Madaktari Sawa Watatoka Cuba, India na China. Manesi Je?

kwa hiyo hela za kuwalipa madaktari wa cuba wanazo ila za kuwalipa madaktari wa hapa hawana?
na hao madaktari wataenda mpaka nanjilinji au wataishia muhimbili?

ama kweli akili ni nywele..........

Hizi ni ndoto za mchana huku Wanatembea!!!!!!!!!!

Kama Serikali ya Tanzania imeshindwa kutekeleza madai ya watumishi wake wa kitanzania ambao:-

(1) Wanaishi Manzese kwa gharama yake
(2) Wanatumia usafiri / daladala kwa gharama yake
(3) Wanaenda Tandale sokoni kwagharama yake.
(4) Wananunua mitumba kwa gharama yake.


JE, WATAWEZA...............!!!!

MTUMISHI TOKA NJE YA NCHI.......SERIKALI IGHARAMIE.....

(1) Mshahara ambao siyo pesa za madafu zisizo na thamani.
(2) Malazi
(3) Chakula
(4) Usafiri
(5) Other International Benefits.



Leo hii Serikali haina pesa hata kulipa mishahara watumishi wake, sembuse hao wa nje itawalipa nini.
Tunajua kuwa Srikali yetu huwa inaropoka tu na tulishuhudia hata mgomo wa kwanza Pinda aliropoka na baada ya walalahoi kufa kwa wingi akaamua bila aibu kuwa mnyenyekevu na kuongea na madakitari. Na ndio mchezo anaoufanya leo tena.


SERIKALI IFIKIE WAKATI IELEWE UBABE HAUFAI.


YANGU MACHO :A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed:


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Serikali ni bora kutuleta madaktari wa kichina. Hawana gharama wala tamaa, tunaweza kuwalipa $100 kwa mwezi na kuwalaza katika mabweni kama wanafunzi. Madaktari wa kutoka Cuba ndiyo kabisaa £25 kwa mwezi watafanya kazi kama hawana akili nzuri. Ni kuwajengea tu mahosteli na kuwapa misosi kama ile tuliyokuwa tunakula mashuleni. Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa na hilo wanalijua fika wasitake kutuumiza vichwa, tuwafukuze kazi wote bila kuchelewa. Wamesoma kwa kodi zetu na pia walikubali hiyo kazi wao wenyewe, kwanini leo wanakuwa vigeugeu?.
 
Kweli huku kuoneshana ubabe! Gharama za kuwatoa huko na mishahara wataiweza.? Vitendea kazi navyo waje navyo lasivyo wiki moja tu watajirudisha kwao.
 
Serikali ni bora kutuleta madaktari wa kichina. Hawana gharama wala tamaa, tunaweza kuwalipa $100 kwa mwezi na kuwalaza katika mabweni kama wanafunzi. Madaktari wa kutoka Cuba ndiyo kabisaa £25 kwa mwezi watafanya kazi kama hawana akili nzuri. Ni kuwajengea tu mahosteli na kuwapa misosi kama ile tuliyokuwa tunakula mashuleni. Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa na hilo wanalijua fika wasitake kutuumiza vichwa, tuwafukuze kazi wote bila kuchelewa. Wamesoma kwa kodi zetu na pia walikubali hiyo kazi wao wenyewe, kwanini leo wanakuwa vigeugeu?.

[h=2]Madaktari Sawa Watatoka Cuba, India na China na ikiwezekana hata wagonjwa waje kutoka huko huko![/h]
 
Kadandia vipi sasa? asitoe maoni yake? hao madaktari wasiwe kama watoto wadogo ambao wana demand kitu papo kwa papo,, naunga mkono serikali kuleta madaktari mbadala, tuone watakula wapi. Tusitake kunyanyasa wananchi hapa kisa eti daktari!! Na sisi wabeba zege tukigoma nani atawajengea majumba yenu? acheni upuuzi. Piga chini hao

Wabeba zege mkigoma, serikali yako legelege itawaleta wengine toka nchi za Cuba, India na China.
 
Too late. Ushabiki wa Wanaharakati, wanasiasa na hata baadhi ya watu wengine wa kawaida kabisa hata ambao hawana uwezo wa kwenda kutibiwa nje ya Kata zao hatukuliona kama hilo ni tatizo lililochangia kukua kwa hamasa ya madaktari kugoma. Tuache Serikali itekeleze majukumu yake. Tukianza kuhoji kama Serikali itaweza hayo sasa majungu. Suala la wageni watalipwa shilingi ngapi , ni lazima tukubali hizo ndizo gharama zenyewe hasa pale wazalendo wanapokosa uzalendo. Ikibidi sasa hata mishahara ya Watumishi ipunguzwe zaidi ili kukabiliana na tatizo , hii ni kama vita huwezi kukwepa uwe unaunga mkono mgomo au la. Letu sote.

KWA KWELI KUNA WATU KATIKA NCHI HII WAMEFILISIKA KI MAWAZO, NANI MUUWAJI KATI YA SERIKALI NA MADAKTARI? TUMEONA MWANZO WALIVIMBA KICHWA LAKINI HATIMAE WALIENDA KUKUTANA NA MADAKTARI BAADA YA WATU KIBAO KUFA NA WALICHOFANYA WAKAKUBALI MASHARTI YA MADAKTARI KITAPELI, TUKUMBUKE YA JAIRO WAZIRI MKUU ALISEMA NNINGEKUWA MIMI NDIO MTEULE LEO HII NINGEMFUKUZA KAZI RAIS ALIPORUDI KAGOMA KUMTOA KELELE ZILIPOZIDI WAKAMTOA. HII NI TATIZO LA KUTEUANA KISHIKAJI HATA MTU AKIBORONGA HUWEZI KUMTOA MAANA MKE WA MPONDA AKIKUTANA NA BABA LIZ HUMUITA SHEM NA MUME WA NKYA NAE HUMUITA SHEM KUNA KUWAJIBISHANA HAPO.
SAWA MADAKTARI NI KAMA KIDNAPPERS AMBAO WANADAI PESA BAADA YA KUMTEKA MTOTO NAWE BABA UNAPOGOMA KUWAPA WAKIMUUA WEWE NDIO MUUUAJI ULIEKATAA KUTOA PESA KUMKOMBOA MWANAO. JE NI NANI AMBAE ATAWATIBU WATU WAKIGOMA? ACHENI KUTAPELI MAISHA YA WATANZANIA ETI TUMEJIPANGA LABDA MSEME MMEJIPANGA KWENDA HUKO INDIA MKIACHA MAELFU YA WATANZANIA WAKIFA.ACHENI KUUNGA MKONO SERIKALI DHALIMU:canada:
 
Katika mgomo huu SLAA ni mtuhumiwa numba moja. Asijifanye kukaa kimya kana kwamba wananchi hawajui hilo.

Mambo yakizidi kuwa mabaya asifikiri atapona , wananchi wataanza naye si alishasema kwamba nchi haitatawalika? kwa nini abaki? Kwanza yupo au kishakimbilia Karatu.

masai kaingia na rungu disko..
 
watu wamenza kufa kuanzai jana sasa hilo walojipanga liko wapi? watatuletea madaktari toka INDIA CHINA HATA marekani na hiyo ahadi hewa itawaumbua. Kikwete alipoona watu wanapiga kelele za RICHMOND aliahidi kuileta REAL MADRID MLIIONA ILIKUJA? changa la macho hilo!!KWANI MPONDA CHUMA NA LUCY MKIA ni nani katika nchi hii. LET THEM GO HOME TO SERVE MILIONS OF TZAN .Kwanza DR MPONDA CHUMA ni BWANA AFYA by profession kikwete ampangie bwana afya wa MSOGA akafanye kazi huko kama anaona akimtoa pale ataumbuka
 
kazi ipo...sasa na vifaa watakuja navyo ama? Na hawa wataishi Manzese, Kibamba, Gezaulole ama?
 
Unajua kitakachotokea hao wa nje si watakuja cha kustaajabu watashangaa mbona vitendea kazi hakuna?
Am sure nao watakuwa frustrated na kuiambia serikali madr wenu wameiba vitendea kazi bila kujua kuwa ndo hali halisi
 
Serikali ni bora kutuleta madaktari wa kichina. Hawana gharama wala tamaa, tunaweza kuwalipa $100 kwa mwezi na kuwalaza katika mabweni kama wanafunzi. Madaktari wa kutoka Cuba ndiyo kabisaa £25 kwa mwezi watafanya kazi kama hawana akili nzuri. Ni kuwajengea tu mahosteli na kuwapa misosi kama ile tuliyokuwa tunakula mashuleni. Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa na hilo wanalijua fika wasitake kutuumiza vichwa, tuwafukuze kazi wote bila kuchelewa. Wamesoma kwa kodi zetu na pia walikubali hiyo kazi wao wenyewe, kwanini leo wanakuwa vigeugeu?.


Umeshalewa pombe ya mnazi wewe unaropoka ovyo hatukuwezi kamwe!!!!




MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Suluhisho la madaktari si kuleta mercenaries wa kitabibu kutoka nchi za kijamaa, bali ni kutatua matatizo yao. Vipi siku JWTZ nao wakigoma?, itakuwaje?. Serikali kwenye hili imeshikwa pabaya sana. Madaktari ni watu muhimu zaidi ya askari. Madaktari wana authority kubwa sana kitaaluma kuhusu miili yetu.

Kwa kuwa wewe unatibiwa nje ya nchi usione kuwa hauhusiki, kuna issue za dharura ambazo zinahitaji huduma in the first 10 minutes kama cardiac arrest ambayo ninaamini viongozi wengi wanatembea kivuli chake. 10 minutes haziwezi kukufikisha India au Germany au USA au UK. Tuache siasa tutatue matatizo yanayotukabili.

Siafikiani na mgomo ila pia siafikiani na njia za kutatua mgomo. Ule ubabe wa miaka ya sitini na sabini leo hii hauna nafasi. Nina hakika kabisa kuwa kama Tanzania ingekuwa inachaguz viongozi wake kwa kura halali, viongozi wangehaha kumaliza matatizo ya wananchi kwa hofu ya kuwekwa kando. Ila kwa kuwa serikali ya Tanzania ni ya kimapinduzi inayopindua matakwa halali ya wananchi kuhusu nani awaongoze kwa kutumia dola ndiyo inawapa kiburi hiki. Sooner or later wote tutalia na kusaga meno tusipotumia busara kwenye mambo madogo ya kitaifa kama hili la madaktari. Je mambo makubwa kama Katiba tutaweza?
 
Kama sikosei gazeti la Rai Mwema nimeiona imetoa idadi ya wagonjwa 216 waliokufa kwenye mgomo wa mwanzo yaani inahitaji uwe na roho ya ngumu zaidi ya sheta kuendelea kuwa na ujasiri wa kutofikiria kujiuzulu kwa hilo. Mie ningekuwa Pinda ningejiuzulu kwa niaba ya Waziri wa Afya na Naibu wake ili kuwapashinikizo na wao wafikirie kujiuzulu.
 
Serikali ikifanya hivyo itatesa watu. Madaktari wetu wappendwa watakula nini. Botswana kazi hakuna tena.
 
Walikuwa wanadai Mawaziri wajiuzulu. Yaani Madaktari bwana thehe thehe thehe, kwa hiyo wasipojiuzulu watoto wa Madaktwari haya hawatakwenda choo? Kazi kweli kweli. Daktari acheni hizo bwana. Mnajua kazi yenu kama kazi nyingine tu. Hivi Daktari ukipewa kazi ya kutengeneza hata stuli utaweza kweli? ukiambiwa umfundishe mtoto wa miaka mitatu hadi ajue kusoma utaweza? ukiambiwa kazi yako ni kuimba kwenye jukwaa ili watoto wako wapate kula utaweza? ukiambiwa ukatembee na viatu unauza mitaani kutoka Igoma hadi Nyakato, Ghana hadi Kirumba utaweza kweli Daktari? Basi hivyo wenzenu tunavyoteseka kuhakikisha familia zetu zinaishi. Kazi yenu kama kazi zingine

Rais akimfukuza waziri kwa tatizo ili (inshu ya madaktari) huo utakuwa uwamuzi utakao leta madhala makubwa sana kwenye anga la serikali ya watanzania na watu wake.Utakuwa ugonjwa uliokosa dawa na kukuwa kwa haraka bila ya tiba uku ukiacha mamimia yakipukutika ndugi zangu lioneni hili kiundani na kiumakini sana.....

Ikiwa waziri mwenyewe kwa hiyari yake atajiuzulu hilo litakuwa somo la shujaa aliepambana mpaka tone lake la mwisho kwisha kuamua kubaki pembeni na kuwapisha wenye nguvu zaidi na wasio na majeraha kusonga mbele kwa hali yoyote itakayojitokeza kushinda au kushindwa bila lawama

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE INSHALLAH
 
Katika mgomo huu SLAA ni mtuhumiwa numba moja. Asijifanye kukaa kimya kana kwamba wananchi hawajui hilo.

Mambo yakizidi kuwa mabaya asifikiri atapona , wananchi wataanza naye si alishasema kwamba nchi haitatawalika? kwa nini abaki? Kwanza yupo au kishakimbilia Karatu.


Acheni kutafuta...mchawi..Chadema wangeamua kushabikia huu mgomo ....serikali ingeshaondolewa na jeshi....maana wananchi wangejaa mitaani ...Chadema, wanaangalia tu ..kwenye hili na kumuonea Jk huruma..
 
Kama kweli imeamua hivyo kwa dhati kuwaleta wataalamu hao kwa emergency basi naishauri ifanye yafwatayo:-
(1)Kuwafukuza kazi madaktari wote waliopo kwenye mgomo.
(2)Kuwanyang'anya vibali vya utabibu madaktari wote waliofukuzwa kazi ikiwemo kutotambua weredi wao.
(3)Kutangaza kazi upya zenye masharti yanayobana kuwepo kushiriki migomo na viapo vya utiifu wa weredi.Na atakayerudi kundini ndiyo anarudishiwa cheti cha utabibu.
(4)Masharti ya namba 3 pia yawekwe kwa madaktari wapya waliohitimu vyuo mbalimbali(Waliomaliza intern).Masharti haya yawahusu pia madaktari wanaohitimu vyuo vya nje /wale wanaojiendeleza kwa elimu ya juu zaidi ambao ni waajiriwa wa serikali na kwamba wasitambuliwe weredi wao mpaka wale kiapo cha utiifu na kuijicommit kwa maelezo.

Kwa kufanya hivyo nauhakika watakaoendelea na mgomo watakuwa ni wale tu ambao ni wajasiriamali wa biashara nyingine ambayo haihusiani na udaktari.Hawa wanaomaliza intern kuwapata ni vyepesi maana hata kazi hawana na vibali vya kufanyakazi za utabibu wasipewe njaa itawakamata na watarejea kundini wenyewe.Madaktari wa mikoani nao ni vyepesi pia kuwapata maana wengi jeuri yao inatokana na vizahanati vyao vya uswahilini ambavyo ambavyo kwa asilimia kubwa wanachakachua madawa na facilities nyingine kutoka hospitali za serikali muda mfupi tu njaa itawakamata watapiga magoti kukili kosa.

Mgomo wa kwanza nilikuwa nao bega kwa bega lakini sasa tangu waanze siasa kwenye maisha ya watu kwa kweli sio siri wamenikera sana!!Leo wameanza na Dr Mponda na Dr Nkya na kesho wakikubaliwa kesho wataibuka na Pinda mwenyewe kwamba kwanini mara ya kwanza aliwatisha hivyo ajiuzuru,mwisho watamalizia na JK kwanini alikuwa kimya wakati wanagoma.At the same time huo ndiyo utakuwa mchezo wa watumishi wa umma maana baada ya hapo wataibuka walimu,mara polisi wamechoka kukaa kwenye full suti wanataka Nahodha ajiuzuru na serikali itakosa muelekeo maana itakuwa inaendeshwa na watu bila kuwa na maamuzi yake!!

Hivi kama ishu ni Dr Nkya na Dr Mponda vile mlivyokuwa mnawazomea na kukataa kukutana nao haitoshi kuonyesha kuwa hamuwataki waendelee kuwepo kwenye nyadhifa zao mpaka mtuue walalahoi tusiokuwa na hatia?

Nawakilisha!!
 
Back
Top Bottom