Upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kupitia pua wafanyika Hospitali ya Mloganzila

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imefanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kupitia pua (Endoscopic transphenoidal pituitary) bila kupasua fuvu la kichwa ambapo tangu kuanza kwa huduma hii takribani watu watano wamenufaika na matibabu hayo.
3acc33d8-e2de-4143-bebd-6a1123204a8b.jpg

Upusuaji huo umefanywa na Madaktari wazawa ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa huduma za kibingwa na kibobezi zinazotolewa katika hospitali hii ikiwa ni juhudi za kuunga mkono Serikali za kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa huduma za upasuaji Muhimbili Mloganzila, Dkt. Godlove Mfuko, amesema upusuaji huo umefanywa kwa ushirikiano wa Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu pamoja na Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Koo na Masikio.

“Upasuaji huu umefanywa na madaktari wetu kwa mafanikio makubwa, leo tumemfanyia mgonjwa mmoja, mgonjwa huyu endapo angepelekwa nje ya nchi kutibiwa ingegharimu takribani TZS. 40 Mil kwa mgonjwa mmoja lakini kwa hapa inagharimu taktibani shilingi milioni sita mpaka nane” amesema Dkt. Mfuko.
49157255-9d11-4e20-8253-c2d1156f1c8b.jpg

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili-Mloganzila Dkt. Raymond Makundi ameeleza kuwa wagonjwa wengi wanaofanyiwa upasuaji huo wanakuja wakiwa na dalili za uoni hafifu na wakifanyiwa uchunguzi wanagundulika kuwa na uvimbe ambao unasababisha athari kwenye mishipa ya uoni.

“Sababu zinazosababisha kupata uvimbe kwenye ubongo zipo nyingi ikiwemo swala la vinasaba ambavyo huchangia kwa kiasi fulani ila asilimia kubwa ya watu wanaokutwa na magonjwa haya huwa yanatokea bila sababu yoyote” amesema Dkt. Makundi

Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Koo na Masikio kutoka MNH, Dkt. Edwin Liyombo amesema awali upasuaji huo ulikua ukifanyika kwa kufungua fuvu la kichwa lakini kutokana na mabadiliko ya teknolojia sasa unafanyika kwa kupitia pua ambapo mgonjwa anachukua muda mfupi kupona na upasuaji huo ni salama.
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imefanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kupitia pua (Endoscopic transphenoidal pituitary) bila kupasua fuvu la kichwa ambapo tangu kuanza kwa huduma hii takribani watu watano wamenufaika na matibabu hayo.
View attachment 2712934
Upusuaji huo umefanywa na Madaktari wazawa ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa huduma za kibingwa na kibobezi zinazotolewa katika hospitali hii ikiwa ni juhudi za kuunga mkono Serikali za kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa huduma za upasuaji Muhimbili Mloganzila, Dkt. Godlove Mfuko, amesema upusuaji huo umefanywa kwa ushirikiano wa Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu pamoja na Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Koo na Masikio.

“Upasuaji huu umefanywa na madaktari wetu kwa mafanikio makubwa, leo tumemfanyia mgonjwa mmoja, mgonjwa huyu endapo angepelekwa nje ya nchi kutibiwa ingegharimu takribani TZS. 40 Mil kwa mgonjwa mmoja lakini kwa hapa inagharimu taktibani shilingi milioni sita mpaka nane” amesema Dkt. Mfuko.
View attachment 2712935
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili-Mloganzila Dkt. Raymond Makundi ameeleza kuwa wagonjwa wengi wanaofanyiwa upasuaji huo wanakuja wakiwa na dalili za uoni hafifu na wakifanyiwa uchunguzi wanagundulika kuwa na uvimbe ambao unasababisha athari kwenye mishipa ya uoni.

“Sababu zinazosababisha kupata uvimbe kwenye ubongo zipo nyingi ikiwemo swala la vinasaba ambavyo huchangia kwa kiasi fulani ila asilimia kubwa ya watu wanaokutwa na magonjwa haya huwa yanatokea bila sababu yoyote” amesema Dkt. Makundi

Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Koo na Masikio kutoka MNH, Dkt. Edwin Liyombo amesema awali upasuaji huo ulikua ukifanyika kwa kufungua fuvu la kichwa lakini kutokana na mabadiliko ya teknolojia sasa unafanyika kwa kupitia pua ambapo mgonjwa anachukua muda mfupi kupona na upasuaji huo ni salama.
Hongera sana ziende kwa Madr wetu
 
Halafu utakuta ma daktari muhimu kama hawa wanaokoa maisha ya raia wanalipwa mishahara kiduchu kuliko lile genge (bonge) pale dodoma.
 
Hongereni madaktari bingwa ila inasikitisha kuwapata wataalamu hawa baada ya miaka zaidi ya 60 tangia tupate Uhuru. Tusishangae tutakapokuja kupata wanasayansi wataokwenda mwezini 2500's😄😄
 
Hongereni madaktari bingwa ila inasikitisha kuwapata wataalamu hawa baada ya miaka zaidi ya 60 tangia tupate Uhuru. Tusishangae tutakapokuja kupata wanasayansi wataokwenda mwezini 2500's
walikuwepo miaka hiyo sema walikuwa wachache pia tuangalie safari yetu tumetoka wapi na sasa tupo wapi.
 
Dr Godlove Mfuko,those times at Sokoine Lindi regional refferal hospital
 
Back
Top Bottom