Kwako Mpendwa wetu Unique Flower

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,527
14,403
Habari yako Miss Unique Flower , nikiwa kama moja ya Wanachama wa JamiiForums nachukua nafasi kukupa ushauri huu hapa jamvini. Soma huu Uzi mara nyingi uwezavyo ili kuleta mabadiriko ya afya ya Akili yako.

NB: Wewe ni Mtu wa thamani sana acha kuwababaikia Wanaume , anayekupenda kweli atakufuta Mwenyewe lakini ukiwa unawashobokea watakutumia na kuzidi kukuvuruga akili yako na utajiona haufai.

Sisi sote tunapitia msongo wa mawazo kwa njia tofauti. Mara nyingi, tunaweza kushindwa kujua kuwa tunachopitia ni msongo wa mawazo. Ikiwa unapata mabadiliko haya, kuna uwezekano kuwa unakabiliwa na msongo wa mawazo.

1• Kupoteza hamu na tamaa ya kufanya yale mambo uliyokuwa furahia hapo mwanzo

2• Kuhisi kukata tamaa na kukosa tumaini

3• Kujihisi vibaya kujihusu Mwenyewe, au kuhisi kuwa umefeli maisha na kujiona hauna thamani.

4• Kujihisi mvivu au kuhisi kutotulia, kubabaika (Unakosa utulivu kwa Kila jambo ufanyalo)

5• Unawaza kwamba ni bora kufa au kujiumiza kwa njia yoyote ili upate faraja kutoka kwa watu wengine.


Je, unawezaje kudhibiti hisia za msongo wa mawazo?

Fanya haya ili kudhibiti Msongo wa mawazo

1. Mazoezi
Shughuli kama vile kukimbia, kucheza mpira wa miguu, kutembea, ni moja ya mambo yanayo saidia kuinua mhemko wako na kukusaidia kulala vizuri.

Kufanya mazoezi
mara kwa mara pia hukusaidia kusahau wasiwasi na shida zako na husaidia kusahau
mawazo ambayo yanasababisha msongo wa mawazo.


2. Kulala
Kulala hupunguza msongo wa mawazo sana. Kuwa na utaratibu wa kulala
husaidia kukutuliza, inaboresha hali yako na inakusaidia kufanya maamuzi bora.
Wataalamu wanapendekeza kulala kwa angalau masaa 8 kila usiku.

Jaribu kupata mpangilio bora wa kulala kwa kufanya mazoezi, kupunguza unywaji wa
pombe au kafeini (chai / kahawa) wakati wa kulala unapokaribia.


3. Lishe Bora
Ingawa chakula hakiwezi kuondoa hisia za kuchanganyikiwa na msongo wa mawazo kabisa, lishe bora inaweza kuongeza mhemko wako, kupunguza shida za kuwa na shinikizo la damu, na kujenga kinga yako ya mwili. Kuna vyakula ambavyo vinaweza kupa utulivu wa msongo ikiwa unazijumuisha kwenye lishe yako ya kila siku. Hii ni pamoja na vyakula vyenye:


• Vitamini C na madini - matunda na mboga
• Protini kama mayai, nyama, na maharagwe.
• Vyakula vinavyotoa nishati kama mahindi, ngano na viazi vitamu.


4. Panga kazi yako na uorodheshe majukumu yako

Panga kazi zako za kila siku ukianza na kazi za haraka. Mwishoni mwa siku, zingatia majukumu ambayo umeweza kuyafanya. Hii itakusaidia kukumbana na hisia za kuzidiwa na shughuli zako za kila siku.

5. Wakati
Usibebwe sana na kasi ya maisha. Chukua muda kupumzika ili ufurahi na ufanye kitu unachofurahia kila siku. Hii haitaongeza burudani zako tu, lakini pia itakupa kitu cha kukupatia tumaini la baadae.


6. Zungumza na watu unaowaamini
Kuzungumza na kuwaambia watu wa karibu nawe shida zako kunaweza kusaidia kupunguza viwango vyako vya msongo wa mawazo, huku kujumuika na familia na marafiki wanaweza kukusaidia kuwa mtulivu na kupunguza msongo wa mawazo. Ni vizuri kuzungumza na wengine kwani watu wanaweza kukusaidia kupata suluhisho la kile kinachokusumbua. Kumbuka, kuna watu ambao wanaweza kuwa wamepitia hali kama wewe. Hata hivyo, ikiwa haufikiri kuzungumza, unaweza kuandika hisia zako.


7. Epuka njia mbaya za kukabiliana na msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo kunaweza kusababisha kuongezeka kwa kishawishi cha kutumia madawa ya kulevya kama vile pombe, sigara, na vitu vingine. Ingawa dawa hizi zinaweza kusaidia kwa muda lakini husababisha hatari kubwa kiafya.

Matumizi mabaya ya dawa za kulevya pia husababisha ulevi, kuongezeka kwa viwango vya msongo wa mawazo na athari mbaya za kitabia na kijamii.

Jihadhari na tabia zingine mbaya za kukabiliana na msongo wa mawazo kama vile kula sana na mazoea hatari ya uhusiano kama tabia hatari za kingono ambayo ni hatari kwa afya yako.

#Nikutakie Ijumaa Kariim
 
Salama Mkuu?
Kinachomsumbua huyu ni Vijana tu wale wanao hit na ku run. Wanamuachia maumivu ya akili na kujiona duo kitu nimemshauri hapo juu.
Am not trying to be nasty, ila uhalisia ni kwamba zipo factors nyingi zinazosababisha mtu abaki kwenye mahusiano lakini huruma sio moja wapo. Hivyo asitegemee huruma, badala yake awe mpole, aliyewake atamfata popote alipo.

Binafsi siamini kama wanaomchanganya wapo humu JF, ila nahisi anaitumia kama platform ya kutolea aliyonayo moyoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom