Mafuru wa VodaCom kuwa CEO mpya wa TTCL?

TTC is underperforming and one of the reason naamin ndani ya TTCL kuna "double agent" I belive in TTCL there are some decion makers wana sabotage hili shirika kwa manufaa ya kampuni nyingine shindani

If it is True hope Mafuru is not among them and will bring innovite ideas to keep TTCL ahead.

Mkuu kuna ukweli usiopingika katika hili. Celtel=Zain=Airtel ndo wamelifikisha pabaya shirika letu la simu. Wametumia miundo mbinu yao ikiwemo majengo na line zao nasikia bure kama si malipo kidogo sana na hujuma zingine kadha wa kadha.

Kwa upande wa Mafuru inawezekana kabisa kupata hicho cheo kwani "kingmaker RA " ni mdau huko Vodacom aliko Mafuru kwa sasa na mapendekezo yake huwa hayana kikwazo kwa JK.
 
Hivi hawa "Industrial Top Performers" hapa Tanzania "wanajulikana" kwa vigezo vipi?

Hivi ni TTCL inaweza kuwa revamped over-night na "kichwa" kimoja?

TTCL CEO anateuliwa na Rais wa Tanzania so the issue of "short-listing" is just a formality
 
Wanaoifanya TTCL ishindwe kufanya kazi kwa UFANISI ndiyo majority share holders kwenye makampuni ya simu za mkononi (Zain & Vodacom), na kama hiyo haitoshi Bodi ya TTCL inaenda kufanya "secret shopping" kutoka huko huko!
 
Inawezekana,cha msingi ni kama sifa zote zinazohitajika anazo,asipendelewe,haki itendeke!!!
 
Kumekuwa na threads nyingi zinazoonyesha kwamba Mafuru anawekewa njia kuwa CEO wa shirika moja la Umma. Ninachofahamu ni kwamba kama mkuu wa masoko wa Vodacom tulitarajia kuona amefanya kazi nzuri katika ushindani huu wa Mobile services Operators.

Performance ya Vodacom imekuwa ikidorora kutoka mwaka hadi mwaka. Na yafuatayo na matokeo ya Vodacom kwa miaka mitatu kwa faida kabla ya kodi.

Mwaka unaoishia:
31.03.2008 = Shs 54 billion
31.03.2009 = Shs 55 billion
31.03.210= hasara 9 billion

Mafuru ameshindwa kuweka mikakati mahususi ya masoko kuiwezesha vodacom ku- compete na tigO na Zain. Nadhani ameanza kujipendekeza kwa JK ili ahamie kwenye siasa maana pale alipo amekalia kuti kavu.

Kwa kweli hawezi kuleta Tija. Nadhani jambo la msingi ni kwamba akaajiriwe na H Lundega aendelee kumsaidia kusaka vidosho wa miss tz mitaani, namaanisha wale mabinti wanaopenda kuanika mapaja yao nje.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni..... nadhani kama elimu yangu ya darasani imenisaidia basi wa kulaumiwa mkubwa pale kampuni inapota hasara ni yule anayejihusishwa na maswala ya fedha na yule kiongozi mkuu maarufu kama MD au CEO..
 
We bwana una ugomvi binafsi na Mafuru?

Huo ni mtazamo wako. Sie tunataka mtu mwenye uwezo anayeweza kuchangia mafanikio ya shirika. Kama mkuu wa masoko ameshindwa kuwa mbunifu kuchangia mafanikio ya kampuni yake. Hawezi kutufaa kuwa MD wa shirika la umma. Kwanza anayejua qualifications zake, azimwage hapa!!!
 
we bwana acha uhuni huo, huo ugomvi wako na watu binafsi utuondolee hapa. Leta mambo ya maendeleo na mustakabali wa nchi yetu sio unafyatuka na madata yako uongo kwamba vodacom inapata hasara kwa sababu ya marketing manager.

Kanza hizo takwimu ambazo hazina miguu au kichwa umezitoa wapi? hata hazileti maana kutafsiri ya financial position ya kampuni. Tutolee hapa agenda za kijinga
 
Watanzania tunapigana vita wenyewe kwa wenyewe huku wageni wakiachiwa mashirika kuchota watakavyo.

Acheni Watanzania washike hayo mashirika na wakishindwa tuwaondoe na kuleta wengine. Ifike mahali tutegemee vichwa vyetu badala ya kuletewa hao wanaoitwa wataalam kila siku.

Haya ya kutafutiana vimakosa vidogo vidogo haitatusaidia maana kila binadamu huko nyuma amewahi kufanya makosa tu. Kama Mafuru atachaguliwa itakuwa nzuri kwa TTCL. Na wengine pia tunaweza kuamua kusaidia. Sioni kwa nini shirika kama TTCL lizidiwe ngumu na makampuni kama VODACOM, ZAIN nk.
 
Mafuru ahusiki na maamuzi makubwa yeye ni Marketing zaidi!

Na performance ya kampuni haipimwi kwa kuangalia kampuni moja ungeziweka zote hapo halafu uangalie vigezo kama 5 hivi usiende tu kuangalia faida baada ya kodi labda kodi imeongezeka je? kwanza hizo data umepata wapi? hasara bilioni 9?
 
kama taratibu za ajira zitakua zimefuatwa ni halali kijana kupewa hiyo nafasi maana pia ni kijana mzuri kama ameweza kuvumilia miaka yote vodacom na kama mnavyojua vodacom ukilinganisha na makampuni mengine ya simu ndo inatoa misaada mingi ya kijamii kuliko yote.
INSHALAH Mwacheni akatusaidie pale TTCL maana tunahitaji vijana wenye mawazo mapya kama yeye na msianze habari za uswahiba.
Maslahi ya nchi mbele.


safiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mafuru deserves this position or any other demanding job!!! binafsi namkubali najua kuwa anaweza pia ni mpiganaji mzuri. Anapenda mabadiliko na maendeleo, si ajabu akawa ni mmoja wetu hapa JF!!!!!
 
kichwa kwa kuandaa miss vodacom tanzania au? nchi hii bana imeoza kabisa..Mafuru is not CEO material at all..at all

wengine humu JF mmeishakuwa POLLUTED na NEGATIVITY. Wekeni fikra zenu HURU muweze kuchambua mbivu na mbichi, pumba na mchele.
 
Back
Top Bottom