Mabalozi CCM wanaswa wakiandikisha wapigakura

311717_2092603682907_1479725938_31913536_415493289_s.jpg

Wali waliohonga CCM Igunga huu hapa
 
Huyo mzee aliisha achana na ubalozi siku nyingi na si kada tena wa CCM.Huu ni ujanja wa CDM kutaka kujisafisha kwa kitendo cha aibu walichomfanyia DC.Watu wa Igunga wanajua ukweli labda wadanganyeni watu wa Arusha na K'njaro.
kwahiyo untaka kusema hyo picha ni uchaguzi uliopita???simple minded
 
Hili sio la kulifumbia macho, ni kuhakikisha majina yote walioandikisha yanakuwepo siku ya kupiga kura, bila kuchakachuliwa.

Hivi hawa magamba hawaon i hii mbinu wanayoitumia imepitwa na wakati?
 
main(19).jpg

Kada wa CCM abambwa na shahada za kura

Balozi wa nyumba kumi, katika Kijiji cha Mwayunge Mashariki, Kata ya Igunga mkoani hapa Nghoboko Masele, anadaiwa kukamatwa na vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwa na shahada ya kupigia kura na orodha ya majina ya wapiga kura pamoja na namba za shahada zisizo zake. Akizungumza na NIPASHE, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa la Chadema (Bavicha), John Heche, alisema kuwa balozi huyo alikamatwa jana asubuhi akiwa katika harakati za kuandikisha majina ya wapiga kura na namba za shahada zao.

“Tumemkamata akiwa na orodha ya majina ya wapiga kura na namba za shahada zao zaidi ya 40 na tulipomhoji alisema kuwa ametumwa na Mwenyekiti wa CCM, wa Wilaya ya Igunga kuorodhesha majina hayo kazi ambayo wamepewa wenyeviti wa vitongoji wote wanaongoza kwa tiketi ya CCM,” alidai Heche. Alisema balozi huyo aliyekutwa akizunguka katika nyumba za watu kuorodhesha majina ya wapiga kura. “Alituambia kuwa anayekataa kufanya hivyo anamwambia hatapiga kura na hatapata chakula cha msaada kinachotolewa na serikali kwa ajili ya njaa,” alisema.
Alipoulizwa Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini wa Jeshi la Polisi, Isaya Mungulu, alisema kuwa yuko nje kidogo ya kituo cha Polisi na hana taarifa juu ya kukamatwa kwa balozi huyo.

Source: IPPMedia
 
Huyo mzee aliisha achana na ubalozi siku nyingi na si kada tena wa CCM.Huu ni ujanja wa CDM kutaka kujisafisha kwa kitendo cha aibu walichomfanyia DC.Watu wa Igunga wanajua ukweli labda wadanganyeni watu wa Arusha na K'njaro.

We unatumia kiungo gani kufikiria kati ya hivi vifuatavyo? masaburi, pua, ulimi, uume?
 
Huyo mzee aliisha achana na ubalozi siku nyingi na si kada tena wa CCM.Huu ni ujanja wa CDM kutaka kujisafisha kwa kitendo cha aibu walichomfanyia DC.Watu wa Igunga wanajua ukweli labda wadanganyeni watu wa Arusha na K'njaro.
<br />
<br />
WAKIKUBALI MAGAMBA KAZ KWEL KWEL!
 
I don't believe that this story bears any validity although many crassest credulous simpletons buys it unquestionably. There is some contradiction on the day and place where this photos were captured. As far as I understand, Igunga is a semi-arid region, then how comes that the backround is something different from Igunga I know? I can conspicuously smell elements of apocryphalness and mendaciousness on this story.
 
Najaribu ku-imagine kibano wanachokula CCM huko Igunga toka kwa CDM! Wanajuuuta kuwafahamu Makamanda!
 
07kurabalo.jpg

CUF Nayo yalalamika CCM kuhujumu Uchaguzi

main(19).jpg

WAKATI joto la uchaguzi mdogo wa Jimbo a Igunga likiendelea kupanda, Chama cha Wananchi (CUF) kimekituhumu CCM kuwa kimeanza kukusanya na kuorodhesha kadi za wapiga kura na kwamba, kimemkamata mmoja wa mabalozi wa nyumba kumi wa CCM wakati akifanya kazi hiyo. Tuhuma hizo dhidi ya CCM zilitolewa jana na mgombea wa CUF, Leopold Mahona, ambazo tayari zimeshapingwa na Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba.

Akiwa katika kijiji cha Imalilo, Kata ya Nguru, jimboni humo, Mahona alisema kazi kuorodhesha majina ya wapiga kura na kadi zao inaratibiwa na kusimamiwa na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM. Mahona aliwataka wakazi wa kijiji hicho kukataa mpango huo kwa kutotoa vitambulisho vyao vya kupigia kura, kwani wakikubali kufanya hivyo watashindwa kuchagua mwakilishi mwenye uwezo wa kuwasaidia.

Kauli ya Mahona imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, kuwataka wakazi Igunga kujiandaa kukabiliana na hujuma zinazotarajiwa kufanywa na CCM kwa lengo la kulazimisha ushindi, kutokana na chama hicho kupoteza mvuto kwa wananchi. "Wakija kuwaomba shahada kataeni, hata wakiwatisha msikubali, mkae kimya na msiwafanye chochote. Subirini siku ya kupiga kura na mnichague mimi nikaletee maendeleo,'' alisema Mahona. Mahona alidai kuwa, wajumbe hao wanawatisha wakazi wa jimbo hilo wanaounga mkono upinzani na kulaani kuwa, kitendo hicho kinakwamisha maendeleo na juhudi za mabadiliko ya kidemokrasia.

Hujuma sehemu mbalimbali

Wakati mgombea huyo wa CUF akilalamikia kitendo hicho, mwandishi wa habari hizi imeshuhudia tukio la uandikishaji kadi hizo ukiendelea katika maeneo mbalimbali. Mwandishi alishuhudia kijana mmoja, mkazi wa kata ya Iborogero, nje kidogo ya mji wa Igunga akiorodhesha majina ya wenye vitambulisho vya mpiga kura pamoja na namba za vitambulisho vyao vya mpigakura. Kijana huyo alipoulizwa na Mwananchi, huku akisita kutaja jina lake, alisema kazi hiyo amepewa na wakubwa wake ambao alikataa kuwataja na kusisitiza kuwa, anachofanya ni kuorodhesha majina ya wapiga kura na vitambulisho vyao kupigia kura kisha kuviwasilisha kwa wakubwa.

''Mimi kazi yangu kukusanya taarifa za watu wenye vitambulisho vya mpigakura. Ninaandika majina yao pamoja na namba ya kitambulisho nawasilisha kwa wakubwa, wao watatoa maelekezo na hatua za kuchukua,'' alisema kijana huyo. Mmoja watu waliotoa kadi zao, Chiristina Kaloli, mkazi wa Iborogero alipoulizwa na gazeti hili alikiri kuwa, kadi yake imeishaandikishwa mjumbe wa CCM huku kusisitiza kuwa hiki ni kipindi cha mavuno kwao.

Kadi hiyo ambayo mwananchi iliona kumbukumbu zake Ikiwa na namba 05262605 inaonyesha kuwa, &#8216;Chritina Kaloli alijiandikisha kuwa mpiga kura Desemba 26, 2004 katika Shule ya Msingi Mpogoro, Wilaya ya Igunga'.

Source: Mwananchi
 
I don't believe that this story bears any validity although many crassest credulous simpletons buys it unquestionably. There is some contradiction on the day and place where this photos were captured. As far as I understand, Igunga is a semi-arid region, then how comes that the backround is something different from Igunga I know? I can conspicuously smell elements of apocryphalness and mendaciousness on this story.
If don't believe this what else can you believe?..Balozi wa Nyumba Kumi katika Kijiji cha Mwayunge Mashariki, Kata ya Igunga mkoani Tabora, Nghoboko Masele, Akiwa chini ya ulinzi baada kukamatwa na wafuasi wa chadema na shahada za kupigia kura pamoja na orodha ya majina ya wapiga kura aliyodaiwa kukutwa nayo
 
Tunaomba hao mabalozi na mwenyekiti wa wilaya ccm igunga nao wakamatwe na polisi wakahojiwe isiwe tu kuwakamata wabunge wa cdm
 
Hiyo sura kama mkaanga sumu, huyu hakosi misukule kama 20 hivi nyumbani kwake.
Taratibu mkuu, umejiangalia kwenye kioo kabla ya kupost thread yako? Unamejitabiria baada ya miaka kumi utakuwaje? Unafikiri yeye anatafuta mchumba, yeye anatafuta kura period
 
Makamanda wanafanya kazi nzuri sana uko Igunga, mpaka magamba watie akili safari hii
 
CUF Nayo yalalamika CCM kuhujumu Uchaguzi

main(19).jpg

WAKATI joto la uchaguzi mdogo wa Jimbo a Igunga likiendelea kupanda, Chama cha Wananchi (CUF) kimekituhumu CCM kuwa kimeanza kukusanya na kuorodhesha kadi za wapiga kura na kwamba, kimemkamata mmoja wa mabalozi wa nyumba kumi wa CCM wakati akifanya kazi hiyo. Tuhuma hizo dhidi ya CCM zilitolewa jana na mgombea wa CUF, Leopold Mahona, ambazo tayari zimeshapingwa na Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba.

Akiwa katika kijiji cha Imalilo, Kata ya Nguru, jimboni humo, Mahona alisema kazi kuorodhesha majina ya wapiga kura na kadi zao inaratibiwa na kusimamiwa na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM. Mahona aliwataka wakazi wa kijiji hicho kukataa mpango huo kwa kutotoa vitambulisho vyao vya kupigia kura, kwani wakikubali kufanya hivyo watashindwa kuchagua mwakilishi mwenye uwezo wa kuwasaidia.

Kauli ya Mahona imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, kuwataka wakazi Igunga kujiandaa kukabiliana na hujuma zinazotarajiwa kufanywa na CCM kwa lengo la kulazimisha ushindi, kutokana na chama hicho kupoteza mvuto kwa wananchi. "Wakija kuwaomba shahada kataeni, hata wakiwatisha msikubali, mkae kimya na msiwafanye chochote. Subirini siku ya kupiga kura na mnichague mimi nikaletee maendeleo,’’ alisema Mahona. Mahona alidai kuwa, wajumbe hao wanawatisha wakazi wa jimbo hilo wanaounga mkono upinzani na kulaani kuwa, kitendo hicho kinakwamisha maendeleo na juhudi za mabadiliko ya kidemokrasia.

Hujuma sehemu mbalimbali

Wakati mgombea huyo wa CUF akilalamikia kitendo hicho, mwandishi wa habari hizi imeshuhudia tukio la uandikishaji kadi hizo ukiendelea katika maeneo mbalimbali. Mwandishi alishuhudia kijana mmoja, mkazi wa kata ya Iborogero, nje kidogo ya mji wa Igunga akiorodhesha majina ya wenye vitambulisho vya mpiga kura pamoja na namba za vitambulisho vyao vya mpigakura. Kijana huyo alipoulizwa na Mwananchi, huku akisita kutaja jina lake, alisema kazi hiyo amepewa na wakubwa wake ambao alikataa kuwataja na kusisitiza kuwa, anachofanya ni kuorodhesha majina ya wapiga kura na vitambulisho vyao kupigia kura kisha kuviwasilisha kwa wakubwa.

‘’Mimi kazi yangu kukusanya taarifa za watu wenye vitambulisho vya mpigakura. Ninaandika majina yao pamoja na namba ya kitambulisho nawasilisha kwa wakubwa, wao watatoa maelekezo na hatua za kuchukua,’’ alisema kijana huyo. Mmoja watu waliotoa kadi zao, Chiristina Kaloli, mkazi wa Iborogero alipoulizwa na gazeti hili alikiri kuwa, kadi yake imeishaandikishwa mjumbe wa CCM huku kusisitiza kuwa hiki ni kipindi cha mavuno kwao.

Kadi hiyo ambayo mwananchi iliona kumbukumbu zake Ikiwa na namba 05262605 inaonyesha kuwa, ‘Chritina Kaloli alijiandikisha kuwa mpiga kura Desemba 26, 2004 katika Shule ya Msingi Mpogoro, Wilaya ya Igunga’.

Source: Mwananchi

Katika mazingira kama haya unashangaa viongozi wa vyama vya upinzani wanaendelea kutoa matamko, hapa ni mpumbavu tu ndiye anayeweza kuamini kuwa haki itatendeka katika huu uchaguzi. Kuendelea kushiriki uchaguzi huu bila ya kuwa na plan b ya tutafanya nini kuzuia matokeo ambayo moja kwa moja yanaonyesha ccm ndio wanaenda kushinda kwa hila nao ni upumbavu mwingine. Hapa naona kabisa kunakupoteza nguvu na raslimali nyingine bure wakati imeshajulikana nini kinaenda kutokea hapo igunga 2/10/2011. Katika mazingira kama haya unategemea kuona muujiza gani zaidi ya vyama vingine kushindwa na ccm. Mbaya zaidi na vyama hivi vya upinzani vinasubiri vishindwe kwa kuchezewa rafu ndio vianze kulialia.
 
naona anaye watetea ndio kisha kula ban sijui nani mwingine atawakilisha upande wa ccm..humu jamvini!
 
Back
Top Bottom