Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

ABS inatakiwa kuwa On muda wote au haitakiwi kuwa On!?.
Brevis ina kaclutch flani pembeni ya Brake pedal, nikishusha chini kanaiwasha taa ya ABS na nikipandisha taa ya ABS inazima!. Kwa uelewa wangu ninavyohisi ABS inanisaidia kipindi cha Emergency so acha iwe on muda wote!. Swali je nipo sahihi!?..
(nimeona Mshana Jr kaweka picha hapo juu taa ya ABS ikiwa on nikamuone fundi).
 
Nenda kwa Wataalamu wabadili raba ya nyuma na mbele pia wacheck kwenye Oil Sampo huwa ina leak kwa kulowa tu huwezi ona ikidondoka chini kwahiyo wafungue sampo watakapoirudishia wajaribu kuzipaka na silicon kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Km 30000 mbona nyingi sana.. Au sijakuelewa.. Mara nyingi unatakiwa kufanya service kila baada ya km 2000, 3000, 5000 au 10000.
 
Watabe....nauliza wapi ntapata wataalaam wa kupiga rangi gari...location...dsm....any referal?!
Kuna jamaa anaitwa Hemed kama hujapata fundi nijulishe nikuunganishe naye.

Anapatikana maeneo ya Sayansi. Binafsi wiki mbili zilizopita amenipakia rangi gari langu na nimeridhika kabisa. Ni muaminifu pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau kuna gari aina ya Nissan xtrail inatatizo la kushindwa ku-start asubuhi au wakati wa baridi, mafundi wamejitahidi ila tatizo halijaisha, temperature sensor na starter vimebadilishwa bila ya mafanikio.... msaada tafadhali
 
Kuna hii premio ya mwaka 2002, yenye CC1490, VVTI. Nimeipenda na bei yake ni nzuri tuu milion 13.5 : naomba mtu anaye imiliki au amewah kuwa nayo anipe ABC zake kidogo.
 
Wadau kuna gari aina ya Nissan xtrail inatatizo la kushindwa ku-start asubuhi au wakati wa baridi, mafundi wamejitahidi ila tatizo halijaisha, temperature sensor na starter vimebadilishwa bila ya mafanikio.... msaada tafadhali
Mara nying inakuwa vitu vitatu, battery imechoka, oil unayotumia sio sahihi hivyo kusababisha hilo kutokea, weka oil sahihi ya nissan, na mwisho inawezekana kuna unyevu au maji kwenye line ya mafuta, hivyo flush line na tank liwe safi kabisa kisha weka mafuta mapya, kwa hayo tatizo litakuwa limeisha. Mara nyingi mafundi wanakimbilia starter lakini haiwi tatizo katika ugonjwa huo.
 
Back
Top Bottom