Lugovoy
JF-Expert Member
- Mar 2, 2011
- 573
- 170
Haipendezi hata kidogo kwa mtu mwenye akili timamu kushabikia mgomo wa madaktari...!!!
Mgomo wa madaktari ni jambo la kusikitisha sana, maana yake kuna watu wanakufa kwa kukosa
matibabu...kama mkeo/mumeo amepelekwa MNH akakutana na huo mgomo unaweza shabikia??
Jambo la msingi ni kuihimiza serikali yetu tukufu iwasikilize haraka madaktari kama ilivyofanya kwa
wabunge, maana karibia waalimu wataanza, kisha mahakimu watafuatia, halafu sijui nani tena wanajeshi au???
Ok fine sio vyema kushabikia mgomo wa madaktari,lakini wana madai yao ya msingi sana hata wagonjwa wenyewe wanawaunga mkono,kwa nini hatuukubali ukweli kwamba uzembe na ubinafsi wa serikali ndio chanzo cha manyanyaso yote haya kwa wagonjwa tunabaki kuwapa lawama madaktari,tusiwe selfish kiasi hicho!!!!!!!!!!!!, na hapo kwenye red sijui umetumia vigezo gani?