Kamata kamata ya sukari itaongeza tatizo kwa walaji, chonde Serikali acheni hii kitu

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,458
Nimesikitika sana asubuhi kusikia viongozi wanajitamba kuwakamata wafanyabiashara wanaouza sukari bei juu...😜😁😁Nachrka kwa dharau.

Unamkamata muha,mangi mwenye kirobba cha kg 25 kanunua 100,000 unataka uauzeje sukari? Yeye kanunua duka la jumla, kosa lake ni nini? Yeye hana kiwanda, kwanini msipambane na wasambazaji wakubwa?

Madhara Haya sasa
Ili kukwepa kukamatwa inabidi hawa wafanyabiashara wadogo wafiche sukari waliyonayo kwa wakati huo kwa hofu ya kukamatwa wawauzie wanaowajua tu.

Hujaongeza tatizo hapo?

Akimaliza kiroba chake je atathubutu kununua tena?

Sukari haijapanda zaidi?

Kila mfanyabiashara ataogopa kununua na mwishowe walaji ndio watakoteseka siyo msambazaji wala mfanyabiashara.

Serikali iache swala hili kama ina nia nzuri ilete sukari ya kutosha iingizwe mtanaani na walioficha watapata hasara lakini kufanya operesheni ni kuongeza tatizo.
 
Huko mtwara wameuziwa sukari ya bei elekezi, wao wanapandisha makusudi,
Wafungwe tu
 
Hao wadogo bora wasiuze ili wasambazaji iwadodee na ikiwadodea watapunguza tu bei,kuhusu sisi wananchi usiwe na hofu tumeshachukuliana na hali.
Kwa sisi tunaogemea kwa ajili ya juisi na lamba lamba tule wapi?
 
Hao wadogo bora wasiuze ili wasambazaji iwadodee na ikiwadodea watapunguza tu bei,kuhusu sisi wananchi usiwe na hofu tumeshachukuliana na hali.

Ndomana nasemaga,watu wapunguze matumizi ya sukari

Hao wenye viwanda na wasambazaji wakubwa wenyewe watalegea

Wanachofanya hawa mabonyenye wa sukari ni kuwafanya walaji wa sukari kama watumwa,mateja

Watu wana addiction ya sukari bila wao kujijua

ova
 
Back
Top Bottom