Magufuli alipofariki dunia tu, Samia akachukua Urais. Ndugai alipoanguka tu, Tulia akawa Spika. Wanawake wa CCM wamejipanga!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,357
35,832
Linapokuja suala la mali au madaraka huenda kundi la wanawake ndio kinara wa kuvuna kirahisi sana, iwe kwa haki au kwa hila, wanawake ni wavunaji tu.

Wakati watawala wa CCM walipokuwa wanawapanga wanawake kwenye safu mbalimbali za uongozi kama alama ya ujanja ujanja ya kuwatumia ili kuimarisha mamlaka ya wanaume, sasa ngoma imegeuka vibaya, leo wanaume wa CCM wamebakia kulialia tu baada ya wanawake kuwafyatua vibaya, tena kwa aibu kubwa.

Ilianza kwa Magufuli, alipokufa tu, wanaume wa CCM wakajikuta wanatamani serikali ya mpito (ambayo haikuwa inakubalika kikatiba) ili Samia Suluhu asiwe rais! Lakini ngoma ikagonga mwamba.

Mikakati mbalimbali mizito ya wanawake ndani ya CCM ikapangwa kuhakikisha Ndugai inatoka kwenye kiti, pasipo kujua akaingia mkenge, akapigwa ngwala na kutupwa mbali, leo hii ni hadithi tu sasa mwanamke anayejulikana kama Tulia anakwenda kukalia kiti cha Spika.

Kwa kuwa madaraka huwa ni matamu, na wanawake wa CCM hawanaga mishipa ya aibu au kutosheka, kituo kinachofuata ni kuhakikisha wenyeviti wa kamati za kudumu za bunge wengi wanakuwa wanawake kama inavyoelekea sasa kwenye baraza la mawaziri.

Yote kwa yote, huenda kituo kinachofuata ni nafasi ya waziri mkuu, Majaliwa ajipange, wenye CCM yao (wanawake!?) wameshafika.
 
Kama magufuri aliuawa wazi kabisa lakini hata hakuna anayemtetea na hakuna anayejali hata watoto wake kuwapa hata UDC, usidhani kama samia hajajipanga na wanawake wenzake. Kwanza haya kura za wanaume hawazitaki tena
 
Kama magufuri aliuawa wazi kabisa lakini hata hakuna anayemtetea na hakuna anayejali hata watoto wake kuwapa hata UDC,,usidhani kama samia hajajipanga na wanawake wenzake..Kwanza haya kura za wanaume hawazitaki tena
Kumbe vyeo mnapeana tu so long as ni mtoto wa mwenzenu!! Ndiyo maana hii nchi haiendelei
 
Yule chizi aliyekuwa mkuu wa mkoa wa mbeya ameshtuka, anasema kwa katiba hii makamu wa raisi alimroga Raisi akafa, huenda na naibu alimroga spika, akajiuzuru,

Katiba mpya izuie makamu na naibu kuchukua nafasi za maboss wao wanapokufa au kujiuzulu
 
Post ya kipumbavu kabisa hii. Yaani hakuna hoja wala tija. Haya nyanyukeni wajinga MaCHADEMA wanaume mpambane na wanawake wa CCM. Katafute urojo u kalale tena.
Haya machadema yanatoa hoja dhaifu na za kipumbavu kama ya mtoa post haafu yanajiita akili kubwa!
 
😅😅😅 Miaka yote CCM huwatumia sana wamama kama ngome yao kuu, ... wakubali tu matokeo maana HAMNA NAMNA!
1642825051812.png
 
Ajenda yako ni WANAWAKE tuu...wewe aliye kuzaa ni mwanamke na ameitunza familia yenu vizuri sasa kuna ubaya gani mwanamke huyo huyo akiitunza nchi?

Miaka nenda rudi wanaume wameongoza wala hakukuwa na nongwa tuache na wanawake waongoze.
 
Ni kama unaongea kuwa makaimu wanafuata kwenye kila position endapo head ataondoka

Sasa siasa za makaimu ni mbaya sana tutashindwa hata kunywa maji kwenye vikao

Kunae shida mahali
 
Ajenda yako ni WANAWAKE tuu...wewe aliye kuzaa ni mwanamke na ameitunza familia yenu vizuri sasa kuna ubaya gani mwanamke huyo huyo akiitunza nchi?

Miaka nenda rudi wanaume wameongoza wala hakukuwa na nongwa tuache na wanawake waongoze.
Safari hii tumefanikiwa KUONA sura halisi za wanaume,
 
Bawacha ni chama dume kivipi?

Labda ACT wazalendo!
Chadema ni chama Dume wewe! Kwanza kinaongozwa na Makamanda. Hilo lazima utambue. Na utambue pia Kamanda wa kike wa chadema ni nusu mwanume! Yaani ni kazi kazi! Huwezi kumuona akicheza taarab, akipiga umbea, akichamba, au kukuna nazi.

Sasa ukija ccm, mambo ni tofauti kabisa. "Nimekosa mimi, nimekosa sana! Naomba nisamehewe! " Pumbavu! Hao ACT Wazalendo, nadhani nitapoteza tu muda wangu kuwajadili.
 
Linapokuja suala la mali au madaraka huenda kundi la wanawake ndio kinara wa kuvuna kirahisi sana, iwe kwa haki au kwa hila, wanawake ni wavunaji tu.

Wakati watawala wa CCM walipokuwa wanawapanga wanawake kwenye safu mbalimbali za uongozi kama alama ya ujanja ujanja ya kuwatumia ili kuimarisha mamlaka ya wanaume, sasa ngoma imegeuka vibaya, leo wanaume wa CCM wamebakia kulialia tu baada ya wanawake kuwafyatua vibaya, tena kwa aibu kubwa.

Ilianza kwa Magufuli, alipokufa tu, wanaume wa CCM wakajikuta wanatamani serikali ya mpito (ambayo haikuwa inakubalika kikatiba) ili Samia Suluhu asiwe rais! Lakini ngoma ikagonga mwamba.

Mikakati mbalimbali mizito ya wanawake ndani ya CCM ikapangwa kuhakikisha Ndugai inatoka kwenye kiti, pasipo kujua akaingia mkenge, akapigwa ngwala na kutupwa mbali, leo hii ni hadithi tu sasa mwanamke anayejulikana kama Tulia anakwenda kukalia kiti cha Spika.

Kwa kuwa madaraka huwa ni matamu, na wanawake wa CCM hawanaga mishipa ya aibu au kutosheka, kituo kinachofuata ni kuhakikisha wenyeviti wa kamati za kudumu za bunge wengi wanakuwa wanawake kama inavyoelekea sasa kwenye baraza la mawaziri.

Yote kwa yote, huenda kituo kinachofuata ni nafasi ya waziri mkuu, Majaliwa ajipange, wenye CCM yao (wanawake!?) wameshafika.
Kwenye Sakata la Ndugai Tulia alijikausha utadhani yeye alikuwa kwnye Mhimili wa Jeshi
 
Chadema ni chama Dume wewe! Kwanza kinaongozwa na Makamanda. Hilo lazima utambue. Na utambue pia Kamanda wa kike wa chadema ni nusu mwanume! Yaani ni kazi kazi! Huwezi kumuona akicheza taarab, akipiga umbea, akichamba, au kukuna nazi.

Sasa ukija ccm, mambo ni tofauti kabisa. "Nimekosa mimi, nimekosa sana! Naomba nisamehewe! " Pumbavu! Hao ACT Wazalendo, nadhani nitapoteza tu muda wangu kuwajadili.
Ni kweli kamanda Halima Mdee ni kidume na nusu!
 
Back
Top Bottom