Mafundi wazuri wa Nissan Duals

Habari ndugu wana jamii forum,nimejikongoja kdg nimenunua nissan duals naombeni ushauri kuhusu mafundi wazuri maana hii gari naipenda sana japo watu wanadai ina changamoto nyingi ila kwa upande wangu naikubali sana hii gari
Hongera sana. Pale kwenye mafra kubwa kuja kwenye engine wapunguze Yale mapamba kwa pembeni. Pili usilioshe kwa presure ya maji. Hasa kwenye engine. Waoshe kawaida tu. Ikiwezekana engine wawe kama wanaifuta hivi badala ya kupiga maji mengi.

3. Hiyo senser ya mlango wa nyuma,ile switch ya kufungua buti isipigwe presure,inahifadhi maji yakipigwa kwa presure hii ni pamoja na Subaru nyingi.

4. Hiyo roof ya juu ya kufungua hivi usiichezeechezee inaweza kugomea upande iwe nyuma.

5. Hiyo roof ya minguo nguo hiyo pamoja na hiyo ya kwenye kiegemeo cha milango yote ukipata hela nenda kwa fundi rezer (fundi sit cover) akayang'oe hayo manguo,piga rezer kote ili baadae yasikukere

Hongera
 
Changamoto yakehizo gari over heating Kwa safari ndefu na kujiwakiamoto fundi wa kazi gani
 
Habari ndugu wana jamii forum,

Nimejikongoja kidogo nimenunua Nissan Duals naombeni ushauri kuhusu mafundi wazuri maana hii gari naipenda sana japo watu wanadai ina changamoto nyingi ila kwa upande wangu naikubali sana hii gari

Sio wa Ilala, Dar es salaam kila mtu ni fundi, Hata ukimpata tumia akili yako sana, mafundi wa kweli wachache sana
 
Dah mkuu asante sana kwa ushauri, umenifungua vtu muhim sana
Yale mapamba pembeni ya mafra yakioshwa oshwa yanalegea theni yanasogea pale kwenye mafra. Na pale pana joto Kali sana. Kwa hiyo ni rahisi kushika moto. Moto huwa unaanzia hapo kwa hizi Duas. Kwa hiyo ukiyapunguza yakabaki kwa mbali utakuwa umepungiza hatari ya hizi duas kuungua
 
Asante sana mkuu
 
Asante sana mkuu
Pia fundi wa gari unalotumia wewe ni wewe mwenyewe. Jitahidi sana kuizoea gari yako. Mfano ukikuta kitu kiko tofauti labda unavyowasha au unavyoendesha ukasikia mngurumo usio wa kawaida au unapoendesha ukakuta kuna mahala kama panagonga au pana mlio tofauti. Hapo ndio unaenda kwa fundi kujua nini tatizo. Na wewe ni fundi wa kwanza ksbb inatakiwa wewe ndio uwe wa kwanza kutambua tatizo,na kawaida iko hivyo. Kwa hiyo ukienda kwa fundi unamuelewasha tu wapi unapasikia pana shida.

Jifunze kupima tu oil asubuhi kabla hujaiwasha. Maana hizo gari zina kawaida ya kupunguza oil. Siku ya siku kama huna kawaida ya kupima utakuja kuendesha gari kumbe imekausha oil yote. Hayo ni mambo yanaanzia kwako sio kwa fundi.

Mfano mwingine gari unaendesha barabarani inang'ang'ania upande hapo unampigia simu fundi wako kujua ni nini?. Hapo fundi wa kwanza ni wewe kutambua gari haiendi sawa. Zoea kupima upepo tyre kila baada ya wiki 2. Haya ndio mambo ya mwanzo wewe kuyajua na kuzingatia kwenye gari. Karibu
 
Habari ndugu wana jamii forum,

Nimejikongoja kidogo nimenunua Nissan Duals naombeni ushauri kuhusu mafundi wazuri maana hii gari naipenda sana japo watu wanadai ina changamoto nyingi ila kwa upande wangu naikubali sana hii gari

Kuna jamaa wanjiita ‘MR. IST’ unaweza ukawapata instagram. Siwajui personally lakini naona wamefamya kwa muda sasa kazi za dualis na xtrail, wana spare pia na oil n.k.
Ukiwapata bila shaka watakupa na ushauri mwingine wa jinsi ya kutumza hiyo gari.
Ila kwa haraka haraka make sure engine na gearbox zinapata oil sahihi kwa ajili ya hiyo gari na kwa wakati sahihi, service kwa wakati na make sure coolant level iko sawa kila wakati. Usiende kwa kila fundi
 
Back
Top Bottom