Maisha yangu na baada ya miaka 50

Patrick Rugemalira - Huyu jamaa yupo Minneapolis, Minnesota.

Penina Mhando - Prof. Penina alihamia Nairobi na bado yupo na masuala yake ya
ualimu na uandishi wa vitabu nafikiri amerudia jina lake la Mhando
kama sio Mlama.

Norman Sabuni - Alisoma huko Eastern Europe nafikiri bado yupo Lugalo Hospital
ni Daktari hapo.

Zuberi Zayumba - Huyu Jamaa nami nafahamiana nae vizuri tulipoteana muda mrefu,
tulionana mwaka jana Arusha katika Msiba wa James Mgani,Zuberi
yupo Sigara na anaishi Tabata.

Rosemary Tesha - Ni mke wa Leodgar ,huyu mama yupo Hazina

Naona hii List ni watu wa Chang'ombe miaka ya 70 enzi za safari Tripers na Timu ya Soccer Avengers!!
Zuberi Zayumba Alisha tangulia mbele ya haki.
 
Ongera kaka, na haswa kwa kuwa na kumbukumbu kubwa ya kuwakumbuka wale uliowahi soma nao zaidi ya miaka 35 nyuma.
Wengi wa vijana hivi leo kumbukumbu ya miaka 10 nyuma ni mtihani kwao.

Katika hao school mate wako ninamfahamu mmoja Zuberi Zayumba, huyu jamaa niliwahi fanya naye kazi... Nadhani mdau mmoja amekwisha kukudokeza wapi alipo. Nakumbuka pia huyu jamaa alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kuchangisha fedha kwa ajili ya timu ya taifa, na pia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Executive Sport Marketing (ESM) hapo Dar. Kwa wakazi wa yale maghorofa ya Tabata Sigara watakuwa wanamfahamu, jamaa ni mtu poa sana.

Ongera kwa mara nyingine tena...! Stay strong... Mzee wa pale pa Mfaranyaki!
Zuberi Zayumba alishatangulia mbele ya haki.
 
Namkumuka sana Vero sijui yuko wapi sasa, not seen her for the last 37-40 years!
Aliolewa na bwana mmoja wa kinyakyusa walikuwa majirani,nyumba zao zilikuwa zinapakana,akiitwa Brown,nakumbuka yule mumewe Alisha tangulia hakini,kuna kipindi enzi zile za ndege ya alliance yule Vero alikuwa na mdogo wake alikuwa cabin crew nilipanda ndege akanikumbuka ndio akanieleza hayo.
 
Watu wa zamani walitoka vizuri sana cv zao haziongopi yaani walio bahatika form 6 miaka mi5 ya mwanzo baada ya mkoloni kuondoka mpaka miaka ya 90 hivi walipata kilicho bora na hawa ndio waliofanya baadhi ya shule zinavuma mpaka sasa.Nawakubali sana.
 
...ASANTE SANA kwa yule aliyeutafuta na kuibua tena uzi huu Miaka 7 baada ya mimi kuuanzisha! maisha yanasonga mbele, na wiki iliyopita nimetoka kusherehekea miaka 57 ya kuzaliwa. ASANTE MUNGU. katika kipindi cha Miaka 7 baada ya kuuweka uzi wangu huu hapa, nimeweza kukutana na Norman Sabuni, Zuberi Zayumba ambaye miezi kadhaa baada ya kukutana akafariki dunia na ikawa huzuni kubwa sana kwangu. R.I.P Zuberi Zayumba. nikapata pia kufahamu kuwa katika mihangaiko ya maisha we did work together with Annet Kibwasali at a certain communication company's office na kwamba pia alikuwa shemeji yangu! R.I.P Annet. Asante kwa JF. Life goes on...
 
Jamani H
...kama ulikuwepo mkuu! Safari Trippers walikuwa wakifanya mazoezi yao kwenye nyumba moja pale mitaa ya Chang'ombe Maduka mawili enzi hizo Tukipaita Uhindini!
Wimbo wa Georgina tumeanza kuusikia hapo hata kabla haujaingia Redioni! Hapo pia unazungumzia mambo ya akina Comets, Rifters na Sunburst!

Naomba nifafanue Mkuu. Huyu Penina Mhando ninayemzungumzia siye yule mama wa Chuo Kikuu ambaye enzi hizo tulikuwa tunamfahamu kutokana na kitabu chake cha 'Hatia' ambacho ni miongoni mwa vitabu tulivyokuwa tukipenda kuvisoma.
Penina Mhando aliyekuwa classmate wangu alikuwa anakaa magorofa ya NHC karibu na karibu na lile ghorofa la wachina!
jamani Huu uzi ulinipita. Mwalimu Baruti anaishi Kijitonyama na matoto wake Raymond Baruti. Dada yaowa kwanza Mary Baruti alifariki miaka zaidi ya 10iliyopita (RIP). Jaqulibe Baruti yuko Tanga.
Sakina Mkwawa Yuko TRA.
Umenikumbusha mbali saana , Chang'ombe Primary. nadhani ulisikia kuwa Florence Dyauli ( aliyekuwa TBC) alifariki.
Jamani kuna haja ya Ex-Chang'ombe Primary kukutana.Iliwahi kuwa arranged ila ni muda sasa haijafanyika.
Jordan Rugimbana Mkuu wa Mkoa Dodoma kwa sasa.
Dah FSafarii Trippers tulikuwa tunaenda kuwaangalia wanafanya mazoezi na wimbo wa Georgina ninaupenda sana na Georgina mwenyewe namfahamu ( naamnin Ex Changombe wengi wa kilindi kile wanamfanamu) yaani maisha yalikuwa mazuri wapiga bendi wanaapreciate mnavyoenda washudhudia wakipractice hamna hata hatari yoyote ooh those old good days!
 
...ASANTE SANA kwa yule aliyeutafuta na kuibua tena uzi huu Miaka 7 baada ya mimi kuuanzisha! maisha yanasonga mbele, na wiki iliyopita nimetoka kusherehekea miaka 57 ya kuzaliwa. ASANTE MUNGU. katika kipindi cha Miaka 7 baada ya kuuweka uzi wangu huu hapa, nimeweza kukutana na Norman Sabuni, Zuberi Zayumba ambaye miezi kadhaa baada ya kukutana akafariki dunia na ikawa huzuni kubwa sana kwangu. R.I.P Zuberi Zayumba. nikapata pia kufahamu kuwa katika mihangaiko ya maisha we did work together with Annet Kibwasali at a certain communication company's office na kwamba pia alikuwa shemeji yangu! R.I.P Annet. Asante kwa JF. Life goes on...
ooh jamani Zuberi amefariki may his soul rest in Peace!
 
...Lole, wewe kweli ni original Chang'ombenian! Miaka hiyo uliyomaliza nafikiri utakuwa ulifuatana fuatana na kina Andrew Simkoko na yule dada yake sikumbuki jina lake, akina Anet Kibwasali, kina Peter Makorongo (RTD!) na Tammy na wengineo.
Walimu wa Changombe walikuwa kweli ni very, very dedicated. nakumbuka shule ile ilikuwa inaongoza shule zote za jirani za kibasila, mgulani, wailes na kadhalika.
Nimesikitika sana kuhusu Mr. Nkani! Mwalimu alikuwa anajua kutembeza fito yule si utani!lakini pia alikuwa dedicated kwenye kazi yake.
Mwl Kirwanda alikuwa the Best. Unakumbuka kuwa ndio aliongoza halaiki ya MIaka Kumi ya Uhuru ambayo wengi wanaamini kuwa ndio ilikuwa the best kuliko zote zilizofuata baadaye?
Thank you Mkuu, kwa taarifa yako!
Yes Mr. Nkane alinifundisha hesabu dah. Alikuwa mkali siku ya zamu yake mapaka dada zetu na kaa walikuwa wanajua ni zamu ya mwalimu nani. Mr.Kirwanda mwalimu wa sayansi jamani. Mwaka wetu tulikuwa tunarudia mchana kwa ajili ya yeye kutufundisha. Sidhani kama nilikosa hata swalimoja la sayansi mtihani wa mwishona si peke yangu wengi. Alikuwa dedicated katika kufundisha ajamni! Nilikutana nae maiaka mingiiliyopita TPH , Samora akawa anamwambia Director wa TPH, hawa wakati nafundisha iikuwa inatokea hamna mwanafunzi anayefeli somolangu. Na Changombe Several times ( kabla ya hizi academia) ilikuwaga inaongoza Tanzania kitaaluma ( STD VII results) . Kijumla walimu walikuwa wanafundisha kwa moyo hasa.
mwalimu Matemu wakiswahili jamani hizo nahau anaziandika zoooote ubaoni na maaana zake! Dah
 
Dah uzi kama huu kapukuz wakiuona hata hawaelewi. Shikamoo BabaDesi :).
Tuombee nasi tuje na uzi kama huu siku moja:)

cc Bitoz
 
Jamani H

jamani Huu uzi ulinipita. Mwalimu Baruti anaishi Kijitonyama na matoto wake Raymond Baruti. Dada yaowa kwanza Mary Baruti alifariki miaka zaidi ya 10iliyopita (RIP). Jaqulibe Baruti yuko Tanga.
Sakina Mkwawa Yuko TRA....
....Asante sana mkuu mwana, nimefarijika mno kufahamu kuwa mama Baruti yupo hapo knyama tu! nitatafuta namna kwenda kumjulia hali tu. kuna faraja katika kumuona mwalimu aliyekufundisha 'domestic science' miaka 40 na zaidi nyuma ukiwa wewe si chochote si lolote wakati yeye tayari ni mtu mzima na wewe ni kama mwanae tu! yah! mwl Nkane na mkwara wake aliotoka nao National Service wa "Ntakuchuuna wee!"...nakumbuka aliwahi kumshikia bango binti mmoja aliyekuwa ameandika 'love and peace' kwenye kiatu chake hadi ikabidi binti aje na mzazi wake shule kutoa maelezo! wakati ule nidhamu ilizingatia hasa!
 
Haya ntakutumia number yake kwa PM. Kwa kweli ni jambo zuri sana na ukizingatia jinsi walivyokuwa wanajitoa kutufundisha!
 
...ASANTE SANA kwa yule aliyeutafuta na kuibua tena uzi huu Miaka 7 baada ya mimi kuuanzisha! maisha yanasonga mbele, na wiki iliyopita nimetoka kusherehekea miaka 57 ya kuzaliwa. ASANTE MUNGU. katika kipindi cha Miaka 7 baada ya kuuweka uzi wangu huu hapa, nimeweza kukutana na Norman Sabuni, Zuberi Zayumba ambaye miezi kadhaa baada ya kukutana akafariki dunia na ikawa huzuni kubwa sana kwangu. R.I.P Zuberi Zayumba. nikapata pia kufahamu kuwa katika mihangaiko ya maisha we did work together with Annet Kibwasali at a certain communication company's office na kwamba pia alikuwa shemeji yangu! R.I.P Annet. Asante kwa JF. Life goes on...
Anet ni yupi Mkuu?
 
Back
Top Bottom