DOUBLE AGENT
Member
- Jul 3, 2011
- 38
- 34
Ifuatayo ni orodha ya magazeti ya Tanzania ambayo wamiliki wake au wahariri wake au wote wamiliki na wahariri wamekuwa wakitumika kumsafisha Edward Lowassa katika mradi wake wa kutaka kwenda Ikulu 2015 kwa gharama yoyote ile. Magazeti haya yalitumiwa sana kupotosha umma kuhusu matokeo ya vikao vya NEC na Kamati Kuu ya CCM Dodoma juzi na kutoa habari na picha za kumpamba Lowassa kila mara akitumia viongozi wa dini njaa kujisafisha:
1. Mtanzania na RAI
Ingawaje hayasomwi tena na Watanzania makini, magazeti haya yanamilikiwa na Rostam Aziz, kingmaker wa viongozi mafisadi Tanzania na chief financier wa Lowassa.
2. MwanaHalisi
Gazeti linalomilikiwa na Saeed Kubenea ambaye sasa amefika bei kwa mafisadi na anawatumikia kama kibarua wao kuwasafisha na kuwatukana maadui wao, hususan Waziri Samuel Sitta.
4. Tanzania Daima
Gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ambalo mhariri wake mkuu, Absalam Kibanda, yuko kwenye payroll ya Lowassa na Rostam kwa miaka mingi sana
5. Jamhuri (soon-to-be launched)
Gazeti la Lowassa ambalo litazinduka hivi karibuni, wahariri wake wakiwa ni vijana wa Lowassa wa siku nyingi -- Deodatus Balile na Manyerere Jackton -- ambao amewaazima kutoka kwenye magazeti ya rafiki yake Rostam. Hii ni baada ya jarida la Lowassa la Umoja linaloendeshwa na Absalom Kibanda wa Tanzania Daima kufeli na mpaka kufikia hatua ya kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake.
6. Mwananchi
Kuna "mdudu" ameingia hivi karibuni kwenye gazeti pendwa la kila siku la Tanzania ambalo na gazeti hili nalo sasa linatumiwa kwenye mradi wa kumsafisha Lowassa. Hii ilijidhihirisha kwenye mkutanon wa juzi wa NEC ambapo habari kuu iliyotoka kwenye kikao cha NEC iliandikwa na mtu mmoja na kuchapishwa kwenye magazeti matatu -- Mwananchi, Tanzania Daima na Mtanzania -- neno kwa neno.
7. Daily News
Kaimu Mhariri Mkuu wa Daily News, Mkumbwa Ally, amejisalimisha kambi ya Lowassa ili athibitishwe na kupewa cheo kama Mhariri Mkuu wa magazeti ya serikali, TSN. Wakati huo huo, gazeti la Habari Leo lililo chini ya TSN limekuwa likipambana kuleta habari za ukweli kuhusu mafisadi. Hii imesababisha habari za Daily News na Habari Leo kuhusu kujivua gamba kutofautiana kabisa wakati yote ni magazeti ya serikali chini ya kampuni moja.

- Mpaka hivi sasa, genge la kina Lowassa limejaribu na kushindwa kufanikiwa kwenye kila jitihada za kuyaingia au kuyamaliza kabisa magazeti mawili pekee yaliyosimama kidete kuueleza umma wa Tanzania ukweli. Nayo ni RAIA MWEMA na DIRA.