Mbunge Kikwete agawa bima za afya kwa mabalozi Chalinze, asisitiza kuwapa kipaumbele

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora amewakumbusha viongozi na CCM -Halmashauri ya Chalinze kuwapa kipaumbele Mabalozi katika kazi za kila siku zinazofanywa na fursa zinazojitokeza ili kuwatambulishaU umuhimu wao katika kazi na ustawi wa Chama.

Maneno hayo ameyasema alipokuwa akiongea na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata ya Msoga kwenye mkutano Mkuu maalum wa kupokea taarifa ya miaka Mitatu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kata hiyo.

Katika kikao hicho ambapo pamoja na kupokea Ilani, Ndg. Mbunge aliwagaia Mabalozi 180 wa Kata ya Msoga kadi za Bima ya Afya kwa ajili ya kupata huduma ya afya pale inapotokea hitaji la matibabu, aliwaasa kutambua umuhimu wao na kuwaasa kuwa haya yanayofanyika ni kwa ajili ya kuwaimarisha wakitumikie Chama Chao na kuwa Chama kinawajali.

Akimshukuru Mbunge wa jimbo hilo, Diwani wa kata ya Msoga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze alimuhakikishia Mbunge kuwa Chalinze ususani kata hiyo itqendelea kuwa ngome ya CCM na kwamba wamejipanga kwa ajili ya ushindi katika chaguzi zote mbili wakianza na hii ya Serikali ya Mtaa 2024 na baadae ule Mkuu wa 2025.

FB_IMG_1708651694237.jpg

#KaziInaendelea #MikutanoMrejesho
 
Kwa nini hadi wagawiwe hizo bima za afya?

Kwani hawawezi wao kufanya maombi kwenye taasisi husika na kupata hizo bima za afya?

Je, kuna shida kwenye mfuko wa bima ya afya kwa waombaji wapya?

Kugawiwa bima naitafsiri kama ni takrima na vitu kama hivi vinafanyila kisiasa target ikiwa ni chaguzi...

Maana kuna mtu kaingia mfukoni hapo...
 
nachompendea huyu mzee ni kupuuza wapuuzi na yeye kundelea na maisha yake...yale maneno ya wapuuzi juu ya usaliti wake kwa Lowassa ingekuwa mzee goi goi angeshapata stroke saa hizi,lkn chuma hicho kinaendelea na yake
 
Ila hili swala la viongozi wa ccm kuendekeza kuwaridhisha watoto wao madaaraka linaweza kuja kuleta chuki sana huko mbeleleni tena ndani ya ccm
 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora amewakumbusha viongozi na CCM -Halmashauri ya Chalinze kuwapa kipaumbele Mabalozi katika kazi za kila siku zinazofanywa na fursa zinazojitokeza ili kuwatambulishaU umuhimu wao katika kazi na ustawi wa Chama.

Maneno hayo ameyasema alipokuwa akiongea na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata ya Msoga kwenye mkutano Mkuu maalum wa kupokea taarifa ya miaka Mitatu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kata hiyo.

Katika kikao hicho ambapo pamoja na kupokea Ilani, Ndg. Mbunge aliwagaia Mabalozi 180 wa Kata ya Msoga kadi za Bima ya Afya kwa ajili ya kupata huduma ya afya pale inapotokea hitaji la matibabu, aliwaasa kutambua umuhimu wao na kuwaasa kuwa haya yanayofanyika ni kwa ajili ya kuwaimarisha wakitumikie Chama Chao na kuwa Chama kinawajali.

Akimshukuru Mbunge wa jimbo hilo, Diwani wa kata ya Msoga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze alimuhakikishia Mbunge kuwa Chalinze ususani kata hiyo itqendelea kuwa ngome ya CCM na kwamba wamejipanga kwa ajili ya ushindi katika chaguzi zote mbili wakianza na hii ya Serikali ya Mtaa 2024 na baadae ule Mkuu wa 2025.

#KaziInaendelea #MikutanoMrejesho
Hii ni rushwa dhahiri
 
Back
Top Bottom