wajingawatu
JF-Expert Member
- Jan 20, 2013
- 2,048
- 2,442
Kila kitu kikitumiwa kwa wingi kina madhara na siyo sukari tu.
Mkuu Zogwale Sukari ina madhara lakini
Asali haina madhara sukari iliyoko ndani ya Asali ni Natural Pollen sugar haina Madhara kwa binadamu ni Dawa
na ni Tiba kwa Afya ya Binadamu hata kama utakuw unakunywa kila siku Asali haita kudhuru sana itakuongezea nguvu za kiume katika mwili wako na kukutibu baadhi ya magonjwa yaliko mwilini mwako. Hizi hapa chini ni baadhi ya Faida ya kutumia asali.
Asali ina manufaa mengi mojawapo ikiwa ni kusaidia kupunguza uzito. Mtumiaji huweka kijiko kikubwa kimoja ndani ya maji ya moto na kunywa kila siku asubuhi. Hii pia humsaidia kupunguza kitambi.
Pili, asali husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Mtumiaji anaweza kunywa kijiko kikubwa kimoja asubuhi, mchana na jioni. Kama hiyo haitoshi, asali pia - hasa ile ya nyuki wadogo - wakubwahusaidia kutibu kikohozi kwa watoto na.Wakubwa.
Wakati mwingine baadhi ya watumiaji huchanganya na kiini cha yai na kutengeneza mkorogo unaonyeshwa watoto. Kumbuka kuwa ni vema mkorogo huo ukatumika siku hiyo hiyo.
Pamoja na matumizi hayo, asali pia husaidia pale inapotokea mtu ameungua kwa moto. Basi ni vema ikapakwa mara moja wakati mgonjwa akielekea hospitali kwa matibabu zaidi. Waweza pia kupaka na yai bichi lililovunjwa kama unalo.
Kwa ndugu zangu akina dada na akina mama, asali pia hutumika kwa ajili ya kufanyia steaming ya nywele. Ukienda nayo saloon wataalamu watakusaidia bila kusahau kuongeza mng'aro wa ngozi ya mtumiaji iwapo anatumia.
Labda niseme kuwa katika nyakati za hivi karibuni kumekuwa na tatizo sana la kisukari linaloathiri nguvukazi ya taifa. Tatizo hili
pia linaweza kuepukwa kwa kiwango fulani kwa mtumiaji wa chai na kahawa, kuweka asali badala ya sukari katika vinywaji hivyo.
Vile vile badala ya kupaka jamu kwenye mkate, kwa wenzangu wenye shida ya uzito mkubwa waweza kuweka
asali. Kumbuka si tu utaburudika bali pia unatibu shida za kiafya. Ikumbukwe kuwa matumizi makubwa ya sukari hayana tija sana kwa mwili, hivyo ni bora kukinga kuliko tiba kwa sababu ni ghali.
Hivyo basi, ni vema wanafamilia mkajitahidi kuhakikisha kuwa mnakaa na asali nyumbani kama huduma ya kwanza. Asali inayopatikana katika maduka mbalimbali au katika vibanda maalumu vya uuzaji asali pia inafaa.
Mkuu.@Zogwle Kuamsha tamaa ya kiume au kikeAsante sana Dr. MziziMkavu,
Kwa hakika matumizi ya asali nayakubali na huwa ninatumia japo si kila wakati (si unajua tena sisi ambao tumefikia saa 10 jioni). Je kwa wanawake haisaidi katika kuongeza nguvu ya yale mambo ya wakubwa? maana na wao si unajua tena wakifikia 40s wanaanza ile law of diminishing return!!! Au kuna njia nyingine natural kwa wanawake? Angalao kwa mamen inakuwa ni kama nuts, asali, etc.
Mkuu.@Zogwle Kuamsha tamaa ya kiume au kike
Juisi ya tangawizi nusu kijiko pamoja na yai nusu iliochemshwa na asali. Tumia kila siku kwa muda wa mwezi mmoja.
As Usual respect to U.....
Tunaomba na madhara ya chumvi nayo utuletee mkuu. Siku njema....
Ni kijiji gani unachokiongelea mkuu,isije ikawa unaongelea mabwe pande?Vema kabisa mkuu,sukari sio kitu cha lazima kwetu. Mi nashangaa hii kuwa ajenda wakati wengi huko vjijini wanatumia chumvi kama mbadala wa sukari,kama vile kwenye uji.
Vema kabisa mkuu,sukari sio kitu cha lazima kwetu. Mi nashangaa hii kuwa ajenda wakati wengi huko vjijini wanatumia chumvi kama mbadala wa sukari,kama vile kwenye uji.
Ni kijiji gani unachokiongelea mkuu,isije ikawa unaongelea mabwe pande?
Hizo ni sababu mufilisi kabisa tafuta utetezi mwingine huu bado haukidhiKwani mkuu wee unaamini kwamba bila sukari ya miwa huweza kuishi? Hiyo tu ndo inakufanya upumue? Ukinywa uji bila hata kuweka chumvi au hiyo sukari miwa mwili haupati sukari yake kama kawaida?
Hizo ni sababu mufilisi kabisa tafuta utetezi mwingine huu bado haukidhi