Magazeti yanayomsafisha Lowassa haya hapa!

Jamani Mwl Nyerere alipokuwa akimpigia Mkapa campaign kuwa ni MR CLEAN si sote tulikubali na kumpa kura? Katoka akiwa MR DIRTY sio? ndio maana watu wanasema ni Fisadi.
Sasa acheni MR DIRTY ambaye sasa anajulikana kama fisadi wa Richmond maana mimi sijasikia tuhuma nyingine, pia Mwl Nyerere alimkataa aingie madarakani atatoka wote tukisema MR CLEAN. Mchawi mpe mtoto akulelee.
 
Jamani Mwl Nyerere alipokuwa akimpigia Mkapa campaign kuwa ni MR CLEAN si sote tulikubali na kumpa kura? Katoka akiwa MR DIRTY sio? ndio maana watu wanasema ni Fisadi.
Sasa acheni MR DIRTY ambaye sasa anajulikana kama fisadi wa Richmond maana mimi sijasikia tuhuma nyingine, pia Mwl Nyerere alimkataa aingie madarakani atatoka wote tukisema MR CLEAN. Mchawi mpe mtoto akulelee.

Ndugu Mtanzania, zinduka! Kwa nini Lowassa ang'ang'anie kuongoza taifa la Julius Nyerere, wakati sote tunajua ni fisadi? Je, tumerogwa?! Mbona viongozi wengine waadilifu na wachapa kazi wapo wengi tu! Tusiwe majuha....

Kwa faida yako na wengine ambao hawajaona au hawataki kuona, baadhi ya tuhuma za ufisadi dhidi ya Lowassa ukiacha Richmond ni kama zifuatazo, kama ambavyo mwana JF mmoja kaziweka kwenye thread hii:

Ufisadi wa Lowassa huu hapa:

1. Kununua jumba la kifahari London, Uingereza, lenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 1 za Tanzania

Metropolitan police wa Uingereza wanachunguza suala hili. Wamewasiliana na anti-money laundering unit ya Tanzania kuchunguza suala hili.

2. Ufisadi wa Nyumba ya Sanaa

Lowassa ni mhusika mkuu wa kufanya uporaji wa ardhi ya Nyumba ya Sanaa iliyopo karibu na Serena Hotel (zamani Movenpik Hotel). Nyaraka zinaonesha yeye ni mmiliki wa kampuni inayojenga gorofa kubwa kwenye eneo hilo la Nyumba ya Sanaa.

3. Utajiri usioelezeka (unexplained wealth)


Akiwa kama kiongozi wa umma, Lowassa amejilimbikizia mali nyingi sana za thamani ya mabilioni ya shilingi. Mali alizo nazo haziendani na kipato chake kama kiongozi wa umma. Sheria ya kupambana na rushwa Tanzania iko wazi kuwa kiongozi wowote wa umma mwenye utajiri usioendana na mapato yake halali anastahili kufikishwa mahakamani. Kutokana na sera za kulindana na kuogopana, Lowassa, Andrew Chenge, na viongozi wengine wa umma hawajafikishwa mahakamani kwa kosa hili na PCCB. Pia kwenye fomu za kila mwaka za kutaja mali, Lowassa haja declare assets zake zote. Ana miliki Alphatel, Alpha Schools, Alpha House, apartment blocks Dar es Salaam, Arusha na nje ya nchi.

4. Land grabbing

Alipokuwa Waziri wa Ardhi enzi za utawala wa Mwinyi alihusika na uporaji mkubwa wa ardhi sehemu mbali mbali nchini.

5. Richmond

Lowassa ndiye aliyeagiza TANESCO waporwe madaraka ya kusimamia tenda ya umeme kinyume na sheria ya manunuzi, PPRA. Aliunda kamati ya makatibu wakuu na kusimamia kwa karibu majadiliano ya kamati hii na nRichmond na kuagiza wapewe tenda wakati Tanesco waliikataa Richmond kuwa haifai. Lowassa ndiye mhusika mkuu wa kashfa ya ufisadi ya Richmond ndio maana alilazimika kujiuzulu.


6. Need I say more?

Lowassa ni mchafu wa maadili. Anapenda sana mali, amejilimbikizia utajiri kuliko kipato chake halisi. Wafuasi wake wanamfanananisha na Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Tofauti ya Zuma na Lowassa ni kuwa Zuma alifikishwa mahakamani na kusafishwa na mahakama. Lowassa apelekwe kortini kujibu shutuma za ufisadi, akishinda kesi ndio atakuwa amesafishwa kweli. Si kwa kutumia vyombo vya habari na waandishi wa habari wenye njaa.
 
Back
Top Bottom