Magreat Thinkers ninaowafeel...........

Bora iweke moyoni , hiyo siri mwana flani
Siri ibaki sirini, siyo tena hadharani
Hapo utaweza wini, ewe mtunzi makini

Nimetoa changamoto, naomba nguvu tilia,
Mambo yawe motomoto, na sote kujisikia
WomanOfSubstance umeuanza mpito............
 
Wow yaani hata mwezi bado humu umewajua wote hawa??? Au ulikuwa unatumia jina lingine humu before???

Nice one kama mwezi bado na unashinda humu
 
Shairi lako halijakamilika japo nimekupa thanks

Yo Yo Kwangu piga hodi, kunitaka ushauri
Nami nyuma sitarudi, nikatongowa mazuri
Yo Yo sasa huna budi, iogelee bahari
Njoo imara shadidi, kwa mdomo wa hariri
 
Wiselady m'baya, ninasema hadharani,
Hatufai kwenye kaya, amekosa shukurani
Ameikosa hidaya, si mtu mwenye ubani

Na ukuu wa wilaya, haupati asilani
Atabaki anagwaya, hata aende shambani,
Hata aende Ulaya, atakuwa kisirani

Kabila yangu Mhaya, Bukoba napatamani,
Akipenda kuwa yaya, simpeleki nyumbani,
Atakuja sota waya, atoe jasho kwapani,

kukujibu kwa ushairi siwezi ila mohamed kashakujibu on behalf,,ukiendelea jela miezi 6,,,au unanisifia kwa mafumbo nini!!
 
Mbona wanitisha, ewe uloleta tungo
Nabaki ninalo shaka, kama nisomacho ndicho
Naweza hata kubisha, labda uje thibitisho

Kofia nakuvulia, na koja ninakuvika
Vibua waviachia, dagaa mwiko kushika
Simvuvi sinzia, ndio maana unawika.
Thibitisho atoa Wengine wamo kulia, mbinu unazotumia
Waloweze kuwambia, nyayo zako kufatia.
 
We mshairi wa ukweli. Kweli kiswahili lugha yako. Ila naomba kama ulikuwa na maana ya rais wangu dr.Slaa naomba urejee ID yake vizuri,kama una member mwingne poa ,ila kwa rais wangu dr. Slaa iyo si ID yake. Mwisho nakupongeza kwa kipaji cha utunzi.
 
Nimeiona kwenye members waliokuwa online hiyo ID mkuu na shukran sana kwa hongera zako nami nasema

Gsana Naingia jamvini, hapana tena ajizi
Nazikubali shukrani, kwa juhudi zangu hizi
Kushajiisha jamvini, watunzi wa zama hizi
Kheri ipo kwa manani, Mpaji katujaalia.

Hii beti itakuwa included/inserted kwenye thread as well.
 
Senksi yangu ya via mobile kama siioni vile!!Asante MS...me like you too!Ngoja na mimi nijipange kuangusha kitu!
 
Wow yaani hata mwezi bado humu umewajua wote hawa??? Au ulikuwa unatumia jina lingine humu before???

Nice one kama mwezi bado na unashinda humu

Mbongopopo
Chunga heshima na cheo, na maovu usifikwe
Fidhuli umjuapo, usimtoze neno lake,
Takuudhi na wenzio, ushikapo pasishikwe
Umjuaye kunyakwe, simnyishe penye watu....
 
Senksi yangu ya via mobile kama siioni vile!!Asante MS...me like you too!Ngoja na mimi nijipange kuangusha kitu!

Senks yako haifjafika labda ipo niani lol. Kumbe ndio maana viewers wengi wanaochangia wachache kumbe mnaenda kujipanga!
 
M.Shossi nakupa mia, kwa tungo zako murua,
yaonekana umekamia, malenga wakongwe kuwabidua,
Kimokole natazamia, shairi lijalo kuingia,
Screen naitumbulia, mimacho kodokodo nimeitoa
 
M.Shossi nakupa mia, kwa tungo zako murua,
yaonekana umekamia, malenga wakongwe kuwabidua,
Kimokole natazamia, shairi lijalo kuingia,
Screen naitumbulia, mimacho kodokodo nimeitoa

Kimokole moyoni nafarijika, malenga tukikutanika,
Ya haki kuyatamka, batili kuzifunika,
Kheri ikaminika jamvini tukanufaika.
Bwana Kimokole, nakushukuru hakika
 
Kimokole moyoni nafarijika, malenga tukikutanika,
Ya haki kuyatamka, batili kuzifunika,
Kheri ikaminika jamvini tukanufaika.
Bwana Kimokole, nakushukuru hakika

Malenga mkijuana, furaha yashika hatamu,
Tutafunika kila kona, JF wasiishe hamu,
Ingawa maisha yabana, JK kutuhujumu,
Tutakomaa kinamna, hadi haki ishike hatamu.
 
Malenga mkijuana, furaha yashika hatamu,
Tutafunika kila kona, JF wasiishe hamu,
Ingawa maisha yabana, JK kutuhujumu,
Tutakomaa kinamna, hadi haki ishike hatamu.

Kimokole umesibu, umenena ya uhakika
Tena umenistaajabu, kunijibu kwa haraka
Wajibu tena faradhi, malenga kukusanyika
Jamvini bila tabu, wote tukafarijika.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom