani.

Hiyo ndiyo dunia ilivyo. Kuna watu wanakupambania, basi unapoona kwamba kweli umepambaniwa, usiwabadilikie hao watu, ungana nao hata kama wanafanya uovu.

Sasa sikia! Pale nchini Marekani kuna marais wawili tu ambao waliuawa wakiwa madarakani. Elewa neno kuuawa na si kufa. Rais wa kwanza alikuwa Abraham Lincoln ambaye alikuwa ni rais wa 16 wa nchi hiyo.

Huyu jamaa pale Marekani wanamkubali sana, alikuwa bonge moja la rais ila aliwakera baadhi ya watu baada ya kusimamisha biashara ya utumwa.

Mchizi alianza kuutumikia urais kuanzia mwaka 1861 mpaka 1865. Aliuawa kwa kupigwa risasi ya kisogoni ikulu bila shaka. Sasa chanzo cha kuuawa kwake ni hilo suala la kusimamisha biashara ya utumwa.

Wakati huo biashara ilikuwa kubwa sana, watu walipiga sana pesa kwa kuwauza akina Mhaya kutoka Tanganyika na kuwapeleka huko Liberia kabla ya kuwaingiza ndani ya meli na kwenda US.

Sasa mchizi alipoingia madarakani, akakemea biashara ya utumwa, tena ilikuwa ukikutwa unaifanya aisee msala unao, halafu wale watu waliokuwa wakiwatesa watumwa na kuwamaliza, walikuwa wakisakwa wauawe.

Nadhani ushawahi kuiona muvi ya Django, yule Mzungu alipokuwa akiongea na watu alisema ana barua kutoka kwa Lincoln kwamba wale watu waliokuwa wameua watumwa walitakiwa kuuawa, sasa pale unapolisikia jina la huyo rais basi jua ndiyo alikuwa ameisimamisha rasmi biashara hiyo ya utumwa.

Sasa machizi walipoona amezingua kwa kufanya hayo maamuzi, mchongo ukapigwa, mtu akasetiwa kwa ajili ya kwenda kummaliza, alipigwa risasi ikulu kwa nyuma na kufariki dunia, tena mbele ya mkewe.

Sasa bwana! Miaka ikaenda na kwenda na ikakatika. Ilipofika mwaka 1961 kijana machachari, John F. Kennedy akachukua kiti cha urais wa nchi hiyo. Mchizi alikuwa msela tu, mchizi boti halafu alikuwa mzee wa totozi.

Unamkumbuka Marlyn Monroe? Niliwahi kuandika kwa kifupi kuhusu stori yake humu. Alikuwa demu fulani mkali kama Beyonce, na kipindi hicho ndiye alikuwa staa kuliko mademu wote, na alikuwa mrembo mno. Sasa huyu rais alikuwa anapiga kisela hapo.

Sasa Kennedy baada ya kuingia madarakani, kosa kubwa alilolifanya ni kuwatetea watu weusi. Unajua sisi watu weusi hutakiwi kututetea, ukijaribu kufanya hivyo lazima watu wakupeleke kaburini.

Sasa yeye akaanza kututetea, akasaini mikataba mingi ya kuwatetea watu weusi, na kipindi hicho ndipo kukawa na wanaharakati wengi wa kututetea weusi, wakaibuka akina Martin Luther, Huey P. Newton, Bobby Seale, Elbert Howard na wengine wengi. Pia wakaanzisha vikundi vya kutetea watu weusi kikiwepo kile cha Black Panther.

Tafuta muvi ya Judah and Black Messiah ujifunze zaidi.

Huyu Kennedy alitupa nguvu kubwa sana watu weusi, wengi tukaingia barabarani na kudai haki zetu za msingi. Sasa Wamarekani walipoona vile, wakaona hii siyo, akiwa kwenye gari lake, pembeni ya mkewe, naye akala shaba ya kichwa na kufariki dunia.

Kilichowaua kilikuwa ni usaliti. Watu walikuwa na mitikasi yao lakini wao walipoingia madarakani wakataka kuiharibu hiyo mitikasi. Wakapigwa risasi na kufariki.

Kuanzia mwaka huo, Marekani wakatangaza kwamba hakutokuwa na rais yeyote yule ambaye atauawa akiwa madarakani. Na hiyo imedumu mpaka leo hii.
 
We jamaa punguza kutafuta kick, ukitaka umaarufu jaribu kuandika maudhui ya kueleweka, story zako zimezoeleka humu jaribu kuja na vitu vipya. NI USHAURI TU
 
We jamaa punguza kutafuta kick, ukitaka umaarufu jaribu kuandika maudhui ya kueleweka, story zako zimezoeleka humu jaribu kuja na vitu vipya. NI USHAURI TU
Staki ushahuri wako
 
Hao niliowazungumzia ni waliuwawa kwa sababu za kujaribu kutetea watu weusi kuwa huru... Kitendo cha kutaka kuharibu biashara za maboss wengi walijimilikisha watu weusi kama watumwa
Acha kupindisha maneno. Ulisema hivi:

Sasa sikia! Pale nchini Marekani kuna marais wawili tu ambao waliuawa wakiwa madarakani. Elewa neno kuuawa na si kufa. Rais wa kwanza alikuwa Abraham Lincoln ambaye alikuwa ni rais wa 16 wa nchi hiyo.
 
Back
Top Bottom