Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,304
- Thread starter
- #81
Hongera mkuu
Sekyu kaka
Hongera mkuu
Kimokole umesibu, umenena ya uhakika
Tena umenistaajabu, kunijibu kwa haraka
Wajibu tena faradhi, malenga kukusanyika
Jamvini bila tabu, wote tukafarijika.
si kwamba namchukia, Wiselady mtani,
ila yamenizidia, yake makeke kundini,
fujo azipalilia, ili apate kuwini,
tunatamani kulia, tumtiapo machoni,
yeye anafurahia, tuingiapo shidani,
nina shaka si raia, bali yeye ni mgeni,
akiona unalia, yeye kwake burudani,
apenda kuzidishia, shida iliyo moyoni,
hapendi kufarijia, wiselady mtani.
Wala sikufanya haraka, ni wepesi wa kuandika,
Nilishikwa na wahaka, Kimo jina umeliweka,
Furaha ikanishika, hima Keyboard kuchapa.
Nimefurahi hakika, Kimokole betini nawika
mmmhh haya ngoja kichwa kinanizunguka sasa
sasa sijui ni ajili ya hii thread au mambo ya saturday night
mmmmhhhhh..
samahani sana mkuu , itabidi nirudi hapa asubuhi
na macho yang manne ni some tena
hahahah lol:coffee:
si kwamba namchukia, Wiselady mtani,
ila yamenizidia, yake makeke kundini,
fujo azipalilia, ili apate kuwini,
tunatamani kulia, tumtiapo machoni,
yeye anafurahia, tuingiapo shidani,
nina shaka si raia, bali yeye ni mgeni,
akiona unalia, yeye kwake burudani,
apenda kuzidishia, shida iliyo moyoni,
hapendi kufarijia, wiselady mtani.
Mohammed Shossi nisaidie kupambana na huyu PJ ananionea sana na mm umalenga siuwezi, pls do it for me
Kazi unayonituma, sina budi ujira kupatana Utaweza kubali, matai tusije kamatana Nataka nyama ilonona tena mwanana Sitakiutumbo japo wachanga wanapikia banana Walasitaki yakidadi kwenye meno yashikana Wala sitaki ya mbuzi hata iwe kilo nane Nataka paja la swala alienona mwanana Wiselady nauliza je wajua kuwinda?
Dah! PJ nipe break kidogo,,,
furaha yangu,huwa ni furaha yenu
huzuni yenu,huwa ni huzuni yangu
mnitiapo machoni,huwa mnafarijika
hata kama mlikuwa mna njaa,huwa mnashiba
kama mlikuwa na huzuni,huwa mnafarijika
japo mie siko ktk list ya unaowafeel lkn nisipokupa hongera nitakuwa mchoyo,
hongereni na wanamalenga wote,inafurahisha sana kuona jinsi mnavyoinyambua lughakupitia hizi tungo/tenzi.
ewe cheusi mangala, salamu nakutmia,japo mie siko ktk list ya unaowafeel lkn nisipokupa hongera nitakuwa mchoyo,
hongereni na wanamalenga wote,inafurahisha sana kuona jinsi mnavyoinyambua lughakupitia hizi tungo/tenzi.