Madereva wa magari ya abiria kushuka na kuacha gari kwenye foleni kuna hatarisha usalama wa abiria

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
356
550
Kumekuwa na Trends siku hizi Madereva hasa hawa wa Daladala wakifika sehemu kuna taa au Foleni huwa wanashuka na kujizugisha zugisha au kulizunguka Gari akisubiri foleni itembee.

Hichi Kitendo ni kibaya na kinahatarisha usalama wa Abiria, Ikitokea Gari inakuja imefeli breki au kukosa uelekeo Dereva aliyeshuka kwanza anakuwa hatarini mwenyewe, pia atakosa nafasi ya kuondoa Gari yake kwa haraka na kuikwepa yenye tatizo, hivyo anayaweka hatarini maisha ya Abiria wake kwa uzembe.

Kama Abiria unashauriwa kujali usalama wako unapokuwa kwenye Chombo cha moto, usichochee sifa za Dereva, uzembe wake, wala usumbufu na Madereva wengine Barabarani. Kuwa Mkali ufike salama usiruhusu Dereva akupoteze uwahi kwa Uzembe wake.

1693979776055.png
 
Tunafanya hivyo kwa ajili ya kufanya mazoezi na kujinyoosha viungo vyetu vya mwili, migongo na viuno vinachoka sana, mtuhurumie kazi ya udereva ni ngumu sana. Pia ni kwa ajili ya usalama wenu sababu Kuna wakati misuli inakaza. Kuwa mpole mkuu na jaribu kuwa muelewa.
 
View attachment 2740571
Wanafanya hivyo kupunguza uchovu wa kukaa kwenye kiti kutwa nzima, bila kufanya hivyo anaweza akasinzia na kuwatumbukiza kwenye mtaro.
 
Uliwahi kuona dereva wa Basi la Mkoni kajinyoosha? au Dereva wa gari ndogo au wa Lori? why wa daladala pekee? na kwanini wasisimame kituoni kujinyoosha?
 
Wanafanya hivyo kupunguza uchovu wa kukaa kwenye kiti kutwa nzima, bila kufanya hivyo anaweza akasinzia na kuwatumbukiza kwenye mtaro.
Basi afanye hivyo mahala ambapo ni salama kwa kuepusha ajali zisizotarajiwa kwa uzembe
 
Hata akibaki ndani ya gari atafanya nini au ataipeleka wapi gari wakati umeshasema yupo kwenye foleni
Kuna Namna zinaweza chukuliwa hatua ambazo zitapunguza Imact.. Mfano wewe gari yako ndo ya mbele mean ikitokea hitilafu wewe ndio unaanza kupata madhara lakini pale una nafasi ya kuepuka hitilafu hiyo
 
Kitu kizuri n kua yule ambaye gari yake ni ya mbele huwa hawashuki maana muda wowote wakiruhusiwa yeye ndio anatakiwa kuondoka.

Hawa wa katikati ndio huwa wanashuka na wanashuka kujinyoosha na kupunguza uchovu/usingizi sio jambo baya
 
Swali zuri sana, Lakini kuwa nje ya gari risk ni kubwa sana tofauti na ukiwa ndani utatafuta namna. wewe kama abiria upo tayari kuachwa?
Sikubaliani na kuachwa ila ikitokea kuna hali kama niliyohoji dereva hana cha kufanya ikiwa kuna foleni.
 
Hawajali maana madereva wa daladala wana ushirikiano mzuri
Na matrafik police,kumbuka daladala hizo daily wanatoa hela kwa traffic police

Ova
 
Back
Top Bottom