Maisha yangu na baada ya miaka 50

Hongera sana kwa kukatiza nusu ya karne.
Noel Sabuni(a.k.a Nobi) huyu mheshiwa yupo Dar na Kampuni moja inayotoa huduma ya bima ya afya inayoitwa Prosperity Health. Yeye atakueleza kwa wakati huu mdogo wake alipo Norman kama bado yupo Lugalo au la.

MwK! Asante sana kwa Taarifa Hii! Nitaifuatilia.
 
Duh mkuu hongera zako, umenikumbusha usemi wa Confucius (551-479 BC) "At 50 I understood the mandate of Heaven". Kwa hivyo mkuu below 50 ulikuwa unajifunza, then sasa umeanza kuishi....!tehe tehe..
 
Nafurahi kuwajulisha wana JF kuwa tarehe 8 Juni mwaka huu 2009 nitakuwa natimiza miaka 50 toka nilipozaliwa. Miongoni mwa mambo ninayotaka kufanya ni kufahamu walipo watu ambao kwa namna moja ama nyingine nilikutana nao katika hiyo miaka 50 ya maisha yangu. Tafadhali kama unamjua mmoja wapo ama una taarifa zake nijulishe na kama wewe ni mojawapo basi tafadhali ni-PM. Natanguliza Shukurani.

Leo naomba nianze na orodha wa watu niliosoma nao Chang'ombe shule ya Msingi kati ya mwaka 1970 nilipohamia hapo nikitokea St Anthony Tanga (siku hizi ni Changa Primary School) hadi mwaka 1973 nilipohama kwenda Mfaranyaki Songea.

1. Mr Kirwanda - Mwalimu
2. Mr Nkani - ''
3. Mr Matemu - ''
4. Mr Sindamwaka - Mwalimu Mkuu
5. Mama Baruti - Mwalimu

Wanafunzi Wenzangu:

1. Norman Sabuni - alikuwa na kaka yake anaitwa Noel Sabuni na mdogo wake anaitwa Nina Sabuni. Kaka yao mkubwa alikuwa Raphael Sabuni wakati huo akiimbia STC Jazz na akina Marijani Rajab.

2. Hassan Zawayai
3. Zuberi Zayumba
4. Abraham Mwasongwe
5. Helena Sebastian
6. Gosbert Roderick na dada yake Esther Roderick
7. Georgina Rugimbana na dada yake Rosemary Rugimbana - walikuwa dada wa Jordan Rugimbana ambaye alikuwa nyuma yetu darasa moja na sasa ni mkuu wa Wilaya Kinondoni.

8. Mariam Himid
9. Lucy Mkande
10. Edith Masanja
11. Sarah Kilua
12. John Tesha
13. Rosemary Tesha
14. Mbiliyawaka Hango
15. Mohamed Adam
16. Patrick Rugemalira
17. Richard Kilandeka
18. Suna Said
19. Neema - jina la pili nimesahau lakini mama yake alikuwa
mwalimu hapo hapo Chang'ombe S/Msingi
20. Penina Mhando
21. Shabaani Mohamed na mdogo wake Faraji Mohamed
22. Selina Mkaja
23. Rizwan - Alikuwa muasia akiishi mitaa ya Chang'ombe
Jamatini.

Baba Desi nashukuru sana kwa kunikumbusha watu wengine ambao nilikuwa nimewasahau kabisa.
Nilimaliza hapo Chng'ombe Pr 1970 na Mwalimu Nkane alinipiga kibao cha sawasawa nikiwa darasa la 5-kwa kutoimba vizuri.Sikumsahau mwalimu huyu kwa ufedhuli ule na akinikuta Chuo Kikuu akiwa fresher nami nikiwa namaliza degree.
Nasikia amefariki dunia miaka kadhaa iliyopita.
Kirwanda .Sindamwaka , Matemu(Ole wako!!) Mama Baruti were all very good dedicated teachers , mazao yao yapo pote nchini
 
...kama ulikuwepo mkuu! Safari Trippers walikuwa wakifanya mazoezi yao kwenye nyumba moja pale mitaa ya Chang'ombe Maduka mawili enzi hizo Tukipaita Uhindini!
Wimbo wa Georgina tumeanza kuusikia hapo hata kabla haujaingia Redioni! Hapo pia unazungumzia mambo ya akina Comets, Rifters na Sunburst!

Zamani hizo kulikuwepo mchuano mkali sana kati ya Safari Trippers na Afro 70.
Mchuano ulikuwa mkali kiasi cha shule nzima nzima kuwa upande fulani wa vijana hao wa wakati ule.
Mchuano ule uliendeleza sana talents za utunzi na upigaji wa miziki kipaji kinachoelekea kupungua miaka hii.
 
Nafurahi kuwajulisha wana JF kuwa tarehe 8 Juni mwaka huu 2009 nitakuwa natimiza miaka 50 toka nilipozaliwa. Miongoni mwa mambo ninayotaka kufanya ni kufahamu walipo watu ambao kwa namna moja ama nyingine nilikutana nao katika hiyo miaka 50 ya maisha yangu. Tafadhali kama unamjua mmoja wapo ama una taarifa zake nijulishe na kama wewe ni mojawapo basi tafadhali ni-PM. Natanguliza Shukurani.

Leo naomba nianze na orodha wa watu niliosoma nao Chang'ombe shule ya Msingi kati ya mwaka 1970 nilipohamia hapo nikitokea St Anthony Tanga (siku hizi ni Changa Primary School) hadi mwaka 1973 nilipohama kwenda Mfaranyaki Songea.

1. Mr Kirwanda - Mwalimu
2. Mr Nkani - ''
3. Mr Matemu - ''
4. Mr Sindamwaka - Mwalimu Mkuu
5. Mama Baruti - Mwalimu

Wanafunzi Wenzangu:

1. Norman Sabuni - alikuwa na kaka yake anaitwa Noel Sabuni na mdogo wake anaitwa Nina Sabuni. Kaka yao mkubwa alikuwa Raphael Sabuni wakati huo akiimbia STC Jazz na akina Marijani Rajab.

2. Hassan Zawayai
3. Zuberi Zayumba
4. Abraham Mwasongwe
5. Helena Sebastian
6. Gosbert Roderick na dada yake Esther Roderick
7. Georgina Rugimbana na dada yake Rosemary Rugimbana - walikuwa dada wa Jordan Rugimbana ambaye alikuwa nyuma yetu darasa moja na sasa ni mkuu wa Wilaya Kinondoni.

8. Mariam Himid
9. Lucy Mkande
10. Edith Masanja
11. Sarah Kilua
12. John Tesha
13. Rosemary Tesha
14. Mbiliyawaka Hango
15. Mohamed Adam
16. Patrick Rugemalira
17. Richard Kilandeka
18. Suna Said
19. Neema - jina la pili nimesahau lakini mama yake alikuwa
mwalimu hapo hapo Chang'ombe S/Msingi
20. Penina Mhando
21. Shabaani Mohamed na mdogo wake Faraji Mohamed
22. Selina Mkaja
23. Rizwan - Alikuwa muasia akiishi mitaa ya Chang'ombe
Jamatini.

Ongera kaka, na haswa kwa kuwa na kumbukumbu kubwa ya kuwakumbuka wale uliowahi soma nao zaidi ya miaka 35 nyuma.
Wengi wa vijana hivi leo kumbukumbu ya miaka 10 nyuma ni mtihani kwao.

Katika hao school mate wako ninamfahamu mmoja Zuberi Zayumba, huyu jamaa niliwahi fanya naye kazi... Nadhani mdau mmoja amekwisha kukudokeza wapi alipo. Nakumbuka pia huyu jamaa alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kuchangisha fedha kwa ajili ya timu ya taifa, na pia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Executive Sport Marketing (ESM) hapo Dar. Kwa wakazi wa yale maghorofa ya Tabata Sigara watakuwa wanamfahamu, jamaa ni mtu poa sana.

Ongera kwa mara nyingine tena...! Stay strong... Mzee wa pale pa Mfaranyaki!
 
...XPASTER! Shukurani kwa pongezi zako! Shurani zaidi pia kwa taarifa za Zuberi Zayumba. Nafanya Jitihada za Kuwasiliana naye. Hiyo ya 'Mzee wa pale kumfaranyaki'' naomba kuitolea maelezo kidogo!
Pale nilienda kumalizia tu darasa la saba 1974, unajua tena mambo ya kufuatana na madingi wanapohamishwa kikazi! Mi natoka kipande ya kuleee kwa akina mzee Makamba...Ushoto!!! :)
 
Baba Desi nashukuru sana kwa kunikumbusha watu wengine ambao nilikuwa nimewasahau kabisa.
Nilimaliza hapo Chng'ombe Pr 1970 na Mwalimu Nkane alinipiga kibao cha sawasawa nikiwa darasa la 5-kwa kutoimba vizuri.Sikumsahau mwalimu huyu kwa ufedhuli ule na akinikuta Chuo Kikuu akiwa fresher nami nikiwa namaliza degree.
Nasikia amefariki dunia miaka kadhaa iliyopita.
Kirwanda .Sindamwaka , Matemu(Ole wako!!) Mama Baruti were all very good dedicated teachers , mazao yao yapo pote nchini

...Lole, wewe kweli ni original Chang'ombenian! Miaka hiyo uliyomaliza nafikiri utakuwa ulifuatana fuatana na kina Andrew Simkoko na yule dada yake sikumbuki jina lake, akina Anet Kibwasali, kina Peter Makorongo (RTD!) na Tammy na wengineo.
Walimu wa Changombe walikuwa kweli ni very, very dedicated. nakumbuka shule ile ilikuwa inaongoza shule zote za jirani za kibasila, mgulani, wailes na kadhalika.
Nimesikitika sana kuhusu Mr. Nkani! Mwalimu alikuwa anajua kutembeza fito yule si utani!lakini pia alikuwa dedicated kwenye kazi yake.
Mwl Kirwanda alikuwa the Best. Unakumbuka kuwa ndio aliongoza halaiki ya MIaka Kumi ya Uhuru ambayo wengi wanaamini kuwa ndio ilikuwa the best kuliko zote zilizofuata baadaye?
Thank you Mkuu, kwa taarifa yako!
 
Babadesi respect sana fifte si mchezo ati.....miaka hii magonjwa yanakuja sehemu mbaya mbaya....ukimwi,mafua ya nguruwe n.k yaani kukwepa kazi sana.....

...babadesi nina swali nasikia nyie wakongwe zamani mlikuwa na akili sana kushinda hawa serengeti boys.....nini haa lilipelekea muwe na akili zaidi ya serengeti boys?
 
Baba Desi thanks for the compliments.
Andrew Simkoko namkumbuka sana, nasikia sasa yuko Arusha,alikuwa one class behind, dada yake mkubwa,Anna, alisoma darasa moja na dada yangu.
Nitumie ujumbe tuonane wapi, ni vizuri na inampendeza Mungu watu waliosoma shule moja kukutana baada ya miaka mingi.(39 yrs ago)
Mke wangu alisoma hapo hapo Chang'ombe nikikutajia lazima utamfahamu!!
 
baba desi,between georgina and rosemary rugimbana,i dont know which is which one of them is a resident of london vilevile lucy mkande anaishi london
 
Acha vijana wajivinjari, kwani wakikua wataacha na isitoshe JF si ni ya watu wote jamaniiiiiiiiiiiiiii???????????

Other wise Dilunga vipi unamfahamu mtu aitwaye Kambangwa?
 
Acha vijana waenjoy, wakikua c wataacha na watakuwa kama wewe?
Isitoshe Jamii ni ya watu wote

Otherwise vipi Dilunga unamfahamu mtu anayeitwa Kambangwa?
 
Baba Desi

Kwanza Shikamoo na Pili Hongera sana kwa kufikisha 50yrs.Mungu akubariki ili uweze kuishizaidi na zaidi.

Hongera sana Baba Desi
 
Baba Desi heri ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa
.

Nahakika kama wapo humu wataku pm, assuming wanataka ku re-establish contacts with any piece of you!

Lakini sidhani kama hili jamvi lina watu wengi wa demographics yako. Nimegundua wengi aidha si watu wazima au hawa act their age. Ningefurahi sana kama mpo kina Baba Desi wengi mtuletee mitazamo ya angle yenu. Mnahitajika sana, and that's one thing I miss in this baraza. Watu mnaokumbuka foleni za kununua sukari na kadi za mgao wa petroli.

I gotta tell you one thing though. Inahitaji uvumilivu kuwepo hapa watu wa rika lako, na nashukuru uwepo wenu mtu ka wewe na wengine wanao sound matured and responsible, the Rev. Kishoka's of the forum, the Kichuguu's, JokaKuu's, Mwawado's, Jasusi's, QM, Mama's, Mzee Mwanakijiji's, Augustine Mosha's, SteveD, WomenofSubtanc, Blueray, Painkiller, the BubuAK's, Halisi, the Fundi Mchundo's of the jamvi and a handful others, I don't care how old you are, but I read you guys as sooo matured and full of gravitas. And of course, the illustrious FMES types, when he acts his age.

Maana kwa kweli kuna aina ya mandhari fulani humu yanaweza kufukuza watu wazima, and I put the blame squarely on Jakaya Kikwete himself, Invisible that is, maana ana very high tolerance na watu wa mizaha mizaha na mambo ya kitoto humu.

Again, hongera na heri ya siku ya kuzaliwa Baba Desi.

Watu wa umri wa baba Desi tuko kibao,ila tu hali za maisha zinatusambaratisha.Ni kweli ulivyosema humu walio wengi ni wazalendo baada ya Azimio la Arusha ,Kuwapata wapigania uhuru na wanaharakati wa awali ni adimu mno.Kiasi kwamba mijadala mingi inayojitokeza humu ni ile isiyokuwa na chimbuko la kimaadili yenye mitazamo ya upeo mfupi sana.Unajua wengi walifundishwa na waalimu wa UPE na kudanganya kwenye mitihani,Elimu ya hesabu za kikwetu ,Hekaya za Abunuwasi na Hadithi za Esopo,Alfa ulela,Safari za Sindbad nk hawazijui kabisa.
Binafsi nasikia faraja sana kusikia na kuona watu wanakumbukana katika enzi zao.Kwa namna moja au nyingine watu hukutana na kujuana,Pia huachana na kupotezana.Shime wanajamvi tukumbukane tuliko ,tuelezane nini la kufanya ili gurudumu hili la nchi yetu lisogee mbele.Miaka hamsini ni safari ndefu ya maisha japo bado tuendako nako ni mbali.
 
Na sisi vijana ambao tunakaribia 33 yrs tumefanya nini memorable??

1. Alexander, the great, at 33 yrs
Had nearly 90 % of the then known world under his control

2. Julius Caesar, nearly 33 yrs
It is said that another time, when free from business in Spain, after reading some part of the history of Alexander, he sat a great while very thoughtful, an at last burst out into tears. His friends were suprised, and asked him the reason of it. "Do you think," said he, "I have not just cause to weep, when I consider that Alexander at my age had conquered so many nations, and I have all this time done nothing that it memorable?
 
Last edited:
Watu wa umri wa baba Desi tuko kibao,ila tu hali za maisha zinatusambaratisha.Ni kweli ulivyosema humu walio wengi ni wazalendo baada ya Azimio la Arusha ,Kuwapata wapigania uhuru na wanaharakati wa awali ni adimu mno.Kiasi kwamba mijadala mingi inayojitokeza humu ni ile isiyokuwa na chimbuko la kimaadili yenye mitazamo ya upeo mfupi sana.Unajua wengi walifundishwa na waalimu wa UPE na kudanganya kwenye mitihani,Elimu ya hesabu za kikwetu ,Hekaya za Abunuwasi na Hadithi za Esopo,Alfa ulela,Safari za Sindbad nk hawazijui kabisa.
Binafsi nasikia faraja sana kusikia na kuona watu wanakumbukana katika enzi zao.Kwa namna moja au nyingine watu hukutana na kujuana,Pia huachana na kupotezana.Shime wanajamvi tukumbukane tuliko ,tuelezane nini la kufanya ili gurudumu hili la nchi yetu lisogee mbele.Miaka hamsini ni safari ndefu ya maisha japo bado tuendako nako ni mbali.

Mkuu hapo umenena busara zako nimezikubali kwa 101%
 
Baba Desi nashukuru sana kwa kunikumbusha watu wengine ambao nilikuwa nimewasahau kabisa.
Nilimaliza hapo Chng'ombe Pr 1970 na Mwalimu Nkane alinipiga kibao cha sawasawa nikiwa darasa la 5-kwa kutoimba vizuri.Sikumsahau mwalimu huyu kwa ufedhuli ule na akinikuta Chuo Kikuu akiwa fresher nami nikiwa namaliza degree.
Nasikia amefariki dunia miaka kadhaa iliyopita.
Kirwanda .Sindamwaka , Matemu(Ole wako!!) Mama Baruti were all very good dedicated teachers , mazao yao yapo pote nchini

Kunradhi Baba Desi , Mwalimu aliyenipiga kibao miaka hiyo na amefariki several years ago ni Mwl Nsibu(sio Mwl Nkane).My apologies and sorry for any inconveniences not intended.
Hata hivyo nimekumbuka waalimu kadhaa:
Mr Ntanga
Mrs Mwanza
Mrs Kahemele
Mrs Mwansasu
na wa zamani zaidi(asians)
Miss Figuiredo(later Mrs Fernandes)
Miss Killochia
Mrs Walji

na wazungu
Mr Brown
Mr Dalton mwalimu wa Dini
Miaka mingi imepita hapo naongelea 1964-68 sijui kwa sasa hivi wako wapi,
Mwenye habari tafadhali.
 
Babadesi respect sana fifte si mchezo ati.....miaka hii magonjwa yanakuja sehemu mbaya mbaya....ukimwi,mafua ya nguruwe n.k yaani kukwepa kazi sana.....

...babadesi nina swali nasikia nyie wakongwe zamani mlikuwa na akili sana kushinda hawa serengeti boys.....nini haa lilipelekea muwe na akili zaidi ya serengeti boys?

Yo Yo, Thanx! Pongezi zako zimefika nashukuru. Kuhusu hilo swali lako, kuna Mkuu mwenzangu ameishalijibu hapo. KITABU!! Unajua zamani starehe pekee ya wanafunzi ilikuwa ni Kusoma Vitabu na Michezo, basi! Mzee mwenzangu ameishasema hapo kuwa siku hizi ukiwatajia watoto wetu vitabu kama 'Mashimo ya mfalme Suleiman', 'Hadithi ya Allan Quaterman', 'Visa vya Ajabu', 'Mashujaa', Hadithi za Alfu Lela Ulela' hii ni mbali na vitabu vya masomo, achilia mbali pia mzee wetu Shabaan Robert ambaye kwake nimeazima kichwa cha habari cha thread hii. Kuna mambo mengi yanapoteza concetration ya watoto wetu siku hizi...!
 
Last edited:
Back
Top Bottom