Mafuru wa VodaCom kuwa CEO mpya wa TTCL?

utendaji wa kazi katika shirika lolote lenye mkono wa serikali ni mgumu sana kwa sababu za miingiliano ya maamuzi ya kitendaji na maamuzi ya kisiasa.pia maamuzi mengi huchukua muda mrefu kupitishwa ukizingatia wajumbe wa bodi wanakuwa na majukumu mengi na wameteuliwa kwa upendeleo
Hata Kama Ephraim atafanikiwa kupata u CEO hapo TTCL ajiandae kupambana na vikwazo vya urasimu tofauti na Vodacom alipozoea
 
Aliyekuwa, Vodacom's Marketing Director, Ephraim Mafuru anatarajiwa wakati wowote kuteuliwa MD mpya, wa TTCL. Well placed source inatutaarifu Kwa sasa Mafuru amejiuzulu nafasi yake ndani ya Vodacom Tanzania.
 
Kama ni kweli, nakupa pongezi sana kijana wa pod (Pugu)-Efraim Mafuru. Kila la heri, hukula mihogo ya mzee wa shamba bure.

All the best.
 
hii thread ilishawekwa hapa kwenye jukwaa la siasa na sasa imehamishiwa kule Business and economy..
 
Huyu ni mchagga ? vipi tena ule makakati wa kuwatosa umeishia wapi ?.
 
mbona nasikia anaenda bodi ya utalii? kuwa director wa marketing?
 
Sifahamu uweleo wa Mafuru kwenye kuongoza kampuni ambayo iko kwenye comma kama TTCL. Lakini nitachallenge wale wote ambao watasema kwamba jamaa hana vigezo sababu tuu ametoka Vodacom.

Swala kubwa ni moja tuu, jee jamaa ana njia gani za kuoka kampuni yenye decline revenue, with old technology and super high OPEX? Cash Flow ya TTCL ni msiba, high burden ya Labor Cost with benefit plans ambazo TTCL inachangia.

Unaweza kuleta product hata mia kwenye market lakini kama Opex zako zina outnumber revenue then profit margin will always shrink. Sasa bwana Mafuru analipi la kuleta kwenye msiba huu? I will be more than happy kujua.

Sababu kwa nchi kama Tanzania kutoa massive layoff ujue unatafuta ugomvi na watu, na bila kupunguza atleast 30% ya labor expense huwezi kushinda katika soko la ushindani, pili TTCL lazima waliquidate some of assets. Sell it to acquire some cash, then lazima wa develop new technology includes TV, DSL internet and cheap home phone.

Lazima wawekwe strong businss developer kwenye kila revenue unit. Government need to stay away from TTCL. ERP system ni lazima na kuchange organization structure ndio dawa......

I hope TTCL will return, imetusomesha wengine na kutuvisha for many years.
 
Nakubaliana na wewe, yaani nchi hii hata ujue vigezo vinavyotumika ni vipi na wakina nani kwenye hizo board wanaofanya hizo interview kama board zenyewe zinaundwa na vilaza hao hao wanaopewa kwa uswahiba. Hawa vijana bado kabisa hawajafikia viwango, nakubaliana kwamba watu watuambie hizo indicators na success stories za sio tu huyu lakini hao wangine wote wanoamini wanastahili nafasi hizi. Miss Tanzania has never been a sucess story, actually ningekua niko voda na ninamaamuzi nisingei associate brand/product yangu na hii beaty pagent ambayo haijawahi kuwa successful. Wako wenye uwezo Tanzania lakini hawaitwa kwa sababu hawajui kuuza sura kwenye media. Hivi voda kuna innovations gani zaidi ya ku translate msg za vodafone na kufanya matangazo yasiyo na uhalisia wowote wa soko, hebu kumbukeni lile la offer kwa masaa lilivyokuja kuuawa na tangazo la kibonde la celtel ingekua ni cocacola na Pepsi head of marketing, maana hakuwahi kuwa marketing director, na kundi zima lililohusika na hasara hiyo llingeenda. lakini kwa vigezo vya JK huyo ni mwenzao, wakowapi ma CEO waliowahi kufahamika kwa kugeuzi mashirika kuwa productive? yule mama wa habari aliishia wapi? au hizi ni za wanaume tu?
 
Tuache kuchanganya siasa na utendaji,mafuru ameifanya vodacom kuwa superbrand.Tigo na vodacom tigo imeanzishwa siku nyingi sana acha kubadili majina lakini mafuru toka akiwa meneja hadi mkurugenzi ameifanya vodacom kujulikana,kutafsiri mesiji za vodafone ni ubunifu pia.kwani hakuna leo product mpya katika makumpuni ya simu,zote copy paste.
 
kwa nchi hii huu nao ni udhaifu na ni mapungufu .. kwa mtu mwenye sifa na vast experience kama huyu bwana, badala ya kuanza kuwa na speculations za reccruitment destination.. kwanini asiwe emerging entrepreneur kwa kuanzisha consulting firm ya marketing trade leads za mobile phone companies au aspiring mobile phone operator as a native of TZ and get empowerment benefits from us the user/subscribers this would nave been a unique opportunity
 
Kitu gani unachoridhishwa na NHC? tuamie mwenzetu kama umeona lolote zaidi ya press releases ya CV za watendaji wakuu. Sisemi hawezi lakini nataka tumpe muda manaka bado hajafanya lolote. Deliverables za NHC si magazeti, wala presentation za strategic plans, ni ujenz wa affordable houses nyingi tu kwa watanzania na ukusanyaji wa kodi za majengo yao yasasa, kuvunja mikataba ya kinyonyaji iliyoingiwa na viongozi waliopita nk.
 
Namjua Mafuru tangu akiwa makamu wa rais DARUSO.Kuwa CEO wa TTCL bado maana yeye ni mtu wa Marketing pure kwa hiyo hana skills za utawala bado labda aende shule kido zaidi....
 
Back
Top Bottom