Maaskofu Tanzania watoa Tamko, wakemea udini, ukanda na ukabila!

Askofu Shao wa KKKT anatoa tamko la jumuiya ya Wakristo Tanzania.
-Amesema hakuna mfumo kristo
-Asilimia 90 ya viongozi wa JMT ni waislam
-Asilimia 100 ya viongozi ZnZ ni waislam na si kweli kuwa hakuna wakristo wenye uwezo wa kuongozo Zanzibar
-Tume ya mabadiliko ya katiba 2/3 ni waislam
-Mwafaka (MoU) kati ya serikali na kanisa serikali irudishe hosptal na shule kwa wamiliki wa awali(Makanisa na Misikiti) na Ifute MOU na kama haiwezekani serikali itoe tamko la umuhimu au ubaya wa MoU
-Vyombo vya habari vinavyokashifu ukriso vidhibitiwe na Serikali itoe tamko la usalama wa wakristo.

Hiyo statement imeenda shule kuliko maelezo! Majibu ya Serikali yanasubiriwa kwa hamu kubwa na natumaini watafanya haraka iwezekanavyo bila kukawia ili kuondoa kadhia hii ya MoU kwa kitu walichokiomba wao (serikali).

Halafu cha ajabu CCM inaeneza udini utadhani wanachama wao sio miongoni mwa dini hizo zinazochochewa! Hakika hakuna kitu kibaya kama kukosa maarifa.
 
Kuongelea udini ndio jambo baya zaidi kuliko udini wenyewe.

Mtu yeyote anaependa kuongelea udini ni lazima awe mfuasi wa udini.
 
Mfumo kristo ni kiini macho ni Mradi wa kuvuruga Amani Tanzania,Kuna watu wanatajirikia au wanalipwa kwa Kubwabwaja au kupayuka MFUMO KRISTO.
 
Mleta huu uzi ni mnafiki sana kwenye heading ametaja ukanda na ukabila lakini kwa ni sehemu ya mfumo wa itikadi yao anapata kigugumizi kuvitaja vitu hivyo.
 
Tunahaja ya kumomba sana Mungu,manake alilosema askofu tukubali linainyemelea nchi hivyo hatuna budi kuiombea nchi watu watendewe Haki,usawa na huku wakitimiza wajibu wao
Mungu ibariki Tanzania
 
AshaDii kama vile umewah kusoma biblia.
ngoja nikupe mfano wa kisa cha kweli kwenye biblia, mfalme wa Israel Yehoshefati aliwah kupata waraka toka kwa wafalme ambao ni Moabu, wameuni na amoni walikuja kupigana na Yehoshefati. sasa walikuja wajumbe kumletea ujumbe kwamba wanakuja watu kupigana na wewe. yehoshefati alichofanya alisimama madhabahuni pa bwana na kumwadhimisha Mungu akamsihi Mungu awasikie mabaya yasiwapate na awaokoe na upanga wa adui. basi Mungu toka patakatfu pake alisikia akamwambia nendeni mbele yako msibebe silaha ila muimbe na kusifu mtauona waokovu wangu. basi waliiskia sauti ya Mungu waakenda mbele kwa kuimba na kusifu wale maadui wakapigana wao kwa wao hadi wakauana na kupotea hakuna mwisrael aliyeuwawa ama kauumizwa.

sasa kwa mantiki hii napata hisia kwamba sio kwamba waisam ndio maadui zetu bali kikundi cha wahuni fuan ambacho sasa wakristo walipaswa waende mbele za Mungu kwa sala na kusifu Mungu awaondoe wale adui zetu katikati yetu. ila haya wanayoyasema ni kuita uchochez utaona kesho utaskia waislam wakitoa tamko juu ya hili.
nenda soma 2nyak20:1-19. utaelewa ninachomaanisha

AshaDii umesema vyema nami nimelisikia tamko labda nikuulize, nani mwenye jukumu la kuilinda amani ya hii nchi? Sababu ata waislamu wamekua wakitoa matamko pia, je ni kosa kwa viongozi wa kikristo kujibu hoja dhidi ya upotoshwaji unaoenezwa na kikundi cha waislamu kwamba hii nchi inaongozwa katika mfumo kristo? Nadhani truth is what will set us free, kuna mambo mengi yanafunikwa ili mwanaharamu apite yet still anarandaranda hapiti naona Tamko ni sahihi at last tumejua kuna mpasuko then we have somewhere to start ndio principle za mediations all side should confess that there is a problem sasa huwez sema issue ya udini haipo na maneno ya kisiasa kuna amani but in the ground kuna tatizo I think it is a high time tukae katika round table wakristo na waislamu haswa viongozi wajadili hii mipasuko then we can start over maisha bila vinyongo! Sikubali upotoshaji kwamba nyerere did nothing katika hili taifa na kusema alibeba wakristo kizazi kitakachokuja kikikaririshwa hivi nakwambia historia ya nyerere itapotezwa! Serikali inakua na unafiki wa hali ya juu kama itazidi kuwa kimya katika hili
 
Last edited by a moderator:
Walisema kuwa watavumilia lakini uvumilivu unamwisho! Kama nchi inaongozwa na waislamu na bado waislamu wanalia kwamba ni mfumo Kristo, wanataka iwe dola ya Kiislamu ili waridhike? Maana mara zote madai ya waislamu kuhusu mfumo Kristo yanapotelewa serikali haijawahi kukanusha! Na kumbuka asiye kinyume nao yupo pamoja nao
 
2015 raisi lazima awe mkiristo basi ebo! Mwnyi/ kikwete wameshndwa mkapa aliweza tamko la maaskofu saaafi sana .
 
Sioni chochote hapa zaidi ya ubabaishaji!
Serikali ipo kimya kwa muda mrefu, kwanini Kanisa lisichukue hatua kwa upande wake kuelezea umuhimu au ubaya wa MoU, au kwanini Kanisa lisisitishe MoU?..kulikuwa na thread nzima hapa kuhusu hili.

ombi la kurejesha taasisi zilizochukuliwa na serikali kwa wenyewe litatusaidia, tutaheshimiana. MoU ivunjwe kama wanavyopendekeza hawa wakristo. labda tutagundua tofauti ya misaada ya tende, nyama ya ngamia, majambia na vifaa vya hospitali, shule, maabara n.k
 
lakin bado mm nina maswali mengi kichwan mwangu,
je kwann hadi maaskofu waseme haya?? je ni kwamba hawana imani na hali ya amani iliyopo?? ni kwamba kuna kuonewa ambapo wamekuona ama ni nini?

je hivi kama wakristo wakikaa kimya wasijibu hoja hata moja ingekuwaje ama wasitoe tamko?? na je hivi mungu wa kikristo huitaj mtu kumtetea hadi wakawajibu waislam hoja zao??

Binafsi Askofu wangu Martin Shao hukukaa rohoni. Simbezi ila kwa wanaonielewa watanielewa tu, alichopaswa kusema ni kwamba sasa wakristo tukaze goti tusali Mungu aliye juu ya yote atajidhihirisha kwa wakati wake. tena angesoma habari za yehoshafati wala asingepotez muda kuongea hayo bali angeikabili madhabahu kwa sala za kumwita Mungu aonekane kwa wakati anaotaka.

Mkuu umelisikia tamko lao hadi mwisho na nini wakristu tunapaswa kufanya mwishoni mwa tamko hilo la jumuiya za kikristu ni kwamba wakristu kujilinda kwetu ni kufunga na maombi tu nguzo kuu itakayosaidia kututoa hapa tulipo na si kulipa kisasi..
 
Hatua waliochukua sii mbaya... Ila inakuwa kama kurudisha nyumba na kuchochea kuni ambazo zilikuwa zimeanza kupoa. Ni wazi kuwa udini sasa upo; lililobaki ni kutafuta suluhu badala ya kujenga hoja na habari ambazo zinaamsha tena hisia 'hasi' za waumini na wasio waumini kwa makundi makuu husika. Hayo maubiri in a way yanakuwa yanasema kama vile "we have the right to get angry" na haijakaa kiusuluhishi; litafanya kila muumini awe right kuona mtazamo wake alio nao wowote ule (uwe wa kujenga ama kubomoa) uonekane ni sawa.

La msingi ilitakiwa atoe kile ambacho anaona ni njia mbadala ya kutatua matatizo... Ilikuwa sio wakati wa kuya 'pronounce' for tayari ilishafanyiwa hivo.

mkiambiwa idhibitini redio imani hamsikii, magazeti ya kiislam yanaandika baadhi ya mambo kwa mtizamo wa kibaguzi na uchochezi kabisa, RAIS wetu naye analalamika, sijui anaogopa kusomewa albadiri!
 
ombi la kurejesha taasisi zilizochukuliwa na serikali kwa wenyewe litatusaidia, tutaheshimiana. MoU ivunjwe kama wanavyopendekeza hawa wakristo. labda tutagundua tofauti ya misaada ya tende, nyama ya ngamia, majambia na vifaa vya hospitali, shule, maabara n.k
Wanapendekeza? kitu gani kinachowazuia kujitoa katika makubaliano?
 
Back
Top Bottom