Waziri Nape aruhusu magazeti kuendelea kusomwa kwa mbwembwe. Mpaka matamko yanakinzana huwa hakuna mawasiliano ndani ya wizara?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Nimeona mjadala wa “Kusoma magazeti”. Nimeelekeza TCRA kuruhusu UBUNIFU kwenye tasnia ya Habari. Staili ya usomaji we magazeti imeongeza MVUTO kwenye usomaji huo, ni jambo linapaswa KUTIWA MOYO badala ya kuzuiwa. Waandishi endeleeni na ubunifu kwenye kusoma magazeti.

Maelekezo mengine yeyote ambayo TCRA inatoa kwenye sekta ya habari yanapaswa kuwa WEZESHI na sio ZUIZI. Ni muhimu TCRA ijenge utamaduni wa kuzungumza kabla ya kuagiza.

Amendika Nape kwemye ukurasa wake wa X.

****
Mpaka matamko yanatoka na kukinzana hivi, ina maana huwa hawawasiliani kabla hawajatoa matamko? Wizara hazina mawasiliano mpaka wanakuja kutiana aibu hivi?

Au ni maigizo kuonesha wanafanyakazi na kweli wapo upande wa wananchi. Yaani wanatengeneza tatizo halafu wanakuja kulitatua. 🤔

Kwenu Wakuu.
 
"Nimeona mjadala wa “kusoma magazeti." Nimeelekeza TCRA kuruhusu ubunifu kwenye tasnia ya habari. Staili ya usomaji wa magazeti imeongeza mvuto kwenye usomaji huo, ni jambo linapaswa kutiwa moyo badala ya kuzuiwa. Waandishi endeleeni na ubunifu kwenye kusoma magazeti.

Maelekezo mengine yoyote ambayo TCRA inatoa kwenye sekta ya habari yanapaswa kuwa wezeshi na sio zuizi. Ni muhimu TCRA ijenge utamaduni wa kuzungumza kabla ya kuagiza." - Waziri wa Habari, Nape Nnauye

Source: Swahili Times
 
Vitu vingine bhana

Igeni Sky news

Lowasa: Ukosefu wa Ajira ni bomu linalosubiri kuripuka

Mtu anaajiriwa clouds kutusomea magazeti ambayo Yako mitandaoni 😂😂😂
 
Tengeneza tatizo likileta tafrani unalitatua fasta ili ujipatie political mileage.

Hiyo style yao tunaijua.
 
Kusoma kwa mbwembwe kuna nyongeza ya maneno yenye ukakasi? TCRA bila shaka waliropoka tu ionyeshe wanawajibika
 
Yule ofisa wao alikurupuka, akala za uso ikabidi aende kwenye media kudai alinukuliwa vibaya, amepotoshwa. Mbwembwe ndio constractive kwa usomaji wa taarifa mbalimbali kulingana na mukhtadha wake kwa hadhira iliyokusudiwa ipate ujumbe.
 
Hata kule kuzuia magazeti yasisomwe kwa kirefu sijui kama kulileta tija labda mauzo kuongezeka au ilikuwaje vinginevyo lilikuwa agizo lisilo na mpango.
 
Nimeona mjadala wa “Kusoma magazeti”. Nimeelekeza TCRA kuruhusu UBUNIFU kwenye tasnia ya Habari. Staili ya usomaji we magazeti imeongeza MVUTO kwenye usomaji huo, ni jambo linapaswa KUTIWA MOYO badala ya kuzuiwa. Waandishi endeleeni na ubunifu kwenye kusoma magazeti.

Maelekezo mengine yeyote ambayo TCRA inatoa kwenye sekta ya habari yanapaswa kuwa WEZESHI na sio ZUIZI. Ni muhimu TCRA ijenge utamaduni wa kuzungumza kabla ya kuagiza.

Amendika Nape kwemye ukurasa wake wa X.

****
Mpaka matamko yanatoka na kukinzana hivi, ina maana huwa hawawasiliani kabla hawajatoa matamko? Wizara hazina mawasiliano mpaka wanakuja kutiana aibu hivi?

Au ni maigizo kuonesha wanafanyakazi na kweli wapo upande wa wananchi. Yaani wanatengeneza tatizo halafu wanakuja kulitatua.

Kwenu Wakuu.
KITENGE ALIMUOKOA WAKATI ULEEEE
 
Hata kule kuzuia magazeti yasisomwe kwa kirefu sijui kama kulileta tija labda mauzo kuongezeka au ilikuwaje vinginevyo lilikuwa agizo lisilo na mpango.
Mkuu,

Hilo katazo alilitoa nani? Serikali au wenye magazeti?
 
Vitu vingine bhana

Igeni Sky news

Lowasa: Ukosefu wa Ajira ni bomu linalosubiri kuripuka

Mtu anaajiriwa clouds kutusomea magazeti ambayo Yako mitandaoni 😂😂😂
Yule Meku mwenzako TCRA alidhani atasifiwa na serikali kutokana na jinsi Kitenge alivyosoma kadhia ya sukari.
Kuita kipindi Good Morning/Habari ya asubuhi kuna Ubaya gani?
Mbona Taasisi yao ya TCRA hawaiandiki kwa kiswahili?
 
Back
Top Bottom