Kaka hili sina uhakika nalo kwakweli
Chukua kitu BMW kaka
Unajua kila mtu ana uzoefu wake inategemea yeye ana Platz model gani,lakini kwa ninazozifahamu mimi sikushauri
Honda nazo zipo ambazo ni vimeo hasa lakini kwa mfano ukipata RD5 ni gari nzuri mno, hata RD 1 pia kuna mdau kavuta moja hapahapa jukwaani baada ya kushauriana anaweza kuwa shuhuda mzuri
BTW gari yeyote ni matunzo, hata upate gari ngumu vp kama itakosa matunzo tarajia kifo cha mapema tu
kuna jamaa yangu alikuwa na gari rav4 ina engene ya D4 ilimzingua akaamua kubadili na kuweka engene ya 3S, gari imekataa kukaa silance tatizo linaweza kuwa nini na afanyeje manake hiyo gari hata kuuzika imegoma.
Voltz kwa maoni yangu ni hybrid ya SuV na sedan....nimeziona no nzuri kwenye ulaji wa mafuta maana ni cc 1780 kama sikosei. Ningemshauri jamaa ainunue nadhani bei hadi 16M
Niliwahi kusoma uzi mmoja humu kuwa Voltz zilitengenezwa piece 10,000 tu na uzalishaji wake ukasimamishwa. Hivyo spea zake itakuwa ishu.
Samahani mimi nina hilux surf ina engine ya 2LT yenye turbo ila imenisumbua sana hadi nikaamua kununua engine nyingine ila mkanganyiko uko pale mafundi wanaponipa ushauri tofauti. Wengine wanadai niweke engine ya petrol, wengine eti niweke isiyo na turbo ila ya diesel, naombeni ushauri.
Sio kweli kuwa turbocharged engine ni mbovu!!, , ila nakubaliana na wewe kuwa kuna baadhi zinasumbua ,Kwanza pole sana 2LT, ni engine majanga sijapata kuona, Hilux Surf nyingi zilipoteza umaarufu kwasababu ya hii engine
Binafsi naomba nikushauri kitu kimoja achana kabisa na Turbo, funga engine yoyote lakini sio ya Turbo!!! Kwa uhakika zaidi fungal engine ya petrol utaokoka na mengi
jamani kuna mdau aliuliza kuhusu Toyota wish hakujibiwa na mimi nilikuwa nasubiri ninufaike hapo, yeyote anayejua mazuri na mabaya yake nahitaji kununua kwa matumizi ya kawaida tu sio rough road. kama kuna mtu anajua consumption ya mafuta na durability yake kwa ujumla msaada.
Sio kweli kuwa turbocharged engine ni mbovu!!, , ila nakubaliana na wewe kuwa kuna baadhi zinasumbua ,
Tunakosea pale tunapojaribu kutumia engine za turbo Kama engine za petroli au natural aspirated diesel engine ,
Turbo ni moja ya vitu complex na very sensitive , lakini fairly treated , huwa zina last almost forever,kiufupi Turbo zinakadiriwa kuwa na maisha sawa na injector pump, by default injector pump zinakuwa na life span ile ile ya engine.
Fanya haya next time utakapotumia engine zenye turbo
Oil.... Hakikisha unatumia oil yenye ubora wa juu
Usizime gari au engine Mara baada ya kufanya kazi nzito au safari ndefu
Air cleaner safisha Mara nyingi uwezavyo
To the best of my knowledge most economic durable,compact and powerful four stroke engine to date ..ni hizo turbocharged diesel engine
Alamsiki !!!
Ni nzuri ila sio imara hasa huko chini kwenye wish-bones , tyrodends ball joints na stabilizer links huyo ndio ugonjwa wake mkubwa
Hebu nieleweshe........Toyota Wish inatumia tie rod end au stab link.......?........
witnessj nilikukumbuka Leo, watu niliiongea nao ambao ni wamiliki wamezisifia sana, wote karibia bado ni mpya hawajazitumia sana hivyo ni ngumu kujua weakness zake, bei zinarange 25-30m, kwa mujibu waoSamahani kaka mshana jr bado haujanijib kuhusu toyota vanguard new model, pia ningependa kujua weakness zake. Shukran