Madaktari Sawa Watatoka Cuba, India na China. Manesi Je?

Serikali makini haijidanganyi kwa kuwa na mipango ya dharura ambayo inaharibu bajeti ya Nchi
bali inakua makini kwenye kutatua matatizo hayo kiumakini
umeme wa Dharura umechukua kipindi kizima cha urais wa jk na sasa madaktari wa dharura kama
wataletwa sijui itakuaje "Mungu ibariki TANZANIA,Mungu ibariki Afrika"
Hapa kuna kitu nimekumbuka,Umeme wa Dharura Former PM sasa Madaktari wa Dharura!, Haya yangu macho!
 
Manesi watatoka Bangladeshi.. Vietnam na Guatemala.. MAJIBU RAHISI KWENYE MASWALI MAGUMU..
 
Hawa madaktari waliogoma imekula kwao kudadadeki. Hizo mil. 3 wanazotaka watazisikia kwenye radio sasa.
Wewe unategemea hao watakaoletwa watalipwa chini ya Mil.3! U must be joking...hawa watalipwa double the salary ya daktari wa Tz... Isitoshe watawaletea Medical Assistants na si Doctors ndipo mtalia na kusaga meno. Huu ushabiki usio na faida kwa taifa wakati mwingine tuuepuke
 
Nani kakwambia hawagomi eti kwa sababu ni watu makini? Ni kwa sababu hata wakigoma impact ya mgomo wao haitaonekana directly and immediately kama madaktari. Mgomo wao hauna nguvu kama wa madaktari. Na kwa mtazamo wa serikali yetu ya sasa, wala haitajihangaisha nao, watakaribisha njaa majumbani mwao tu! Wewe unadhani wanasheria wakigoma shinikizo kwa serikali (yetu) litatoka wapi wakati hata hizo kesi za serikali zenyewe nyingi serikali (jamhuri)inaishia kushindwa? Walimu wakigoma serikali itapata faida kwa kuwa wajinga wataongezeka ili iwaburuze vizuri... Usijidanganye eti hawagomi kwa kuwa ni watu makini, ni kwa sababu wanajua hawana karata za maana kuitishia serikali (yetu).
Well said Mkuu! Na hiyo kureplace madaktari hasa wale wa MNH ni impossible! Zamani waliweza kwani waliokuwa wanagoma ni Interns pekee, safari hii ni kuanzia interns, Registrars, Residents, Specialists hadi maconsultants!
Shughuli pevu!
 
Walikuwa wanadai Mawaziri wajiuzulu. Yaani Madaktari bwana thehe thehe thehe, kwa hiyo wasipojiuzulu watoto wa Madaktwari haya hawatakwenda choo? Kazi kweli kweli. Daktari acheni hizo bwana. Mnajua kazi yenu kama kazi nyingine tu. Hivi Daktari ukipewa kazi ya kutengeneza hata stuli utaweza kweli? ukiambiwa umfundishe mtoto wa miaka mitatu hadi ajue kusoma utaweza? ukiambiwa kazi yako ni kuimba kwenye jukwaa ili watoto wako wapate kula utaweza? ukiambiwa ukatembee na viatu unauza mitaani kutoka Igoma hadi Nyakato, Ghana hadi Kirumba utaweza kweli Daktari? Basi hivyo wenzenu tunavyoteseka kuhakikisha familia zetu zinaishi. Kazi yenu kama kazi zingine

Haya basi goma wewe mtengeneza stuli uone kama hata filimbi itapigwa! Wakigoma watu wa daladala hampigi kelele, leo wamegoma madaktari walioenda shule, wenye shule za kuuunga unga mnapiga kelele kwa kujua wao wana thamani.
 
Hawa madaktari waliogoma imekula kwao kudadadeki. Hizo mil. 3 wanazotaka watazisikia kwenye radio sasa.

You are not serious, hivi unadhani kwa umaskini wetu nisahihi kwa serikali kuagiza madaktari toka nje, kwa economic growth ganituliyonayo? Usidhani ni ma dr pekee ndio watazisikia 3m redioni, hata wewe kamau mfanyakazi wa serikali beware mana mshahara utapata tarehe 45!!!!! Hili sioswala la kuangalia kwa sasa angalia future yake ikoje! Impact yote itakuwa kwawalalahoi mana kuna sehemu watapunguza budget waweze kuwalipa hao madaktari.Kitu kingine jiulize kuhusu mazingira ya hospitali zetu ambazo sometimes hatagloves zinakuwa issue, je hao madaktari ambao kwao mazingira ni superb watawezakufanya kazi kwenye mazingira magumu au ndio kuitaka serikali wanunue vifaa nakuboresha mazingira yao ya kufanya kazi, sasa sio kuruka mkojo na kukanyaga mavi,kwamba bora muwasikilize madaktari wazalendo mmalizane nao!! Hili swala sio lamzaha jamani!!!
 
Mpango wa dharura nchn (kuleta madaktar kutoka nch za watu)teheteh nacheka kama mazur>Mungu ibariki tanzania
 
Serikali inabidi ianze kuandaa back up plan kidogo kidogo kwa kuanzia tunaweza kuanza na kuchukua volunteers au interns za wa nje kwenye exchange programs. Ili in the future migomo kama hii inatatuliwa fasta bila wananchi kupata shida.
 
Walikuwa wanadai Mawaziri wajiuzulu. Yaani Madaktari bwana thehe thehe thehe, kwa hiyo wasipojiuzulu watoto wa Madaktwari haya hawatakwenda choo? Kazi kweli kweli. Daktari acheni hizo bwana. Mnajua kazi yenu kama kazi nyingine tu. Hivi Daktari ukipewa kazi ya kutengeneza hata stuli utaweza kweli? ukiambiwa umfundishe mtoto wa miaka mitatu hadi ajue kusoma utaweza? ukiambiwa kazi yako ni kuimba kwenye jukwaa ili watoto wako wapate kula utaweza? ukiambiwa ukatembee na viatu unauza mitaani kutoka Igoma hadi Nyakato, Ghana hadi Kirumba utaweza kweli Daktari? Basi hivyo wenzenu tunavyoteseka kuhakikisha familia zetu zinaishi. Kazi yenu kama kazi zingine

Udaktari kazi ya kawaida...hahaaa na wewe kasomee udaktari basi ugome......
 
La msingi ni kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya mdaktari na watumishi wote kwenye sekta nyingine. Nchi nyingi zinazofanya vizuri katika tawala zao zinaji wajibisha na uboreshaji wa utendaji kazi wa sekta zake za huduma na sio kuziacha zinatapatapa na kujiingiza na migomo. Utumishi wa umma inao wajibu wa kuhakikisha hili linafanyika. Mikataba ya kazi na masharti ya utumishi iwe wazi ikikubaliwa na pande husika itekelezwe.
Hata wakija watu kutoka nje watahitaji mikataba iliyo wazi. Madaktari watupende ili tuwe nao kwenye hili suala la kuwekewa mazingira mazuri ya kazi wasituumize kwani hao walio usingizini hawatibiwi hapa nchini. Rais ajue hana watu anatakiwa asafishe safu zote. Walimu, wauguzi, na kwa kweli watumishi takriban wote. Mazoezi yaliyofanyika miaka ya nyuma yalilenga
kupunguza ukubwa wa wingi wa watumishi serikalini ili kuongeza ufanisi. Yanayojitokeza ni kwamba walioondolewa serikalini ndio bora kuliko waliobaki ambao kila siku wanavuruga mambo. Kuna watu walikuwa sawa na makamusi ya taratibu na kanuni za utumishi na serikali za mitaa waliondolewa na kuachwa wakiranda mitaani na kandambili! Sasa enzi hizi za kompyuta hata miezi 2 bado mtu hajalipwa kama sio ujuha na uzembe!
 
Back
Top Bottom