Mabalozi CCM wanaswa wakiandikisha wapigakura

07kurabalo.jpg

Cheki hiyo pozi, kweli CCM wameishiwa yaani hiyo Igunga utafikiri uchaguzi wa uraisi!!!!!!!!! Yaani huyo jamaa anaonekana hata jero unamnunua hahaha ahahah!!!!!!
 
Hii tabia ya kuandikisha kadi za wapiga kura ikomeshwe na wanaofanya hilo zoezi wachukuliwe hatua ya ubakaji wa demokrasia ya mpiga kura.Takukuru muko wapi ?Sababu vya vya siasa vikipeleka malalamiko NEC hakuna hatua.Wananchi wakimakata wanaofanya kampeni za maji taka inakuwa wamejichukulia sheria mkononi.Serikali hii ya ccm inakatisha tamaa kabisa.Heri kuwa maskini wa pesa kuliko kuwa maskini wafikira sahihi
 
Haka ni kamchezo ambako CCM imekuwa ikikacheza tangu uchaguzi wa 2000, na umeigwa kutoka Kenya (KANU iliutumia katika uchaguzi wa 1997, lakini ilishindikana katika uchaguzi wa 2002 kwa sababu nguvu ya NARC ilikuwa kubwa mno. Pia umekuwa ukitumiwa sana kule Zimbabwe.

Mchezo huo unataka ushirikiano kati ya chama tawala na Tume ya uchaguzi. Balozi wa kumikumi (wa CCM)huagizwa kukusanya orodha ya majina ya wapiga kura katika maeneo yao na namba za shahada zao za kupigia kura, kwa kisingizio eti wanakusanya majina ya wanachama wao tu.

Mara moja mtu atashituka kwani majina ya wanachama wa CCM si yako katika ofisi ya CCM ya tawi la sehemu hiyo?

Baadaye kinachofanyika ni kwamba orodha ya majina haya hupelekwa Tume ya uchaguzi (NEC) ambako hutafutwa daftari la wapiga kura waliojiandikisha katika eneo hilo.

Wakati NEC inatayarisha orodha ya majina ya wapiga kura yatakayobandikwa katika vituo vya wapiga kura kwa ajili ya siku ya kupiga kura, majina mengine yote huachwa isipokuwa yale yaliyomo katika orodha ya wapiga kura wa CCM iliyopelekwa ambayo ndiyo itaonyeshwa na NEC kam orodha rasmi ya wapioga kura wa eneo hilo siku ya kupiga kura. Huenda yakaachwa majina ya wengine kwa ajili ya kudanganyisha.

Kwa hiyo siku ya kupiga kura watu wengi hawakuti majina yao ingawa shahada wanazo, na ndiyo maana asilimia 42 tu ya wapiga kura wote ndiyo waliweza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

NEC huwa haitaki tu kufanya uchunguzi kuhusu hili kwa sababu hufanya kazi kwa niaba ya CCM. Huishia tu kutoa majibu mepesi mepesi tu kwamba watu hawakuenda kupiga kura.

Kamchezo haka kana hatari yake – kuwarudia wenyewe, kama ilivyotokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Wengi waliyoorodheshwa kwa njia hii kwa kufikiri wangepigia CCM hawakuipigia CCM kwani kampeni zilivyokuwa zikiendlea walibadilisha dhamira na kuipigia CDM.

Kadhalika wengi walioachwa katika orodha ambao wangeipigia CCM hawakuyaona majina hayo, hivyo CCM ilikosa kura nyingi kwa njia hii. Kwa kiasi flani ni kamchezo ka-kubahatisha ingawa dhamira kubwa ni kuwaenguwa wale ambao CCM inafikiri watapigia upinzani – hasa CDM.

Inafaa NEC itoe tamko kuhusu hili kwa kikemea tabia hii ya kimikumi wa CCM kuorodhesha majina ya wapiga kura. CDM iibane sana NEC kwani kukaa kwake kimya inaonyesha inakubali kwamba inashirikiana na CCM katika hujuma dhidi ya upinzani.

CCM walitumia njia hiyo katika uchaguzi mdogo Tarime mwaka 2008 lakini wapiga kura kule walipoona majina yao hayako kwenye orodha siku ya kupiga kura ili hali wanazo shahada walikuja juu na kutaka kuwakata mapanga wasimamizi wa vituo.

Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba baadaye NEC makao makuu iliagiza wote wenye shahada halali za kupiga kura hata kama majina yao hayako kwenye orodha ili mradi shahada zinaonyesha ni wakazi wa jimbo hilo la uchaguzi, basi waruhusiwe kupiga kura. Ndiyo maana CDM iliibuka na ushindi.

Pichani Balozi wa Nyumba Kumi katika Kijiji cha Mwayunge Mashariki, Kata ya Igunga mkoani Tabora, Nghoboko Masele, Akiwa chini ya ulinzi baada kukamatwa na wafuasi wa chadema na shahada za kupigia kura pamoja na orodha ya majina ya wapiga kura aliyodaiwa kukutwa nayo.

SOURCE:Wizi wa Kura Igunga: Sura Mbaya Ya CCM - Tanzagiza
 
07kurabalo.jpg

Cheki hiyo pozi, kweli CCM wameishiwa yaani hiyo Igunga utafikiri uchaguzi wa uraisi!!!!!!!!! Yaani huyo jamaa anaonekana hata jero unamnunua hahaha ahahah!!!!!!

Njaa mbaya sana, hebu angalia hilo mbwiga la CCM kama msukule vile
 
Huyo mzee aliisha achana na ubalozi siku nyingi na si kada tena wa CCM.Huu ni ujanja wa CDM kutaka kujisafisha kwa kitendo cha aibu walichomfanyia DC.Watu wa Igunga wanajua ukweli labda wadanganyeni watu wa Arusha na K'njaro.
 
Alikuwa anafanya njama kwa ajili ya kusaidia ushindi wa chama gani?
 
Huyo mzee aliisha achana na ubalozi siku nyingi na si kada tena wa CCM.Huu ni ujanja wa CDM kutaka kujisafisha kwa kitendo cha aibu walichomfanyia DC.Watu wa Igunga wanajua ukweli labda wadanganyeni watu wa Arusha na K'njaro.

Uko Igunga? Mbona unajazba sana? Source ya kwamba alishaachana na ubalozi? Na kwamba si kada wa CCM tena? Ukiachana na ubalozi ni lazima uhame na chama? Kwa nn unaihusisha CDM na Arusha na K'manjaro? Huoni ni km unaihusisha CCM na mikoa iliyobaki? Huoni km huo ni ujanja wako wa kuisafisha CCM na ni umamluki unaouonyesha kwa kiwango cha juu sana?
 
Ni umbumbumbu wao tu hawa kukubali kuuza shahada/utu wao mbona mtu mwenyewe anaonekana kachoka mpaka basi!anajiuza kwa tsh elf10 na ubwabwa then kesho hali ngumu vile vile
 
Wamemaliza kuwahonga wali, sasa wanamaliza kwa kuchukua shahada zao.
 
Huyo mzee aliisha achana na ubalozi siku nyingi na si kada tena wa CCM.Huu ni ujanja wa CDM kutaka kujisafisha kwa kitendo cha aibu walichomfanyia DC.Watu wa Igunga wanajua ukweli labda wadanganyeni watu wa Arusha na K'njaro.

Wanatafuta sababu za kumaliza visigino baada ya matokeo kutangazwa.
 
Huyo mzee aliisha achana na ubalozi siku nyingi na si kada tena wa CCM.Huu ni ujanja wa CDM kutaka kujisafisha kwa kitendo cha aibu walichomfanyia DC.Watu wa Igunga wanajua ukweli labda wadanganyeni watu wa Arusha na K'njaro.
<br /> <br / ala KUMBE KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA KAHARISHA
 
Uko Igunga? Mbona unajazba sana? Source ya kwamba alishaachana na ubalozi? Na kwamba si kada wa CCM tena? Ukiachana na ubalozi ni lazima uhame na chama? Kwa nn unaihusisha CDM na Arusha na K'manjaro? Huoni ni km unaihusisha CCM na mikoa iliyobaki? Huoni km huo ni ujanja wako wa kuisafisha CCM na ni umamluki unaouonyesha kwa kiwango cha juu sana?
<br />
<br />
mkuu huyo katumwa na nepi kukamilisha kazi. Hebu angalia alivyotoa hoja za ki-mkufunzi wao TAMBWE HIZO ambazo NEPI anazitumia sana siku hizi
 
Huyo mzee aliisha achana na ubalozi siku nyingi na si kada tena wa CCM.Huu ni ujanja wa CDM kutaka kujisafisha kwa kitendo cha aibu walichomfanyia DC.Watu wa Igunga wanajua ukweli labda wadanganyeni watu wa Arusha na K'njaro.
acha hizo wewe tunajua hiyo ni kawaida ya MAGAMBA!
 
Back
Top Bottom