Madereva na Makondakta wawe na kauli nzuri kwa abiria wao

Chulumeshy

Member
Jul 27, 2022
17
11
Nalia na madereva pamoja na makondakta wao kwa kauli zao zinazokera wanazozitumia kwa abiria wao. Imekuwa ni changamoto kubwa hususani kwa makondakta wa daladala zinazoelekea maeneo yenye watu wengi maarufu kama ''Uswahilini'' kama vile Manzese, Mbagala, na sehemu nyingine.

''Ungekuwa na haraka ungepanda uber''

''Ungekuwa na haraka ungepanda tokea jana'' na kauli nyingine ambazo zimeambatana na lugha yenye maneno makali yaani matusi.

Na hii imetokana na changamoto za hapa na pale hususani nyakati za asubuhi watu wanapoelekea makazini na wakati wa jioni watu wanaporudi makazini. Pamoja na hayo changamoto ya makomdakta kutumia lugha chafu ni pale unapokuta daladala limejaa lakini kutokana na kutaka kukamilisha hesabu hulazimisha gari kuwa kama ''Mkunguwa ndizi'' yaani kuwabananisha watu kwa madai ya kwamba ''Daladala Haijai''. Na hii hupelekea abiria kuzozana na makondakta kwa kuchukia kubanwa na harufu mbalimbali za mchanganyiko na mbanano wa watu kwenye daladala.

Hivyo basi, changamoto hii imepelekea ugomvi baina ya abiria, madereva na makondakta na muda mwingine huibua mapigano makali yanayoweza kuamuliwa na Askari wa Usalama Barabarani na hata kupelekwa mbali zaidi katika vyombo vya sheria pale mmoja wapo anapohitaji zaidi kudai haki yake.

Ushauri wangu
Nichukue nafasi ii kuwashauri makondakta na madereva kutumia lugha nzuri kwa abiria wao kwani hii italeta maelewano mazuri na amani katika safari. Sambamba na hilo napenda kuwashauri abiria nao kutumia lugha nzuri pamoja na kukubali kujishusha pale wanapokosea na hii itapelekea kuepukwa kwa baadhi ya migogoro inayoweza kuepukikwa. Mwisho, niwapongeze Askari wa barabani kwa kazi yenu kubwa katika kutatua changamoto baadhi ila pia nipende kuwaomba kutenda haki ili kuijenga Tanzania yenye Amani kwa wananchi wote.

JE, WEWE UMEKUTANA NA CHANGAMOTO GANI BARABARANI?
 
Dawa ya yote haya ni kuwa na good running public transport!just imagine jiji letu lingerie na metro trains zinaanzia pale central na kuelekea sehemu mbalimbali za jiji, why ujenzi wa barabara za mwendokasi haukuenda sambamba na ujenzi wa trains?tuendelee kula mtori nyama zipo chini
 
Back
Top Bottom