Mahakama ya Afrika ya Haki za Binaadamu yapinga Adhabu ya Kifo kuendelea kutolewa Tanzania

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Kwa mara nyingine Tena, Mahakama ya Africa ya Haki za Binaadamu (African Union Court of Human and People's Rights) imetoa tamko juu ya adhabu ya kifo iliyopo kwenye sheria za makosa ya jinai ya Tanzania. Tamko hili limetolewa June 2023 wakati wakifanya mapitio ya kesi ya Bwana Thomas Mwingira dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kesi ambayo Bwana Mwingira aliiwasilisha mahakama ya Afrika akilalamikia kutotendewa haki.

Katika kufikia maamuzi yake, Mahakama hii ilisisitiza kuwa Tanzania inavunja haki za binaadamu Kwa kuendelea kutoa hukumu ya kifo Kwa makosa ya mauaji.

Itakumbukwa kuwa, japokuwa adhabu ya kifo imeendelea kutolewa, mara ya mwisho adhabu hii ilitimizwa mwaka 1995. Marais, akiwemo Hayati Dr. Pombe John Magufuli ambaye alisema bayana kubwa hatasaini Hati ya kunyonga wafungwa, wamekuwa wakikwepa kusaini hati hizo. Jambo hili linapelekea wahukumiwa wa adhabu ya kifo magerezani kubaki bila kujua hatima yao.

Ikumbukwe pia, hii si mara ya kwanza Kwa Mahakama hii ya Afrika kuisihi Tanzania kufuta adhabu ya kifo kama zilivyofanya nchi nyingine za jumuiya ya madola. Mwaka 2019, 2021 na 2022 Mahakama hii ilitoa msisitizo wakati ikitoa hukumu ya kesi tofauti kutokea Tanzania zinazohusisha adhabu ya kifo.
 
Sidhani kama wanaua! By the way so hao wanaoua mbona wenyewe hawaangalii haki za binadamu...? Kutetea upumbavu tu
 
Hio Mahakama haina meno.., ila Binafsi nasema Kifo kingekuwa hukumu watu wangejiua ?!! Huenda kifo sio Adhabu....

Kwa mara nyingine Tena, Mahakama ya Africa ya Haki za Binaadamu (African Union Court of Human and People's Rights) imetoa tamko juu ya adhabu ya kifo iliyopo kwenye sheria za makosa ya jinai ya Tanzania. Tamko hili limetolewa June 2023 wakati wakifanya mapitio ya kesi ya Bwana Thomas Mwingira dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kesi ambayo Bwana Mwingira aliiwasilisha mahakama ya Afrika akilalamikia kutotendewa haki.

Katika kufikia maamuzi yake, Mahakama hii ilisisitiza kuwa Tanzania inavunja haki za binaadamu Kwa kuendelea kutoa hukumu ya kifo Kwa makosa ya mauaji.

Itakumbukwa kuwa, japokuwa adhabu ya kifo imeendelea kutolewa, mara ya mwisho adhabu hii ilitimizwa mwaka 1995. Marais, akiwemo Hayati Dr. Pombe John Magufuli ambaye alisema bayana kubwa hatasaini Hati ya kunyonga wafungwa, wamekuwa wakikwepa kusaini hati hizo. Jambo hili linapelekea wahukumiwa wa adhabu ya kifo magerezani kubaki bila kujua hatima yao.

Ikumbukwe pia, hii si mara ya kwanza Kwa Mahakama hii ya Afrika kuisihi Tanzania kufuta adhabu ya kifo kama zilivyofanya nchi nyingine za jumuiya ya madola. Mwaka 2019, 2021 na 2022 Mahakama hii ilitoa msisitizo wakati ikitoa hukumu ya kesi tofauti kutokea Tanzania zinazohusisha adhabu ya kifo.
Tupia nakala ya hukumu
 
Kimsingi adhabu ya kifo siyo Sawa kwa sababu tunaamini mtu katenda dhambi kwa sababu shetani kamwingia .sasa shetani mwenyewe hajahukumiwa kifo Cha jehanamu sasa huyu mwanadamu si unakuwa umemwonea kwenda jehanamu wakati aliyemtuma kufanya kosa hajahukumiwa? Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom