Serikali piga marufuku mrundikano wa abiria kwenye Daladala

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
315
878
Yaani kuishi nchi hii ya Tanzania imekuwa nongwa sana, kila eneo wafanyabishara wanajiamlia kufanya yao.
Waendesha daladala wanapakia abilia hadi mlangoni, watu wanasimamiahwa na kupangwa kama magunia ya mikaa.

Kwani serikali hatuwezi kufanya hata hili la usafiri kwa kuzingatia level seat nchi zingine zikaja kujifunza hapa kwetu Tanzania?

Cha kufanya serikali toa tamko kwa nchi nzima hakuna abiria kusimama kwenye chombo cha usafiri hasa daladala maana najua angalau kwenye vyombo vingine vya usafiri wa masafa marefu wanazingatia level seat.

Yaani mimi huwa nashangaa Trafiki wa Tanzania anasimamisha gari ndogo mfano Harrier au Juke nakuanza kuizunguka zunguka kukagua huku akiiacha daladala inampita mbele yake ikiwa imejaza abiria hadi mlangoni na ilhali wakijua hiki ni kichume na sheria za usafirishaji.

Serikali toa tamko kwamba Trafiki ashushe abiria yoyote aliyepanda daladala kwa kusimama, hiyo ndiyo iwe adhabu yake huku konda na dereva walioruhusu abiria kusimamia kwenye gari yao wakipigwa faini ya Tshs 30000.
Hii itasababisha abiria, konda na madereva kuheshimu sheria na usalama barabarani.

Hivi kwa ujazaji wa abiria wakiwa wamesimama hadi milangoni, tulishajiuliza endapo daladala hiyo inapata ajali hivi hao abiria walio simama watakuwa na hali gani? Au ndo kusema serikali itakuja na salam za pole kwa wananchi walioondokewa na wao.

Lakini pia serikali kupitia mkurugenzi wa halmashauri waone umuhimu wa kuwapunguzia tozo haya magari yanatoa huduma za daladala kwa wananchi wa Tanzania kwa sababu inawezekana wanajaza ivyo abiria ili wapate pesa za kulipa kodi za TRA na Tozo za halmashauri.

Lakini pia serikali ione umuhimu wa kupunguza kodi za forodha za uingizaji magari ya abiria ili wawekezaji waingize magari mengi ya abiria kwa ajili ya ku_accomodate the excess supply ya abiria inayochangiwa sana na ukuaji wa miji yetu na uzalianaji mkubwa kunakopelekea uongezekaji mkubwa wa idadi ya watu Tanzania.
 
Serikali badala ya kupunguza kodi ya gari za abiria watu wasafiri na Quantum bila kuchoka wao wapo busy na hivi vipanki wanaona navyo ni usafiri kabisa huko gari za shule ndio kichekesho aisee utadhani tumerogwa kwamba hatuhitaji jamii yetu itukie vitu bora.

Punguzeni kodi wafanyabiashara walete gari za ukweli za abiria watu waone faida ya Bandari kuwa Tanzania sio magari mazuri yanaenda Nchi jirani tu na ninyi mnabaki kujisifia Ujinga.
 
Serikali yenyewe imeshindwa kusimamia dala dala zake (Mwendokasi) then unataka Serikali hiyo hiyo isimamie dala dala za watu binafsi??!!
 
Serikali badala ya kupunguza kodi ya gari za abiria watu wasafiri na Quantum bila kuchoka wao wapo busy na hivi vipanki wanaona navyo ni usafiri kabisa huko gari za shule ndio kichekesho aisee utadhani tumerogwa kwamba hatuhitaji jamii yetu itukie vitu bora...
Punguzeni kodi wafanyabiashara walete gari za ukweli za abiria watu waone faida ya Bandari kuwa Tanzania sio magari mazuri yanaenda Nchi jirani tu na ninyi mnabaki kujisifia Ujinga..
Naungana na wewe kabisa ndugu yangu yaani serikali hii inaamini mwananchi kutumia vitu bora hiyo ni anasa kwake
 
tata inabeba abiria waliokaa na waliosimama 80-90 badala ya 45, kwa kila route hesabu inatakiwe iwe na gari mara 2 ya ziluzopo,unafikiri hali ya jiji itakuwaje!

na vipi uwekezaji husika utakuwa unalipa kama ilivyo sasa??maana itatakiwa gari liishi miaka 6 na zaidi kumlipa aliyelinunua.

halafu hiyo sio ajabu hata nchi za watu ipo sana, usafiri wa umma ni wa wengi hauwezi kuwa na standard nje ya economy.

labda tukomae ktk usalama wa hali za magari husika,gari ambazo zina handle hali hiyo ni hizo tata,eicher nyingu zimechoka sana.
 
Kujazana kwenye daladala hadi wengine kuning'inia mlangoni ni kiherehere cha abiria wenyewe. Kwani ukiona gari haina sehemu ya kukaa ukaacha kupanda kondakta atakubeba akutupie ndani?
Watu wanaishi kimazoea na wengi wa watu wameathiriwa na umaskini mzito. Maskini hana chaguzi lililo bora
 
Watu wanaishi kimazoea na wengi wa watu wameathiriwa na umaskini mzito. Maskini hana chaguzi lililo bora
Wakati wa Covid serikali ilipiga marufuku abiria kusimama ndani ya daladala, watu waliendelea kujazana kwenye daladala licha ya kuwa ni afya zao ndio zinapiganiwa. Walikuwa wanasimama wakiona polisi wanachuchumalishwa kwenye daladala.

Watanzania wenyewe sisi ndio tatizo, gari imejaa lakini mtu anapanda ili abembee mlangoni.
 
Sijui mwendokasi itakuwaje maana abiria tayari wanazo tikiti mkononi mabasi yanawaonea aibu yanajificha ndani ya vichuguu.
 
Nchi haiendeshwi kwa matamko ya serikali.

Uchumi wa nchi unaendeshwa kwa nguvu za uchumi za demand and supply.

Ndiyo maana serikali inaweza kuweka bei elekezi ya sukari, halafu watu wakauza kwa bei zaidi. Na serikali ikikomaa kulazimisha bei elekezi ambayo haina faida kwa wazalishaji na wafanyabiashara, wazalishaji na wafanyabiashara hao wataacha kuuza bidhaa.

Ukiwa na mji wenye level seat, kwa maana ya idadi ya watu iliyo standard, na magari standard, hutakuwa na tatizo la watu kujazana kwenye mabasi.

Sasa wewe una mji watu wamejazana pomoni, mpaka mabondeni huko kwenye mito, unataka wakae level seat kwenye mabasi?

Miaka ya sabini kurudi nyuma wakati Dar haijafikia watu milioni moja kulikuwa hakuna daladala lakini pia watu hawakujazana sana kwenye mabasi, kwa sababu mji haukuwa na watu wengi sana.

Mji ulikuwa una mpaka magari ya kukusanya takataka, magari ya Halmashauri ya Jiji Dar es salaam.

Sasa, unataka watu wakae level seat wakati mji wenyewe haujakaa level seat?

Haya matatizo ya watu kujazana kwenye vyombo vya usafiri yapo mpaka New York, Tokyo na London.

Ni matatizo ya miji mikubwa yenye watu wengi waliolundikana pamoja.

Na kwa Dar, bila kutengeneza miundombinu iwe bora zaidi, bila mpango madhubuti wa kuboresha usafiri wa umma, tegemea hilo tatizo lizidi. Dar inaenda ku double idadi ya watu katika muda mfupi sana ujao kuliko wengi wanavyofikiria. Dar ni moja kati ya miji inayokua kwa kasi sana Afrika.
 
Nchi haiendeshwi kwa matamko ya serikali.

Uchumi wa nchi unaendeshwa kwa nguvu za uchumi za demand and supply.

Ndiyo maana serikali inaweza kuweka bei elekezi ya sukari, halafu watu wakauza kwa bei zaidi. Na serikaki ikikomaa kulazimisha bei elekezi ambayo haina faidw, wafanyabiashara wataacha kuuza bidhaa.

Ukiwa na mji wenye level seat, kwa maana ya idadi ya watu ikiyo standard, na magari standard, hutakuwa na tatizo la watu kujazana kwenye mabasi.

Miaka ya sabini.kurudi nyuma wakati Dar haijafikia watu milioni moja kulikuwa hakuna daladala lakini pia watu hawakujazana sana kwenye mabasi, kwa sababu mji haukuwa na watu wengi sana.

Mji ulikuwa una mpaka magari ya kukusanya takataka, magari ya Halmashauri ya Jiji Dar es salaam.

Sasa, unataka watu wakae level seat wakati mji wenyewe haujakaa level seat?

Haya matatizo ya watu kujazana kwenye vyombo vya usafiri yapo mpaka New York, Tokyo na London.

Ni matatizo ya miji mikubwa yenye watu wengi waliolundikana pamoja.

Na kwa Dar, bila kutengeneza miundombinu iwe bira zaidi, bilq mpango madhubuti wa kuboresha usafiri wa umma, tegemea hilo tatizo lizidi. Dar inaenda ku double idadi ya watu katika muda mfupi sana ujao kuliko unavyofikiria. Dar ni moja kati ya miji inayokua kwa kasi sana Afrika.
Lakini kwa nini Tanzania kwenye issue za ustawi wa jamii iko nyuma sana?
 
Lakini kwa nini Tanzania kwenye issue za ustawi wa jamii iko nyuma sana?
Ukisema ustawi wa jamii unamaanisha nini kwenye muktadha wako? Unaweza kufafanua kidogo?

Ustawi wa jamii kiujumla ni matokeo ya uchumi na elimu.

Kama una matatizo ya elimu na uchumi, mambo ya ustawi wa jamii kuwa mazuri ni vigumu sana.
 
Naungana na wewe kabisa ndugu yangu yaani serikali hii inaamini mwananchi kutumia vitu bora hiyo ni anasa kwake
Watu mpaka kesho wapo busy kufua nguo kwa mikono wakati hizo mashine za kufua hata hazina bei kubwa shida ni hiyo kodi yake pana ndugu yangu mmoja nilimpa zawadi ya mashine ya kuosha vyombo yeye alijua nimenunua bei kubwa kumbe hata laki mbili na nusu haikufika baadae nikamwambia hazina bei hizo alishangaa sana na anapiga nayo kazi tuu kwetu kutumia vitu kama Wazambia ni anasa au wengine wanadhani ni pesa nyingi kumbe huko kwenye masoko wanauza bei za kutupa hizo TV smart za ukweli kwa Tanzania bado ni anasa kwa bei yake na matoleo ya zamani...
 
Back
Top Bottom