Magazeti yanayomsafisha Lowassa haya hapa!

Ifuatayo ni orodha ya magazeti ya Tanzania ambayo wamiliki wake au wahariri wake au wote wamiliki na wahariri wamekuwa wakitumika kumsafisha Edward Lowassa katika mradi wake wa kutaka kwenda Ikulu 2015 kwa gharama yoyote ile. Magazeti haya yalitumiwa sana kupotosha umma kuhusu matokeo ya vikao vya NEC na Kamati Kuu ya CCM Dodoma juzi na kutoa habari na picha za kumpamba Lowassa kila mara akitumia viongozi wa dini njaa kujisafisha:
Wewe uliendika unatumiwa na nani?Thibitisha kauli yako"No Research,No right to speak"
 
Kwa mtu yoyote makini, ukisoma magazeti ya Tanzania unaona kabisa yako upande gani. Uweledi kwenye uandishi wa habari Tanzania na kufanya kazi bila woga wala upendeleo hakuna kutokana na njaa kali ya waandishi wa habari na wengi wao kutokwenda shule.

Ndiyo maana magazeti haya mengi yalitumika kujenga hisia kuwa fisadi Lowassa ni victim wa vita ya Urais ya 2015, kumbe ukweli unabaki palepale kuwa huyu ni mtuhumiwa mkubwa wa rushwa. Lazima afukuzwe kwenye chama na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zake.

Naweza kutofautiana na mtoa mada katika kuzungumzia magazeti kiujumla ndio maana hata Raia Mwema na Dira kuna wakati wanamsafisha Lowassa, na wakati mwingine wanamgonga, hali kadhalika Mwananchi na Tanzania Daima., kwa hiyo si vyema sana kushutumu chombo ni bora kujadili habari moja moja japo mizania inaangukia katika utetezi kwa Lowassa ambao umefikia mahali ambapo hata baadhi yetu tunafumbia macho yale tuliyoyaanzisha wenyewe kuhusu Lowassa na wenzake na sasa tunamsafisha.
 
Huyu anadhani kuwa magazeti yanatakiwa kuandika kwa mrengo fulani. Ukweli ni lazima usemwe bila kujali unamhusu nani

Mpita Njia, si sahihi kwa magazeti kumshambulia mtu tu kila mara au kutumika kumsafisha mtu mbele ya jamii. Magazeti yanatakiwa yawe huru, yaandike ukweli ili kuelimisha jamii bila woga au upendeleo. Ukiangalia tasnia ya habari Tanzania hivi sasa utaona media imegawanyika kati ya pro-mafisadi na anti-mafisadi. Karibu kila newsroom na gazeti sasa hivi limeingiliwa kupitia wamiliki, wahariri na reporters. Hakuna objectivity na editorial independence. Waandishi wamekuwa na roho nyepesi kama kuku na kununuliwa
 
Mpita Njia, si sahihi kwa magazeti kumshambulia mtu tu kila mara au kutumika kumsafisha mtu mbele ya jamii. Magazeti yanatakiwa yawe huru, yaandike ukweli ili kuelimisha jamii bila woga au upendeleo. Ukiangalia tasnia ya habari Tanzania hivi sasa utaona media imegawanyika kati ya pro-mafisadi na anti-mafisadi. Karibu kila newsroom na gazeti sasa hivi limeingiliwa kupitia wamiliki, wahariri na reporters. Hakuna objectivity na editorial independence. Waandishi wamekuwa na roho nyepesi kama kuku na kununuliwa

Umeweka vyema lakini kuna utata sana, maana sasa unasema kuna pro mafisadi na anti mafisadi!!! Duh!! Hivi kuna mwandishi makini atakubali kuitwa yuko pro mafisadi? Wao wanasema hakuna fisadi ni "siasa za 2015".... Duh!! Sasa rada, richmond ni siasa!!! Yaani hadi mtu unatamani kulia.. Tuwe wakweli kama mtu kaiba hata akisema "niliiba na Halisi, na ..... Nao ni wezi na ..... Alinituma nikaibe," huwa si utetezi mbele ya sheria. Mwizi tena akishakubali kuwajibika hana tena sababu leo kuibuka na kusema, "na wewe hakimu ulijua naiba".... Hahaa!!
 
Wewe uliendika unatumiwa na nani?Thibitisha kauli yako"No Research,No right to speak"

Nimefanya research yangu kwa zaidi ya mwaka sasa kwa kuangalia mwenendo wa magazeti haya. Nimesoma kwa undani habari kuu wanazozitoa kwenye kurasa zake za mbele kuhusu Lowassa, nimeangalia picha wanazotoa za Lowassa kwenye michango ya harambee, nimeangalia anaandikwa mara ngapi, mara ngapi anaandikwa vizuri na mara ya ngapi anaandikwa vibaya. Nimegundua pia hata MwanaHalisi, ambalo zamani liliongoza kwa habari za uchunguzi na kueleza ukweli kuhusu madudu ya Lowassa, sasa limekuwa likiandika habari za kumjenga tu kila mara.

Kuna vyombo vya utafiki kama REDET, Synnovate au Push Observer, ambavyo vinaweza kufanya utafiti wa kisayansi zaidi kwenye hili na kuonesha ukweli wa hili jambo kwa takwimu halisi -- numbers don't lie.
 
Kuna upotoshaji (misinformation) inayofanywa kwa makusudi kupitia magazeti. Nayo ni kujaribu kujenga dhana potofu kuwa vita dhidi ya ufisadi ndani ya CCM maarufu kama kujivua magamba, ni vita itokanayo na makundi yanayogombania urais wa 2015. Kwa maana hiyo wanataka ufisadi wa Richmond, rada, EPA, wote utupiliwe mbali kwani hiyo ni vita ya Urais wa 2015.

Anayesimamia propaganda hii ni mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru, ambaye amejaribu bila mafanikio kumshawishi Rais Kikwete aachane na dhana ya kujivua gamba ili kumuokoa Lowassa. Kingunge amezeeka vibaya baada ya kuona njaa inamkabili uzeeni akahamia kambi ya Lowassa.

Vita dhidi ya ufisadi ni ngumu mno, na CCM ikishindwa kupambana nao Watanzania wataihukumu kwenye uchaguzi ujao.
 
Mengi ya magazeti uliyoyataja ni magazeti makini na ambayo habari zake zote zinashirikisha pande zote zinazohusika ukiondoa Habarileo na Daily News ambayo kama sio ruzuku ya kodi zetu yangelikua yameisha kufa zamani.

Unapashwa kuelewa kuwa habari hazizuki kama unavyofikiri. Habari ni reflection ya nayotokea katika jamii ikiwemo chama tawala CCM. Nani asie fahamu ya kua CCM kunamakundi, nani asie fahamu ya kua CCM mambo ovyo ovyo, nani asiefahamu ya kua ndani ya CCM vurugu tupu nani asiefahamu ya kua kama mafisadi ndani ya CCM na serikali ni karibu ya asilimia 99 akiwemo rais mwenyewe?.

Magazeti yaliyo makini yanaandika haya na kufuatilia nani asiefahamu ya kua siasa na sera ya CCM ni kusafishana. Kama kweli zoezi la kujivua gamba lingetekelezwa kama kweli walikua na nia thabiti kwa kuwachukulia hatua wahusika wote mara moja bila kujali nafasi zao serikali na CCM tusingekua na ngojera zinazoendelea, siku tisini, wajipime wenyewe, mkutano mkuu, NEC,CC n.k. CCM msitafute Mchawi tatizo na chimbuko la matatizo liko ndani ya CCM KUCHAFUANA NA KUSAFISHANA NI SERA YA CCM.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
we uko mtandao wa kusafisha nini?.lowasa si mchafu wapo yeye ameshajivua kashifa ya richmond so hana haja ya kusa34siwa
 
Kwa mtu yoyote makini, ukisoma magazeti ya Tanzania unaona kabisa yako upande gani. Uweledi kwenye uandishi wa habari Tanzania na kufanya kazi bila woga wala upendeleo hakuna kutokana na njaa kali ya waandishi wa habari na wengi wao kutokwenda shule.

Ndiyo maana magazeti haya mengi yalitumika kujenga hisia kuwa fisadi Lowassa ni victim wa vita ya Urais ya 2015, kumbe ukweli unabaki palepale kuwa huyu ni mtuhumiwa mkubwa wa rushwa. Lazima afukuzwe kwenye chama na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zake.
Duh!ID name yako kiboko!Nimeipenda.
 
Mimi niliacha kusoma MWANA HALISI na Tanzania Daima muda mrefu sasa baada ya kuona jinsi walivyonyea mavi kambi ya kuandika ukweli daima na kupambana na ufisadi na kuhamia kambi ya mafisadi. Waandishi wa Tanzania wenye roho za kuku wanachangia kuliteketeza taifa kama waandishi wa habari wa Rwanda walivyohusika na mauaji ya kimbari ya 1994 nchini mwao.
Kumbe sasa unasoma uhuru na mzalendo? Ulipoacha kusoma MWANAHALISI na Tanzania Daima uliambiwa hayauziki sasa hivi? Watu wengine kwa kujikweza hamjambo. Wewe ni kajitu kadogo sana ktk jamii hii, kenge wewe!
 
Mpaka hivi sasa, genge la kina Lowassa limejaribu na kushindwa kufanikiwa kwenye kila jitihada za kuyaingia au kuyamaliza kabisa magazeti mawili pekee yaliyosimama kidete kuueleza umma wa Tanzania ukweli. Nayo ni RAIA MWEMA na DIRA.
ZINGATIA hapo kwenye RED mkuu, wewe ni OWNER ama MDAU wa Gazeti la RAIA MWEMA na DIRA hivyo unawapondea your COMPITITORS ili wananchi wasiyanunue hayo magazeti? Wewe mpumbavu sana leave the market alone kama yamenunuliwa tutaona sie wasomaji na sio wewe utuambie.

Hata hivyo haya magazeti yako hayana sifa kubwa kuliko MWANAHALISI wala MWANANCHI n.k, wewe Fisadi hajakufuata kwa sababu magazeti yako hayana SOKO kama haya ULIYOYATUKANA kimakusudi kabisa.

Please your marketing aproach is WRONG mzee.
 
Huyu nae yupo kwenye huo mtandao wakumsafisha EL

na wewe unamsafisha nani? wewe kwa nafasi yako na uelewa wangu kamwe HUWEZI kuniambia nini cha kufanya hata kama nitakuwa mbali na kambi yako. Na kwa taarifa yako sina kambi isipokuwa ninachokataa ni kutaka kutuaminisha jinsi wewe na kambi yako, hasa wanaokutuma kutaka kutufanya tuamini ktk mawazo yenu yenye chuki kwenye biashara zenu.
Unapoongelea kikao cha NEC kwenye Mtanzania, kwani Viongozi wa CCM wamesemaje? -"SIRI ZA VIKAO VYA NEC ZIMEVUJA", sasa nini kosa la magazeti hayo? tuache ushabiki usiokuwa na mwelekeo chanya kwa nchi yetu na badala yake tuelekeze nguvu zetu ktk kukemea maovu ambayo kwa mwelekeo wako, katu huwezi kuyakemea.
 
no research no right to speak,weka ushaidi wewe to support ur thread
 
]Nikusahihishe,
mwananchi si GAZET PENDWA,
WACHA NIKUTAJIE MFANO WA MAGAZET PENDWA
RISASI,SANI,TUNU,KIU,UWAZI,HAMU, NA MENGINE YA AINA HIYO

Ndio ni magazeti pendwa lakini kwa WATU gani?
Je ni kwa watu wanaotaka mambo ya serious kama ya KIUCHUMI, KISIASA, KIJAMII yanayo hitaji ANALYSIS ya kina? Au ni ya UDAKU kama EL alivyo wahi kunena? Kumbuka ya kuwa bila SIASA SAFI, UCHUMI huo UDAKU wako haupo wewe.
 
Back
Top Bottom