Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu Tanzania watoa Tamko, wakemea udini, ukanda na ukabila!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yericko Nyerere, Dec 25, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Dec 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 14,648
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 113
  Jukwaa la jumiya ya kikristu leo imetoa tamko kuhusiana na mwenendo wa amani nchini, hasa likijikita kuelezea machafuko yaliyoongozwa na kuratibiwa na baadhi ya makundi ya kiislamu nchini.

  Moja ya mambo yaliyotolewa ni kukanusha kuwa NCHI hii haiongozwi kwa mfumo kristu, na zaidi imefafanua kuwa:

  Rais ni muislamu, Makamu wa rais ni Muislama, Mkuu wa jeshi la Polisi, ni Muislamu, Jaji mkuu ni Muisla, Mkuu wa usalama wa Taifa ni Muislamu,

  Na kwa upande wa Zanzibar 100% ya viongozi wa serikali ni waislamu, na sikuwa kule Zanzibar hakuna wakristu wenye sifa za kuwa viongozi!

  Akisoma maadhimio hayo kiongozi wa kiroho wa ukanda wa Kilimanjaro Dr Martin Shayo amezidi kusisitiza kuwa Jumuiya ya Kikristu inafikiria kuiomba serikali izirejeshe huduma za kijamii zilizokuwa chini ya makanisa hayo zinazoendeshwa na serikali ili na waislamu nao waweze kuendesha huduma hizo!

  Ameiomba serikali kutoyafumbia macho mambo yanayohatarisha umoja wetu,
   
 2. K

  KIBE JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Leo makanisa yamefunguka wamechoka na serikali kufumbia macho uchomaji wa makanisa....
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 21,239
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 63
  Nimepote njia nikatokea TBC nimekuta ibada kuna hotuba inawachana CCM na waislam na propaganda zao mbaya sana.

  Huyu Mhubiri na guts sana. Atatoa data na ujumbe kwa CCM sasa waseme mambo hadharani
   
 4. englibertm

  englibertm JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2012
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 7,927
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 48
  hawa sio katoliki ni kkkt
   
 5. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,490
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 48
  Wafanye hivyo kwa ustawi wa nchi na watu wake
   
 6. M

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 16,410
  Likes Received: 708
  Trophy Points: 113
  Askofu Shao wa KKKT anatoa tamko la jumuiya ya Wakristo Tanzania.
  -Amesema hakuna mfumo kristo
  -Asilimia 90 ya viongozi wa JMT ni waislam
  -Asilimia 100 ya viongozi ZnZ ni waislam na si kweli kuwa hakuna wakristo wenye uwezo wa kuongozo Zanzibar
  -Tume ya mabadiliko ya katiba 2/3 ni waislam
  -Mwafaka (MoU) kati ya serikali na kanisa serikali irudishe hosptal na shule kwa wamiliki wa awali(Makanisa na Misikiti) na Ifute MOU na kama haiwezekani serikali itoe tamko la umuhimu au ubaya wa MoU
  -Vyombo vya habari vinavyokashifu ukriso vidhibitiwe na Serikali itoe tamko la usalama wa wakristo.
   
 7. s

  sad JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 293
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  suala linalo isumbua nchi kwa sasa ni udini sio ukanda. dini ya kikristo na kiislamu. wapagani, wabudha na wahindu wao hawahusiki. hoja ya ukada ni ya kisiasa. na hata udini wameasisi c.c., na baadhi ya watu wakaupokea bila kujua kwamba ni malengo ya kisiasa ili kuwagombanisha wanachi au kuweka chuki.
   
 8. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 12,578
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 63
  Hayo ndo nayaogopa mimi!
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 41,003
  Likes Received: 2,377
  Trophy Points: 113
  Tunapoelekea hii nchi tutaigawana vipande vipande.
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Dec 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 41,003
  Likes Received: 2,377
  Trophy Points: 113
  Udini tayari upo wazi hakuna tena kujificha kama viongozi wa dini wameamua kuongea haya basi tena tujiandae na lolote litakalotokea.
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 21,239
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 63
  wiki hii si yako Lema kakushika, ben Saa 8 kakushika, sasa Maaskofu wanakushika umesoma data hizo?Si ulikuwa busy sana na MOI.?Hii ndiyo Misa ya Al-Masih(Christ Mass). nadhani umefunguka kiakili kiasi fulani.
   
 12. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sioni chochote hapa zaidi ya ubabaishaji!
  Serikali ipo kimya kwa muda mrefu, kwanini Kanisa lisichukue hatua kwa upande wake kuelezea umuhimu au ubaya wa MoU, au kwanini Kanisa lisisitishe MoU?..kulikuwa na thread nzima hapa kuhusu hili.
   
 13. m

  mtendaji wa kijiji JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 500
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 18
  J.k muasisi wa Udini na serikali yako ya sisiem hayo ndo mliyataka . 2010 kwenye compaign mlizunguka Tz nzima mkahubiri kuwa cdm ni cha wa kristo sasa mtaona matokeo yake
   
 14. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,084
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 38
  Mbona hizo takwimu ktk makanisa ya RC sijazisikia? Hapo ndo huwa nawapa big up RC
   
 15. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,327
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 36
  Udini nje nje tunasubiri mashehe nao watoe tamko lao
   
 16. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 21,239
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 63
  Zawadi kwa Ritz,Mkandara, sideeq, Zitto, na wengine waliokuwa na tongotongo, kila mstari ni mavu na pure.
   
 17. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #17
  Dec 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,205
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 63
  Hatua waliochukua sii mbaya... Ila inakuwa kama kurudisha nyumba na kuchochea kuni ambazo zilikuwa zimeanza kupoa. Ni wazi kuwa udini sasa upo; lililobaki ni kutafuta suluhu badala ya kujenga hoja na habari ambazo zinaamsha tena hisia 'hasi' za waumini na wasio waumini kwa makundi makuu husika. Hayo maubiri in a way yanakuwa yanasema kama vile "we have the right to get angry" na haijakaa kiusuluhishi; litafanya kila muumini awe right kuona mtazamo wake alio nao wowote ule (uwe wa kujenga ama kubomoa) uonekane ni sawa.

  La msingi ilitakiwa atoe kile ambacho anaona ni njia mbadala ya kutatua matatizo... Ilikuwa sio wakati wa kuya 'pronounce' for tayari ilishafanyiwa hivo.
   
 18. m

  mtendaji wa kijiji JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 500
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 18
  J.k muasisi wa Udini na serikali yako ya sisiem hayo ndo mliyataka . 2010 kwenye compaign mlizunguka Tz nzima mkahubiri kuwa cdm ni cha wa kristo sasa mtaona matokeo yake
   
 19. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 8,919
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 83
  Hao watumishi wa idara za serikali na mahakama anaowataja tayari walishakuwa viongozi waandamizi kwenye idara husika kabla ya rais Kikwete hajaingia madarakani.Kwa mtazamo wangu ni yeye huyo muhubiri ndio mdini na leo hii amemua kuonyesha ulimwengu kuwa nchi hii ni mfumo kristo kwa kutopenda kuona waislam kwenye nafasi za uongozi.
   
 20. K

  Karibuni masijala JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Akisoma tamko hilo kwa niaba ya Wengine Askofu Dr Martin F. Shao kwenye Ibada ya Taifa ya Christmass inayorushwa na TBC Kwaniaba ya Jukwaa la Kristo Tanzania amedai

  1.Waislamu wanaeneza kashfa dhid ya Wakristo kwa kutumia chombo cha habari na kwa kutumia DVD, CD, KANDA, Mihadhara huku Serikali ikiwa Kimya bila kuchukua hatua ina maana inakubaliana nayo kwanini serikali iko kimya?

  2. Kuhusu kuchoma Quruan jambo hilo linafanywa na waislamu wenyewe akatoa mfano ilitokea huko Zanzibar

  3. Kuchoma makanisa Wakristo wachukue tahadhari maana Serikali si mbagala tu ilikuwa kimya wakadai hawakujua wakati waliambiwa.

  4. Momerandamu wamesema walingia ubia kuendesha shule na afya na Serikali kama wanadai wanapendelewa serikali ijitoe izirudishe au izichukue. Kwanini hawalitolei ufafanuzi jambo hili wako kimya kashfa zinasamba

  5.Madai ya waislamu nchi inaongozwa Kikristo wamesema ni 1 ya kashfa katiba hairusu.Pia wametolea mfano kwa kutaja Raisi,makamu,mkuu usalama,Jajimkuu na Zanzibar100% Waislamu
  Wana Jamvi Hapo vp?
   

Share This Page