Magazeti yanayomsafisha Lowassa haya hapa!

wanajf mwenye ushaidi kuwa lowasa ni fisadi atujuze,kwani tnaweza hukumiwa bila sababu,tmechoka na tetesi jaman u thinkers,juzi nec ddma kaeleza wazi khsu richmond,ni upi ufisadi wake mwingine????

Mbona hukanushi ushahidi mdogo sana uliotolewa na Double Agent? AMA kweli tuna pumba nyingi humu
 
Ufisadi wa Lowassa huu hapa:

1. Kununua jumba la kifahari London, Uingereza, lenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 1 za Tanzania.

Metropolitan police wa Uingereza wanachunguza suala hili. Wamewasiliana na anti-money laundering unit ya Tanzania kuchunguza suala hili.

2. Ufisadi wa Nyumba ya Sanaa

Lowassa amehisika kufanya uporaji wa ardhi ya Nyumba ya Sanaa iliyopo karibu na Movenpik Hotel (zamani Serena Hotel). Nyaraka zinaonesha yeye ni mmiliki wa kampuni inayojenga gorofa kubwa kwenye eneo hilo la Nyumba ya Sanaa.

3. Utajiri usioelezeka (unexplained wealth)

Akiwa kama kiongozi wa umma, Lowassa amejilimbikizia mali nyingi sana za thamani ya mabilioni ya shilingi. Mali alizo nazo haziendani na kipato chake kama kiongozi wa umma. Sheria ya kupambana na rushwa Tanzania iko wazi kuwa kiongozi wowote wa umma mwenye utajiri usioendana na mapato yake halali anastahili kufikishwa mahakamani. Kutokana na sera za kulindana na kuogopana, Lowassa, Andrew Chenge, na viongozi wengine wa umma hawajafikishwa mahakamani kwa kosa hili na PCCB. Pia kwenye fomu za kila mwaka za kutaja mali, Lowassa haja declare assets zake zote. Ana miliki Alphatel, Alpha Schools, Alpha House, apartment blocks Dar es Salaam, Arusha na nje ya nchi.

4. Land grabbing

Alipokuwa Waziri wa Ardhi enzi za utawala wa Mwinyi alihusika na uporaji mkubwa wa ardhi sehemu mbali mbali nchini.

5. Richmond

Lowassa ndiye aliyeagiza TANESCO waporwe madaraka ya kusimamia tenda ya umeme kinyume na sheria ya manunuzi, PPRA. Aliunda kamati ya makatibu wakuu na kusimamia kwa karibu majadiliano ya kamati hii na nRichmond na kuagiza wapewe tenda wakati Tanesco waliikataa Richmond kuwa haifai. Lowassa ndiye mhusika mkuu wa kashfa ya ufisadi ya Richmond ndio maana alilazimika kujiuzulu.

6. Need I say more?

Lowassa ni mchafu wa maadili. Anapenda sana mali, amejilimbikizia utajiri kuliko kipato chake halisi. Wafuasi wake wanamfanananisha na Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Tofauti ya Zuma na Lowassa ni kuwa Zuma alifikishwa mahakamani na kusafishwa na mahakama. Lowassa apelekwe kortini kujibu shutuma za ufisadi, akishinda kesi ndio atakuwa amesafishwa kweli. Si kwa kutumia vyombo vya habari na waandishi wa habari wenye njaa.

Mkuu nakumbuka wakati ule alizuia viwanja vya Mnazi Mmoja visiporwe.
 
Jamhuri halijaanza kutoka unathibitishaje? Kama unahiyo Pay roll ya wanaolipwa na Lowassa scan weka wazi kama huwezi kaa kimya.

Hivi unategemea nini kiandikwe ktk gazeti linalofadhiliwa na Lowassa? Fred Lowassa amenukuliwa akitamba kuwa yeye ndio mfadhili mkubwa wa gazeti hilo, aliyasema maneno hivi karibuni mkoani Dodoma ktk hotel ya NAM wakati vikao vya CCM vinaendelea. Hebu muulize kwanza, akikanusha tumwage radhi na mengine tunayowahifadhi kiubinadamu
 
Mchafu ni mchafu tu na atabaki mchafu. Lowassa ni mchafu wa maadili, hata Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alijua hilo na alituonya tuepukane na huyu mtu. Ni kama nguruwe amezoea kuchea kwenye matope, hata umuogeshe vipi halisi yake ni kuchafuka tu na ataendelea kuwa mchafu tu come what may.

Na baba huyo huyo wa taifa alituambia mkapa ni Mr Clean!
 
Na baba huyo huyo wa taifa alituambia mkapa ni Mr Clean!

Acha ujinga wewe, Hayati Mwl. Nyerere alipokuwa anampigia debe Mkapa alikuwa msafi. Kashfa pekee ya Mkapa ni mradi wa Kiwira. Kashfa hii aliipata baada ya kuwa Rais, tena ktk kipindi chake cha pili cha uongozi. Tatizo lenu nyie mafisadi ni mahodari sana wa kubadilisha maneno.
 
Ufisadi wa Lowassa huu hapa:

1. Kununua jumba la kifahari London, Uingereza, lenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 1 za Tanzania

Metropolitan police wa Uingereza wanachunguza suala hili. Wamewasiliana na anti-money laundering unit ya Tanzania kuchunguza suala hili.

2. Ufisadi wa Nyumba ya Sanaa

Lowassa ni mhusika mkuu wa kufanya uporaji wa ardhi ya Nyumba ya Sanaa iliyopo karibu na Serena Hotel (zamani Movenpik Hotel). Nyaraka zinaonesha yeye ni mmiliki wa kampuni inayojenga gorofa kubwa kwenye eneo hilo la Nyumba ya Sanaa.

3. Utajiri usioelezeka (unexplained wealth)

Akiwa kama kiongozi wa umma, Lowassa amejilimbikizia mali nyingi sana za thamani ya mabilioni ya shilingi. Mali alizo nazo haziendani na kipato chake kama kiongozi wa umma. Sheria ya kupambana na rushwa Tanzania iko wazi kuwa kiongozi wowote wa umma mwenye utajiri usioendana na mapato yake halali anastahili kufikishwa mahakamani. Kutokana na sera za kulindana na kuogopana, Lowassa, Andrew Chenge, na viongozi wengine wa umma hawajafikishwa mahakamani kwa kosa hili na PCCB. Pia kwenye fomu za kila mwaka za kutaja mali, Lowassa haja declare assets zake zote. Ana miliki Alphatel, Alpha Schools, Alpha House, apartment blocks Dar es Salaam, Arusha na nje ya nchi.

4. Land grabbing

Alipokuwa Waziri wa Ardhi enzi za utawala wa Mwinyi alihusika na uporaji mkubwa wa ardhi sehemu mbali mbali nchini.

5. Richmond

Lowassa ndiye aliyeagiza TANESCO waporwe madaraka ya kusimamia tenda ya umeme kinyume na sheria ya manunuzi, PPRA. Aliunda kamati ya makatibu wakuu na kusimamia kwa karibu majadiliano ya kamati hii na nRichmond na kuagiza wapewe tenda wakati Tanesco waliikataa Richmond kuwa haifai. Lowassa ndiye mhusika mkuu wa kashfa ya ufisadi ya Richmond ndio maana alilazimika kujiuzulu.

6. Need I say more?

Lowassa ni mchafu wa maadili. Anapenda sana mali, amejilimbikizia utajiri kuliko kipato chake halisi. Wafuasi wake wanamfanananisha na Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Tofauti ya Zuma na Lowassa ni kuwa Zuma alifikishwa mahakamani na kusafishwa na mahakama. Lowassa apelekwe kortini kujibu shutuma za ufisadi, akishinda kesi ndio atakuwa amesafishwa kweli. Si kwa kutumia vyombo vya habari na waandishi wa habari wenye njaa.

Njia pekee ya Lowassa kusafishwa na tuhuma za ufisadi ni kufikishwa mahakamani iwapo anataka kuwa kama Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Vinginevyo ataendelea kunuka ufisadi tu mbele ya Watanzania.
 
Njia pekee ya Lowassa kusafishwa na tuhuma za ufisadi ni kufikishwa mahakamani iwapo anataka kuwa kama Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Vinginevyo ataendelea kunuka ufisadi tu mbele ya Watanzania.

Siku Fisadi huyu akifanya kosa la kukubali kutinga mahakani ndio itakuwa mwisho wake ktk medani za kisiasa hapa bongo. Sidhani kama ataweza kuidhibiti hali itakavyokuwa mitaani, maana public court imeishamuhukumu.
 
Hivi katika hizi kukuru kakara za kusafishana,ni lini haswa tutasema EL sasa ni msafi na hivyo "akumbatiwe"?

Pls pls, let me know akishakuwa msafi, kwa sababu ni almost two years nasikia tu bado yuko anasafishwa.

Inaonekana alikuwa mchafu sana, so anahitaji kulowekwa kwenye sabuni kali kwa muda mrefu sana. Tatizo ni timing ya kuanza kumsafisha, kila mara wanakosea halafu inabidi zoezi lianze tena upya. Kwa hiyo keep on waiting mkuu. Kitu kikiwa kichafu sana kinahitaji umakini wakati wa kukisafisha, na kwa kuwa tayari watu walikuwa wanajua kwamba ni kichafu sana, lazima watakuwa makini sana kukichunguza ili wajiridhishe kama kimekuwa safi kabla ya kufanya maamuzi ya kukitumia au la.
 
Acha ujinga wewe, Hayati Mwl. Nyerere alipokuwa anampigia debe Mkapa alikuwa msafi. Kashfa pekee ya Mkapa ni mradi wa Kiwira. Kashfa hii aliipata baada ya kuwa Rais, tena ktk kipindi chake cha pili cha uongozi. Tatizo lenu nyie mafisadi ni mahodari sana wa kubadilisha maneno.

Nchi hii bana, mpaka mvua zisiponyesha mnasema Lowassa, El kaondoka miaka minne iliyopita nn kimebadilika! Acheni siasa za majitaka!
 
Mimi niliacha kusoma MWANA HALISI na Tanzania Daima muda mrefu sasa baada ya kuona jinsi walivyonyea mavi kambi ya kuandika ukweli daima na kupambana na ufisadi na kuhamia kambi ya mafisadi. Waandishi wa Tanzania wenye roho za kuku wanachangia kuliteketeza taifa kama waandishi wa habari wa Rwanda walivyohusika na mauaji ya kimbari ya 1994 nchini mwao.

Nina wcwc inawezekana hata bei ya gazeti huijui nn kusoma!
 
........ndugu! kama umetumwa ishia huko huko, RAIA MWEMA na DIRA na MEMBE wenu, hamuwezi tena kutuaminisha ujinga mnaoamini, unataka tutumie lugha ngumu afu useme hekima zimeturuka? mpuuzi kweli wewe, sisi sio wajinga tena kama unavyofikiri, upuuzi wako ufanyie huko huko! ....ck u! upuuzi hauhalalishwi kwa upuuzi, lakininkwa hili la kwako, hamna mwenye akili timamu wa kukuvumilia, kwa sababu utakuwa umetufanya wote wajinga kama wewe!!!!

Matusi siku zote ni ishara ya mtu kukosa hoja za kujibu na kushia kutoa mapovu kama mbwa mwenye ugonjwa wa kichaa. Nashauri mtoa mada akupuuzie tu asijibizane na wewe kwani ukirushiana matope na nguruwe anayeshinda ni nguruwe ambaye matope ni jadi yake.
 
Ifuatayo ni orodha ya magazeti ya Tanzania ambayo wamiliki wake au wahariri wake au wote wamiliki na wahariri wamekuwa wakitumika kumsafisha Edward Lowassa katika mradi wake wa kutaka kwenda Ikulu 2015 kwa gharama yoyote ile. Magazeti haya yalitumiwa sana kupotosha umma kuhusu matokeo ya vikao vya NEC na Kamati Kuu ya CCM Dodoma juzi na kutoa habari na picha za kumpamba Lowassa kila mara akitumia viongozi wa dini njaa kujisafisha:

1. Mtanzania na RAI

Ingawaje hayasomwi tena na Watanzania makini, magazeti haya yanamilikiwa na Rostam Aziz, kingmaker wa viongozi mafisadi Tanzania na chief financier wa Lowassa.

2. MwanaHalisi

Gazeti linalomilikiwa na Saeed Kubenea ambaye sasa amefika bei kwa mafisadi na anawatumikia kama kibarua wao kuwasafisha na kuwatukana maadui wao, hususan Waziri Samuel Sitta.

4. Tanzania Daima

Gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ambalo mhariri wake mkuu, Absalam Kibanda, yuko kwenye payroll ya Lowassa na Rostam kwa miaka mingi sana

5. Jamhuri (soon-to-be launched)

Gazeti la Lowassa ambalo litazinduka hivi karibuni, wahariri wake wakiwa ni vijana wa Lowassa wa siku nyingi -- Deodatus Balile na Manyerere Jackton -- ambao amewaazima kutoka kwenye magazeti ya rafiki yake Rostam. Hii ni baada ya jarida la Lowassa la Umoja linaloendeshwa na Absalom Kibanda wa Tanzania Daima kufeli na mpaka kufikia hatua ya kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake.

6. Mwananchi

Kuna "mdudu" ameingia hivi karibuni kwenye gazeti pendwa la kila siku la Tanzania ambalo na gazeti hili nalo sasa linatumiwa kwenye mradi wa kumsafisha Lowassa. Hii ilijidhihirisha kwenye mkutanon wa juzi wa NEC ambapo habari kuu iliyotoka kwenye kikao cha NEC iliandikwa na mtu mmoja na kuchapishwa kwenye magazeti matatu -- Mwananchi, Tanzania Daima na Mtanzania -- neno kwa neno.

7. Daily News

Kaimu Mhariri Mkuu wa Daily News, Mkumbwa Ally, amejisalimisha kambi ya Lowassa ili athibitishwe na kupewa cheo kama Mhariri Mkuu wa magazeti ya serikali, TSN. Wakati huo huo, gazeti la Habari Leo lililo chini ya TSN limekuwa likipambana kuleta habari za ukweli kuhusu mafisadi. Hii imesababisha habari za Daily News na Habari Leo kuhusu kujivua gamba kutofautiana kabisa wakati yote ni magazeti ya serikali chini ya kampuni moja.

  • Mpaka hivi sasa, genge la kina Lowassa limejaribu na kushindwa kufanikiwa kwenye kila jitihada za kuyaingia au kuyamaliza kabisa magazeti mawili pekee yaliyosimama kidete kuueleza umma wa Tanzania ukweli. Nayo ni RAIA MWEMA na DIRA.

sikubaliani na wewe. Mwanahalisi, Tanzania daima na mwananchi hawamsafishi Lowas hata kidogo. Wanacho kifanya ki kuwa wanaongea bila unafiki kuwa Lowasa ni fisadi na mwizi lakin si yeye tu hata sita na wale wanaojifanya wapambanaji ndani a ccm ni wanafiki wala hawana uzalendo wowote. Kusema sita mi mnafiki na Fisadi haina maana kumsafisha Lowasa hata kidogo ila ni kuanika uovu wa wanasiasa wote ili tuwajue. Wapenzi wa Sita wanaohadaiwa kuwa ni mtakatifu ndani ya ccm wamekuwa desperate baada ya kuona anavochambuliwa uovu wake ni kufikiria hao wanaoibua ouvu wake ka Kubenea na Kibanda ni watu walioongwa na Lowasa kumchafua Sita. Mi nawashukuru san kina Kubenea kwani watatuwezesha kujua viongozi hasa wanaopaswa kuwa rais wetu ni kina nani. Sio sita, si Lowasa, si Membe wala si Maghufuli. Fuatilia Mwisho utajua wanaongelea nini ila ukija kichwa kichwa kama unavohamaki ukisikia jina la Sita linatajwa hutaelewa kitu. Simpendi Lowasa fisadi mkubwa. Sita naye simpi nafasi ya kuwa kiongozi bora hata kidogo kwa kuwa ni wanafiki wanaotuhadaa ni mashujaa huku wanatafuna fedha za walipakodi kupitia chama chao cha mafisadi.
 
Naweza kutofautiana na mtoa mada katika kuzungumzia magazeti kiujumla ndio maana hata Raia Mwema na Dira kuna wakati wanamsafisha Lowassa, na wakati mwingine wanamgonga, hali kadhalika Mwananchi na Tanzania Daima., kwa hiyo si vyema sana kushutumu chombo ni bora kujadili habari moja moja japo mizania inaangukia katika utetezi kwa Lowassa ambao umefikia mahali ambapo hata baadhi yetu tunafumbia macho yale tuliyoyaanzisha wenyewe kuhusu Lowassa na wenzake na sasa tunamsafisha.

Mkuu Halisi,

Je, hiyo bold na highlight haionyeshi dalili ya kwamba watu wamekata tamaa baada ya kuona kwamba muasisi wa operation ya kuvua gamba amekuwa ni mcheza sarakasi na mazingaombe na hivyo anacheza na hisia za wananchi?

Kuna mambo yanaendelea kwenye magazeti ambayo yanachanganya na kukatisha tamaa. Labda wewe unaweza kunisaidia kidogo kuniweka sawa [kama una info zozote]. Pia kuna mambo yanaendelea kwenye Kamati Kuu na NEC ambayo nashindwa kuyaelewa hasa yana mantiki gani. Naomba nitoe maelezo ya kina halafu wewe utanisaidia huko mbele ya safari.

Baada ya NEC ya April kulizuka swali la kwamba ni nani angewaandikia barua mafisadi ya kuwataka wajieleze. Mpaka leo hii hakuna anayejua nini kilikuwa kinaendelea. Zilipigwa dana dana mpaka baadaye tukaambiwa walikutana na Msekwa na kilichoongelewa kwenye hivyo vikao kiliandikwa kwenye magazeti.

Kamati Kuu ilipokutana baada ya kikao cha April [sikumbuki ni mwezi gani], iliisifu Secretariat mpya kwamba inafanya vizuri sana na sifa hiyo ilikuwa ni ile mikutano ya kuzunguka kutangaza Operation Vua Gamba ya siku 90. Juzi Lowassa kasema kwamba hiyo secratariat iliyopongezwa ilikuwa inamchafua kwa kumwita fisadi, kitu ambacho Lowassa hakubaliani nacho anaona kama anasingiziwa, anachafuliwa na anadhalilishwa.

Rostam Aziz alipojiuzulu, Kamati Kuu ilimpiga stop Nape Nnauye asiende kwenye kampeni Igunga, lakini Rostam ambaye ni fisadi aliyebobea akaombwa ashiriki kampeni na alishiriki. Nape Nnauye alipotua Igunga alishambuliwa kwamba kwanini alienda huko na ilihali alikuwa amekatazwa na hakurudi tena. Tafsiri ya hii sarakasi ni nini?

Juzi kwenye kikao cha NEC, JK kasema wameenda Dodoma kwenye mkutano wa kukijenga chama na sio kukibomoa chama. Mukama kwenye TV hivi majuzi kasema kwamba Kamati inayoundwa ya maadili/nidhamu itatoa maamuzi kwa nia ya kukijenga chama na sio kukibomoa. Hizi kauli zinatatiza sana.

Majuzi kuna gazeti limeandika kwamba Kamati ya Maadili inayoundwa inakusanya ushahidi wa siasa za makundi, tayari hawa wameisha hama kwenye agenda kuu ya kuwavua magamba mafisadi, wamekimbilia kwenye hoja nyingine kabisa. Hapa hawajahamisha magoli? Tuhuma za msingi zilikuwa ni ufisadi, hizi tuhuma za siasa za makundi zinatoka wapi? Tukishaanza kukusanya hizo tuhuma uchwara za siasa za makundi hapo hatapona mtu, maana hata akina Sitta ambao wamekuwa wakiropoka kwamba walifanyiwa njama ya kuondolewa kugombea u-Spika nao wataingia humo. Akna Nape walituhumiwa kwa siasa za maji taka au siasa uchwara [according to RA] na wao hawatapona. Je, baada ya kuhamisha magoli kuna mtu atapona?

Nimesoma leo hii nadhani kutoka gazeti la Mtanzania, Benno Malisa anawatuhumu wazee kwamba wao ndio wachawi wa UVCCM na kwa kufuatilia mwenendo wa vikao, hayo yalikuwa ni makombora yaliyomlenga Tyson [Mzee Wassira] na Lukuvi ambao walimshambulia Malissa kwenye kikao cha Kamati Kuu iliyopita baada ya kuuliza viongozi wa UVCCM wa mikoa wamekuja Dodoma kufanya nini?

Kwa mwenendo wa haya mambo yanavyokwenda, baadhi ya watu ambao mlianza nao hizi harakati za vita ya ufisadi wamefika mahali wamekata tamaa maana CCM sasa haina msemaji mkuu na kila anayeibuka anajisemea la kwake na hakuna anayeweza kumchukulia hatua mwingine. Mgogoro wa Arusha kati ya Katibu wa CCM mkoa [Mary Chatanda] vs James ole Millya uko pale pale na Mary Chatanda sasa ameamua kukaa kimya maana akina Tyson wanaokwenda kusuluhisha huo mgogoro wanashindwa kuchukua hatua stahiki. UVCCM Taifa wameenda Arusha wameshindwa kusuluhisha huo mgogoro. Millya kwa kushirikiana na Malissa wamefungua matawi ya CCM bila kibari cha Polisi na hakuna aliyewafanya kitu, huku baadhi ya viongozi wa ngazi ya wilaya wakipinga, je, waliwafanya nini?

Ukiangalia huo mtiririko unafika mahali unakata tamaa na ndio maana sasa wanaomsafisha Lowassa wamepata nguvu na wengine wameona ni ujinga kuendelea na hoja ufisadi huku viongozi wa juu wa chama wakiwa hawajui wafanye nini. Mwisho wa siku JK na Lowassa watabaki wanagonga bilauri za shampeni isio na kilevi [maana JK hanywi pombe] huku wakicheka na kutuacha solemba tukiendelea kutoana macho.
 
Kama walivyosema wengine, dawa ya Lowassa ni ndogo tu... Apelekwe mahakamani haraka kujibu tuhuma za abuse of public office kuhusu Richmond na unexplained wealth kutokana na utajiri mkubwa alionao wa mashaka kulingana na mapato yake halali kama kiongozi wa umma. Hachomoi hapo, lazima aishie Ukonga tu. Hii ndio jinsi ya kupiga FULL STOP ufisadi wa Lowassamania!
 
Mkuu Halisi,

Je, hiyo bold na highlight haionyeshi dalili ya kwamba watu wamekata tamaa baada ya kuona kwamba muasisi wa operation ya kuvua gamba amekuwa ni mcheza sarakasi na mazingaombe na hivyo anacheza na hisia za wananchi?

Ni kweli kabisa, sarakasi za waasisi zimetukatisha tamaa sana na bila kuuma maneno, Sitta na JK ndio wametufikisha hapa. Sitta dhambi ya kufunga mjadala wa Richmond itamtafuna milele na JK kuyumba kwake katika kufanya maamuzi nako kutaligharimu Taifa na baadaye yeye mwenyewe, potelea mbali CCM yake, haina maana, ila hatari yake ni Taifa kuangukia mikononi mwa FISADI.

Baada ya NEC ya April kulizuka swali la kwamba ni nani angewaandikia barua mafisadi ya kuwataka wajieleze. Mpaka leo hii hakuna anayejua nini kilikuwa kinaendelea. Zilipigwa dana dana mpaka baadaye tukaambiwa walikutana na Msekwa na kilichoongelewa kwenye hivyo vikao kiliandikwa kwenye magazeti.

Kamati Kuu ilipokutana baada ya kikao cha April [sikumbuki ni mwezi gani], iliisifu Secretariat mpya kwamba inafanya vizuri sana na sifa hiyo ilikuwa ni ile mikutano ya kuzunguka kutangaza Operation Vua Gamba ya siku 90. Juzi Lowassa kasema kwamba hiyo secratariat iliyopongezwa ilikuwa inamchafua kwa kumwita fisadi, kitu ambacho Lowassa hakubaliani nacho anaona kama anasingiziwa, anachafuliwa na anadhalilishwa.

Rostam Aziz alipojiuzulu, Kamati Kuu ilimpiga stop Nape Nnauye asiende kwenye kampeni Igunga, lakini Rostam ambaye ni fisadi aliyebobea akaombwa ashiriki kampeni na alishiriki. Nape Nnauye alipotua Igunga alishambuliwa kwamba kwanini alienda huko na ilihali alikuwa amekatazwa na hakurudi tena. Tafsiri ya hii sarakasi ni nini?

Juzi kwenye kikao cha NEC, JK kasema wameenda Dodoma kwenye mkutano wa kukijenga chama na sio kukibomoa chama. Mukama kwenye TV hivi majuzi kasema kwamba Kamati inayoundwa ya maadili/nidhamu itatoa maamuzi kwa nia ya kukijenga chama na sio kukibomoa. Hizi kauli zinatatiza sana.

Majuzi kuna gazeti limeandika kwamba Kamati ya Maadili inayoundwa inakusanya ushahidi wa siasa za makundi, tayari hawa wameisha hama kwenye agenda kuu ya kuwavua magamba mafisadi, wamekimbilia kwenye hoja nyingine kabisa. Hapa hawajahamisha magoli? Tuhuma za msingi zilikuwa ni ufisadi, hizi tuhuma za siasa za makundi zinatoka wapi? Tukishaanza kukusanya hizo tuhuma uchwara za siasa za makundi hapo hatapona mtu, maana hata akina Sitta ambao wamekuwa wakiropoka kwamba walifanyiwa njama ya kuondolewa kugombea u-Spika nao wataingia humo. Akna Nape walituhumiwa kwa siasa za maji taka au siasa uchwara [according to RA] na wao hawatapona. Je, baada ya kuhamisha magoli kuna mtu atapona?

Nimesoma leo hii nadhani kutoka gazeti la Mtanzania, Benno Malisa anawatuhumu wazee kwamba wao ndio wachawi wa UVCCM na kwa kufuatilia mwenendo wa vikao, hayo yalikuwa ni makombora yaliyomlenga Tyson [Mzee Wassira] na Lukuvi ambao walimshambulia Malissa kwenye kikao cha Kamati Kuu iliyopita baada ya kuuliza viongozi wa UVCCM wa mikoa wamekuja Dodoma kufanya nini?

Kwa mwenendo wa haya mambo yanavyokwenda, baadhi ya watu ambao mlianza nao hizi harakati za vita ya ufisadi wamefika mahali wamekata tamaa maana CCM sasa haina msemaji mkuu na kila anayeibuka anajisemea la kwake na hakuna anayeweza kumchukulia hatua mwingine. Mgogoro wa Arusha kati ya Katibu wa CCM mkoa [Mary Chatanda] vs James ole Millya uko pale pale na Mary Chatanda sasa ameamua kukaa kimya maana akina Tyson wanaokwenda kusuluhisha huo mgogoro wanashindwa kuchukua hatua stahiki. UVCCM Taifa wameenda Arusha wameshindwa kusuluhisha huo mgogoro. Millya kwa kushirikiana na Malissa wamefungua matawi ya CCM bila kibari cha Polisi na hakuna aliyewafanya kitu, huku baadhi ya viongozi wa ngazi ya wilaya wakipinga, je, waliwafanya nini?
Yote ulosema ni sahihi kabisa. Tatizo lilianza baada ya kikao cha Aprili kilichoazimia kina Lowassa wang'atuke kabla ya NEC ingine. Wakatafsiri NEC huwa inakaa baada ya miezi mitatu, wakaongeza chumvi kwa kuhesabu miezi mitatu ina siku tisini na wenye chama (mafisadi) wakacheza na maazimio (ndio maana hata waraka wameiba na kupeleka Mtanzania)yakawa hayataji majina. Sasa wenyewe wakahakikisha hizo siku tisini ndio zinasemwa sana na kukaa ktk vichwa vya watu na sio ufisadi wenyewe wala wizi, kwa hiyo watu wakaanza kuhesabu siku. Mukama akashituka (msomi) akaanza kusema hakuna cha siku tisini!! Hapo ndio ukaanza mchezo kwamba Nape ni mwongo amesema siku tisini wakati Mukama anasema hakuna siku tisini!!! Ni NEC ijayo, bila kujadili hoja ya msingi ya kuna ufisadi na mafisadi ni nani!! Siku tisini zikaisha na NEC ikachelewa hadi ilipofika, wenye chama wakasafirisha vijana Dodoma, wakasafirisha na watu wengine wenye taaluma zao, wakaandaa na wajumbe, wakaandaa na wazee, yaani wakawa na nguvu za ajabu na za kutisha, Dodoma ikawa ni yao. Mwenyekiti akatishika hadi hata wale wapiganaji wake wengine wakatishwa wasikanyage dodoma, wakawa wanatamba mafisadi na vijana wao wakaishia kusemwa tu kiujanja ujanja. Mwenyekiti wanasema akazidiwa nguvu, wakaona sasa nguvu ya mafisadi NEC ni kubwa. Nec ambayo nathubutu kusema asilimia kubwa wamepata nafasi kwa rushwa, ndio maana wanarudisha gharama katka ajenda kama hizo. Mmoja wapo, hamisi Mgeja amemwambia mtu kwamba kama akipewa milioni 5 kwanini asiseme anachotaka huyo mwenye kutoa!!! Hiyo ndio NEC anbayo JK na watu wake wakaona haiwezi kufukuza mafisadi ndio sasa wamehamishia hoja Kamati ya Maadili na Usalama ambayo sasa wameipa uwezo wa kumaliza kazi. Hoja hapa ndio vipi magazeti yakasema Lowassa kashinda maana iliaminishwa kwamba NEC hii ya juzi ndio fainali, lakini sasa inazidi kusogezwa Maadili, kamati ambayo iliandaa CC kabla ya NEC!! Ilishindwa ssa itaweza? Je, Lowassa atalala tu? Au atakuja na gia mpya ya kumtisha tena Mwenyekiti? Maana UVCCM walitisha Arusha na hawakuguswa, wakatisha Dodoma wameachwa, sasa watakuja kuingia hadi jikoni na wataachwa na siku zinasonga mbele watammaliza mwenyewe Mwenyekiti. Hoja ya kwamba watagonga glasi na EL siioni maana Lowassa kama ni ushindi ameupata kwa jasho lake, hakuna msaada wa JK. Na lowaassa si kama JK ambaye amemsamehe Mkapa aliyetaka kumnyima urais kabla ya JK na wenzake akiwamo Lowassa kumtisha na Mpaka kuzidiwa na kushindwa kuzuia nguvu ya mtandao wakati ule. Ajabu ni mbinu zile zile na pengine watu wale wale, wamemtisha JK akamuogopa EL!! Je, ataendelea kutishika hadi 2015?!! Huo ndio moto!!
 
Nchi hii bana, mpaka mvua zisiponyesha mnasema Lowassa, El kaondoka miaka minne iliyopita nn kimebadilika! Acheni siasa za majitaka!
Ujue amechokwa kwa uovu, ingekua ni mwema, ingekua jamani yaani hata mvua ikinyesha wanasema ni yeye kaileta toka Thailand
 
Ifuatayo ni orodha ya magazeti ya Tanzania ambayo wamiliki wake au wahariri wake au wote wamiliki na wahariri wamekuwa wakitumika kumsafisha Edward Lowassa katika mradi wake wa kutaka kwenda Ikulu 2015 kwa gharama yoyote ile. Magazeti haya yalitumiwa sana kupotosha umma kuhusu matokeo ya vikao vya NEC na Kamati Kuu ya CCM Dodoma juzi na kutoa habari na picha za kumpamba Lowassa kila mara akitumia viongozi wa dini njaa kujisafisha:

1. Mtanzania na RAI

Ingawaje hayasomwi tena na Watanzania makini, magazeti haya yanamilikiwa na Rostam Aziz, kingmaker wa viongozi mafisadi Tanzania na chief financier wa Lowassa.

2. MwanaHalisi

Gazeti linalomilikiwa na Saeed Kubenea ambaye sasa amefika bei kwa mafisadi na anawatumikia kama kibarua wao kuwasafisha na kuwatukana maadui wao, hususan Waziri Samuel Sitta.

4. Tanzania Daima

Gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ambalo mhariri wake mkuu, Absalam Kibanda, yuko kwenye payroll ya Lowassa na Rostam kwa miaka mingi sana

5. Jamhuri (soon-to-be launched)

Gazeti la Lowassa ambalo litazinduka hivi karibuni, wahariri wake wakiwa ni vijana wa Lowassa wa siku nyingi -- Deodatus Balile na Manyerere Jackton -- ambao amewaazima kutoka kwenye magazeti ya rafiki yake Rostam. Hii ni baada ya jarida la Lowassa la Umoja linaloendeshwa na Absalom Kibanda wa Tanzania Daima kufeli na mpaka kufikia hatua ya kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake.

6. Mwananchi

Kuna "mdudu" ameingia hivi karibuni kwenye gazeti pendwa la kila siku la Tanzania ambalo na gazeti hili nalo sasa linatumiwa kwenye mradi wa kumsafisha Lowassa. Hii ilijidhihirisha kwenye mkutanon wa juzi wa NEC ambapo habari kuu iliyotoka kwenye kikao cha NEC iliandikwa na mtu mmoja na kuchapishwa kwenye magazeti matatu -- Mwananchi, Tanzania Daima na Mtanzania -- neno kwa neno.

7. Daily News

Kaimu Mhariri Mkuu wa Daily News, Mkumbwa Ally, amejisalimisha kambi ya Lowassa ili athibitishwe na kupewa cheo kama Mhariri Mkuu wa magazeti ya serikali, TSN. Wakati huo huo, gazeti la Habari Leo lililo chini ya TSN limekuwa likipambana kuleta habari za ukweli kuhusu mafisadi. Hii imesababisha habari za Daily News na Habari Leo kuhusu kujivua gamba kutofautiana kabisa wakati yote ni magazeti ya serikali chini ya kampuni moja.

  • Mpaka hivi sasa, genge la kina Lowassa limejaribu na kushindwa kufanikiwa kwenye kila jitihada za kuyaingia au kuyamaliza kabisa magazeti mawili pekee yaliyosimama kidete kuueleza umma wa Tanzania ukweli. Nayo ni RAIA MWEMA na DIRA.

Kuna habari nyingi za aibu katika magazeti yote lakini hizo zisiyaponze magazeti kama taasisi. Magazeti yte yaliyotajwa tutakua hatuyatendei haki kwa kusema yamenunuliwa maana haiwezekani. Pengine mtoa mada angejadili habari husika kwa kila gazeti. Nakubaliana na hoja kwamba kwa sasa mafisadi wana nguvu kubwa sana, si ktk media tu, utakuta hata katika dola na ktk asasi nyingine hata za kidini. Inatisha sana, lakini ndio ukweli hata mahakama wamezishika na hii ni kwamba wameibaka serikali yote na mihimili mingine.. Mahakama na Bunge na mhimili wa nne nao kwishnehi... Tusilaumu magazeti, maana hata mtoa mada kesho anaweza kwenda kuendesha moja ya magazeti husika. Kuhusu MwanaHalisi, mafisadi hawaliamini maana huwa halitabiriki. Lolote linaweza kutokea... Japo hiyo dhana lazima iwepo, hasa baada ya hoja ya kuvua gamba ianze!!!
 
Back
Top Bottom